ASKARI WA JANGWANI

na Tony Alamo

Malaika wa BWANA akasema na Filipo, akamwambia, “Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa” (Matendo 8:26).

Mhubiri Filipo akaelekea Samaria, Akiwa huko uvuvio ukatokea, uvuvio huo uliambatana na nguvu ya miujiza. Wagonjwa waliponywa, pepo walikemewa, utukufu wa BWANA ukaonekana, na mji mzima ulitekwa na mahubiri ya Filipo. Filipo alikuwa kwenye upeo wa huduma ya kimitume na MUNGU alitembea kupitia kwake. Basi usiku mmoja MALAIKA wa BWANA aliongea naye na kumwambia, “Amka ujitayarishe, uache kazi unayofanya na ushuke kwenda Gaza jangwani.” Nadhani Filipo alijiuliza maswali mengi moyoni mwake kulingana na maelekezo aliyopewa, kwamba aache kazi ya utume aliyokuwa akiifanya. Kuacha kazi ya MUNGU? Kuacha kazi njema ya kutangaza nguvu za MUNGU na kushuka jangwani? Hakuna maji wala chombo cha kurekebisha hali ya hewa jangwani. Hakuna mikahawa ya McDonald au Colonel Sanders. BWANA sipendi jangwa; napenda kubaki hapa katika uvuvio. Uvuvio unanihitaji. Nguvu za MUNGU zinatawala hapa, uvuvio unaendelea, roho zinaokolewa, Ninahitajika hapa!

Basi, Filipo akaanza safari yake kupitia Yerusalemu katika njia kuu iendayo pembezoni mwa pwani ya Mediterania na Afrika ya Kaskazini. Wakati alipokuwa akitembea barabarani alikuwa akisali. “Naam sasa, BWANA nimefika hapa. WATAKA nifanye nini?” Na alipotazama akaona magari ya kifahari ya kipindi hicho – Tajiri akiwa kwenye gari la farasi, akiwa amevalia mavazi ya kifalme. Alikuwa akisoma chuo cha nabii Isaya, baada ya kumwona Filipo, akaamuru gari kusimama, na kumualika Filipo karibu yake. Basi Filipo alimsogelea yule tajiri, akamkuta anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, “Je! Yanakuelea haya unayosoma?” (Alikuwa akisoma sura ya 53 ya chuo cha Isaya iliyomwongelea BWANA YESU KRISTO.) Akajibu, “Nitawezaje kuelewa mtu asipo niongoza?”

MUNGU alimtuma Filipo kumweleza yule mtu habari ya maandiko yale. Basi mtu yule aliamini, akaokoka, na kubatizwa, yote yalifanyika siku iyo hiyo. Historia inatuambia kuwa mtu huyu alikuwa kwenye mamlaka ya juu, katika hazina ya Ethiopia, aliyerudi Ethiopia akaeneza NENO la MUNGU kwa watu wa mahali pale na kuanzisha Kanisa (Kanisa ambalo mizizi yake ipo mpaka leo, na hii ni kwa sababu Filipo alikuwa mtii wa NENO la MUNGU na kushuka jangwani).1

Watu wengi wa MUNGU wamekuwa wakitumwa jangwani.2 Hili ni swala ambalo kila mmoja wetu angependa kuepukana nalo kwa namna yoyote. Hatujisikii vizuri pale MUNGU anapoingilia ratiba zetu na kusema “Nataka ushuke jangwani.” Lakini katika maisha yoyote ambayo MUNGU anatumia lazima kuwe na uzoefu wa jangwa. Katika uzoefu wa Filipo, MUNGU alimuhudumia; alichukuliwa katika ROHO na kutolewa jangwani hata pembezoni mwa bahari kwa nguvu za kimiujiza za MUNGU.

Uzoefu wa jangwa ni lazima katika maisha ya watu wa kweli wa MUNGU.3 Mungu hachagui kusanifisha vyombo vyake safi kwenye mji, bali jangwani. Unaweza kumtambua mtu aliyeko jangwani kwa sababu mara kadhaa utamsikia akisema, “Nahisi ukame, naziona mbingu kama chuma kwangu, na sielewi kwa nini haya yote yananitokea mimi.” MUNGU anakupa uzoefu wa kuishi jangwani. Tunapenda kufanya huduma za kiroho, kujitolea na kusaidia, ni vema. Tunapenda sana kuwa kati ya watu wengi. Tunapenda kuendelea, Lakini MUNGU anatuambia, “Kijana (au binti), nataka uje pembeni. Nataka nikutoe kwenye halaiki ya watu. Nataka nikutenge. Nataka nikuweke peke yako, hapa nje chini ya nyota kwenye sehemu ya upweke, mahali ambapo naweza kuongea nawe. Nataka Kuchomelea  NENO LANGU ndani ya roho yako ya milele.4 Nataka kuweka ujumbe WANGU kinywani mwako.5 Nataka kuingia ndani vilindini mwa nafsi yako, Nataka nikutumie.”6 Na hili ni swala ambalo mara nyingi hatujajiandaa kufanya. Tunalalamika, “Sipendi sehemu pweke. Ningependa kuzungukwa na watu. Ningependa watu wajue ninachokipitia. Ningependa watu wanionee huruma. Ningependa watu wanielewe. Ningependa faraja ya watu wengine.” Lakini MUNGU anasema, “nitakuweka kwenye jangwa, na kama unanipenda MIMI na kuamini NENO langu, utakwenda jangwani. Nakupeleka huko ili nikutane na wewe, peke yako, jangwani.”

Hebu tuzungumze kuhusu jangwa. Namshukuru MUNGU kwamba vipo vijito vya maji. Namshukuru MUNGU kwa vilele vya milima. Lakini pia namshukuru MUNGU kuwa katika maisha ya kila mwanaume na mwanamke anayeitwa Mkristo, kuna ahadi ya mwisho kwetu. Kila mmoja atakaye kuja na ujumbe uchomao nafsi, na kila nabii aliye na ujasiri wa kusimama mbele ya taifa na hata ulimwengu, basi huyo ni mtu ambaye MUNGU amempeleka kwenye sehemu pweke – jangwani – sehemu pweke – sehemu ya kiza nene – sehemu isiyo nyevu – hiyo ni sehemu ambayo MUNGU anaongea na kuvunja na kuunda na kutengeneza na kujenga.7 Basi MUNGU anaweza kumtuma mtu huyo kutoka kwenye jangwa na maji yapeanayo uhai na ujumbe wa wokovu wa mbinguni.

MUNGU alipomuita Musa, alikuwa na umri wa miaka minane. Alimwezesha Musa kupokea Elimu na kuishi kama mwana wa mfalme.8 Kwa muda wa miaka arobaini amekuwa akisubiriwa na kulishwa. Alioga kwenye maji ya vijito vya mto Nile huku watumishi wake wakimsubiri. Alivaa nguo nadhifu na kusherehekea  vyakula vya kifalme kwenye meza ya Farao akijifunza utamaduni wa Wamisri. Siku moja, MUNGU akamwambia Musa, “Sehemu ya kwanza ya elimu yako imekwisha, na sasa nina mkutano   muhimu sana nawe.” MUNGU akamchukua hadi sehemu ya nyuma ya jangwa.9 Kwa miaka Arobaini mingine alitembea jangwani ngozi yake ikaungua kwa jua, na macho yake yakawa mekundu kwa sababu ya changarawe, mpaka MUNGU alipotimiza kazi yake ya kuifanya roho ya Musa kulizoea jangwa.10 Sasa MUNGU alikuwa tayari kukutana na Musa. Maisha yake yaligawanywa katika sehemu tatu za miaka arobaini kila moja; Miaka arobaini Misri, Miaka arobaini jangwani, na miaka arobaini katika hukumu; na alipewa sheria kwa Israeli na kwa dunia.

Musa alikuta kichaka kiwakacho kwenye sehemu ya nyuma ya njangwa.11 Alisikia sauti ya BWANA, akatii, akarudi na moto wa unabii na utukufu wa MUNGU katika moyo wake.12 Aliongoza kati ya Waisraeli milioni mbili hadi tatu toka utumwani, akifanya ishara kubwa na maajabu na miujiza – kwa sababu alikutana na MUNGU jangwani.13

Ikiwa unawaendea watu wa MUNGU kwa ishara na maajabu na miujiza, na kubeba fimbo itakayoleta ukombozi, basi kuna kichaka cha MUNGU kinachowaka katika jangwa lake kwa ajili yako, kitu ambacho ni lazima ukutane nacho kwanza. Usidhani kwamba yupo mtu atakayekuita kutoka katika umati kanisani na kukuwekea mikono na kukugawia huduma ambayo itawatoa wanaume na wanawake kwenye upofu na utumwa. Usidhani kuwa utaenda shule ya Biblia na kutunukiwa Shahada itakayokuwezesha  kuwaokoa watu. Kama unataka kuwatoa watu kwenye utumwa wa Misri, basi unahitaji kuonana na MUNGU kwenye sehemu ya nyuma ya jangwa. MUNGU atakuondolea raha zote, atakuondolea starehe zote, atakuchukulia vitu vyote ulivyopendezwa navyo, atakupeleka mbali na watu, na katika ROHO WAKE, atakupeleka mahali ambapo utakuwa wewe na MUNGU peke yake. Kila nabii wa kweli wa MUNGU, kila askari wa BWANA, na yeyote anayetarajia kutimiza malengo ya MUNGU ni lazima akutane na Muumba wake kwenye sehemu ya nyuma ya jangwa.

Yusufu, njoo na utoe ushuhuda. “Mimi ni mtoto wa kumi na moja kwa baba yangu.14 Nimekuwa na ndoto na maono ya kiroho,15 na  nilijua nina mkutano na MUNGU; lakini nilikuwa nikiishi katika sehemu ya upweke. Watoto wa baba yangu, kaka zangu, walinidharau.16 Niliishi kama mtu aliyetelekezwa kwenye nyumba ya baba yangu.17 Mimi ndiye nilitupwa kizuizini na kwenye huzuni ya jela.”18 Yusufu, unawezaje kuishi kama mtoto wa mfalme katika nchi? Je! Unao uzoefu wa jangwani? “Hakika, nilihitimu mahitaji ya kumfanyia MUNGU kazi nikiwa kwenye gereza la Farao.” Wapi ulijifunza usawa na kusamehe? Ulijifunzia wapi huruma dhidi ya wanadamu wengine? “ Nilijifunza wakati nikilia kwenye dimbwi la upweke ndani ya gereza la Farao. Hapo ndipo nilipojifunza huruma ya MUNGU.”

Yohana, unawezaje kuwa na lugha ya kushawishi kiasi hicho? Yohana, unawezaje kushawishi halaiki yote hii ya watu kufanya toba? Yohana, ni jinsi gani umepata moto na nguvu hizi na shauku ya namna hii maishani mwako, kiasi cha kushawishi taifa kwa mahubiri yako dhidi ya dhambi? “ Niliondoka nyumbani kwa baba yangu nikiwa kijana mdogo nilienda kuitikia wito wa ROHO MTAKATIFU, na kuishi jangwani.19 Nilivaa mkanda wa ngozi, na nilikula asali na nzige,20 na nikakutana na BWANA MUNGU kwenye jangwa. NENO la MUNGU likaniingia moyoni mwangu, na nikatoka jangwani nikiwa na bidii na utukufu wa MUNGU moyoni mwangu. Ni kipindi hicho pekee niliweza kuhubiri kwa watu juu ya toba na kuwafanya watu wamwabudu.

Baada ya Paulo kubadilishwa kwenye njia ya Dameski, alimuhubiri KRISTO kwa muda.21 Kisha akaenda katika jangwa la Uarabuni kwa miaka miwili.22 Maandiko hayatuambii chochote kuhusu miaka hii, lakini alipotelea jangwani kwa muda wa miaka miwili na kuishi maisha ya upweke katika sehemu iliyojitenga. Tangu hapo alirudi akiwa mtume kamili wa MUNGU.

Na hata WEWE, BWANA YESU; WEWE uliyesimikwa kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu kuleta wokovu wa uzima wa milele kwa ulimwengu uliopotea na mauti.23 EWE YESU – uliye BWANA unaenda wapi? Je unakwenda katika hekalu la Yerusalemu kujitangaza kama MASIHI? “Hapana, nimesukumwa na ROHO kwenda nyikani kwa siku arobaini.”24 Na ndani ya siku hizo za kufunga na kuomba, alimthibitishia Shetani nguvu ya NENO TAKATIFU la MUNGU na kutoka jangwani, akiwa amejawa neema na kweli, kutimiza kazi ile iliyomleta kutoka mbinguni.25 Naam, hata YESU MFALME alipitia wakati wake wa jangwani, tena mara nyingi zaidi.

Kila mwanaume na mwanamke ambaye MUNGU amemwekea mikono na kumwita katika huduma ni lazima apitie jangwani kwanza. Ninazungumzia sehemu ya upweke katika maisha yako ya kiroho ambapo MUNGU anakutenga na wengine, kipindi ambacho watu hawakuelewi, hicho ndicho kipindi cha kutumiwa na MUNGU. MUNGU anasema “sitamtuma mtu akuombee ama kukuwekea mikono. Itakubidi ujiombee wewe binafsi.”26 Utaonana na MWENYEZI MUNGU uso kwa uso. MUNGU atakupeleka jangwani ambapo aidha utaelewa mwenendo wako na MUNGU au utakufa. Utamwangukia MUNGU na kulia kwa uchungu mpaka utakapopata kibali mbele za MUNGU. Utatengeneza mahusiano mapya na MUNGU. Na hutajali MUNGU atapokwambia nenda Ninawi, kwa sababu utakuwa kwenye kiti cha enzi cha MUNGU, na utukufu WAKE utakuwa usoni mwako bila kupunguka. Nazungumzia kuhusu mahali ambapo MUNGU atakuelekeza, na utapokea maelekezo YAKE. Sehemu ambayo hutapata faraja ya mwanadamu, mahali ambapo hakuna yeyote anayeelewa unachofanya.

Unafikiri Daudi alipitia hali gani wakati akiwa na watu mia sita na hakuna aliyemwelewa? Alisema “Roho yangu ina kiu ya uhai; MUNGU, umekwenda wapi? Siwezi kuhisi uwepo wako. Nafsi yangu ina kiu ya MUNGU aliye hai.”27 Daudi alikuwa mahali ambapo MUNGU hakuja kuzungumza naye, na akasimamia NENO la MUNGU ambalo lilikua ndani yake. Alilazimika kuwa na imani katika wema na rehema za BWANA, ili MUNGU kwa namna fulani ampitishe kwenye majaribu haya na jangwa la kiroho.28

MUNGU anajaribu kuwakuza watu waume na wake. Unasema, “MUNGU aliniita kutabiri.” Oh! Alikutuma? Kweli?  Kwanza ngoja nione changarawe kwenye viatu vyako. Manabii wa kale walipokuja na NENO la BWANA, wengine walipigwa mawe, wengine walifungwa jela, wengine walitengwa na kuteswa na hata kuuawa.29 Na wewe, unapopata mateso kidogo, unalia na kusema, “Nitarudi nyuma” lakini kama UTAMRUHUSU  na kudumu katika ROHO WAKE, MUNGU atakusanifisha  katika jangwa hilo na kukukuza.

Utakuja wakati kwenye maisha yako ambapo MUNGU atawafungia watu nje na kujifungia ndani akiwa na wewe, nawe utalia, “MUNGU hakuna anayenielewa.” MUNGU atakujibu, “sitaki wakuelewe. Unachotafuta ni bega la kuegemea, nami nataka uegemee bega langu.” Baadhi yenu mpo jangwani hivi sasa, wengine ndio mnatoka jangwani. Mmekuwa na MUNGU, mnaongea na MUNGU, na MUNGU anaongea nanyi. Mmekidhi vigezo vya MUNGU. Mmeipata sehemu ile ya MUNGU ambapo hamtetereki wala kutikisika. Hampepesuki katika maisha yenu ya Ukristo. Mmekutana na MUNGU uso kwa uso na kwa uhalisi. Mmejifunza masomo ya jangwani vizuri. Mnajua namna ya kusali, mnajua namna ya kutunza ahadi ZAKE. Mnajitambua, na mnamtambua MUNGU, hamhitaji uthibitisho wa binadamu, kwa sababu mmesikia kutoka kwa MUNGU MWENYEWE. Hamsikilizi kutoka kwa mwanadamu, bali mnaongea na MUNGU moja kwa moja, naye anaongea nanyi.

“Ondoka na uende jangwani, nina jambo nawe huko jangwani: Mashaka, masikitiko, maumivu ya moyo, mabadiliko.”30 Unaweza ukawa jangwani kimwili, au ukawa kimawazo, au ukawa huko kiroho. Lakini MUNGU anashughulika na moyo wako huko jangwani.

Kwa nini, Filipo, kwa nini unakwenda jangwani? “Kwa sababu kuna mtu huko atakaye uleta Ufalme na hata taifa kwa MUNGU.” MUNGU hakuweki sehemu ya shida kwa sababu hajafurahishwa nawe. MUNGU anaruhusu tu wale bora zaidi kuteseka. Mateso hayapo kwa ajili ya watu wasio na msimamo dhabiti ndani yake, kwa sababu MUNGU hatajisumbua kusaga kitu kingine bali ngano iliyo safi.31

Utajiuliza, “Kwa nini imekuwa rahisi sana kwa wengine, na ngumu sana kwangu?” Imekuwa rahisi kwao kwa sababu MUNGU hakuwataka wasimame kama mti wa mwaloni. “Kwa nini Fulani ana mali nyingi?” Kwa sababu hivyo ndivyo MUNGU alivyowapatia. MUNGU hana imani nao katika mateso. Hawezi kuwaweka kwenye moto kwa sababu wataungua. MUNGU hapotezi tanuru lake la mateso. Kama huna dhahabu rohoni mwako, MUNGU hatapoteza tanuru lake kwa ajili yako. Kama hauna kitu ndani yako kinacholeta maisha matakatifu, MUNGU hatakuletea majaribu wala dhiki. Majaribu na dhiki ni kwa watakatifu wa MUNGU waliobeba NENO LAKE. Beji ya mafanikio ya ukristo ni pale mateso ambayo yalimjia YESU, yanapokujia wewe.

Kila mmoja anapenda kubembelezwa na kusikia watu wakinena yaliyo mema kumhusu yeye. Wang’aa kama taa ya neoni yenye mwanga mkali. Wanataka watu wawapende na kuwawazia mema. Hawataki kusikia watu wakisema, “Usimkaribie huyo. Ni mzushi; yupo kwenye mafundisho yasiyo sahihi.” Lakini MUNGU anasema nini… “Kuwa makini mwanangu, wakati watu wanapoongea mazuri kukuhusu. Hiyo siyo beji ya  mafanikio. Haupo kwenye rekodi ya MUNGU ya tabia nzuri ikiwa kila mtu ananena vema kukuhusu. Lakini wanapokuongelea ubaya na kukutesa na kusema mambo mabaya kwa jina langu kinyume na ukweli, basi furahi na endelea kuishi kwa furaha kwani malipo yako yapo mbinguni.”32 Hivyo basi, inapaswa kuwa kama muziki masikioni mwako pale watu wanapoongea mabaya kuhusu wewe kwa sababu ya jina la YESU.

MUNGU anawatafuta akina Musa na akina Yohana mbatizaji, na akina Yusufu na Debora na Samueli, kwa sababu ulimwengu upo kizani na unahitaji nuru ya uhai. Anahitaji watu waliokwenda nyikani na kukutana naye katika hizo sehemu za siri, katika nyakati pweke, masaa ya maumivu ya moyo, wakati ambao hauwezi kulala na unahitaji kuomba, mahali anakopajua MUNGU pekee, saa ambazo unyevu ni machozi yanayo bubujika kama mto kutoka machoni mwako ukimlilia MUNGU, “MUNGU, nipitishe kwenye jaribio hili, nisaidie niione siku nyingine, usiniache nianguke, MUNGU, nijalie nguvu, nguvu ya ndani, nipate kusimama upya KATIKA ROHO wako. Katikati ya kilio, mahangaiko na uchungu, MUNGU nijalie nguvu ya kusamehe wakati huu. Usikubali haya maumivu yasizidi nikashindwa kusamehe. Nisafishe kwenye damu yako tukufu na unijaze kwa ROHO WAKO.” Umepata uchungu usiku kucha hadi kuona jua likichomoza bila kulala usiku kucha na kitanda kilicho kinyevu kwa sababu ya  machozi na jasho, baada ya kupigana na MUNGU ili kukutana NAYE na kutokea ukiwa umebadilishwa,  kwa sababu MUNGU alisema siku moja “nenda jangwani.”

MUNGU huchagua mashuhuda WAKE, kisha kuwafunza jangwani. MUNGU huwapata watu WAKE kwenye haya Majangwa yakukatisha tamaa. Wakati tabia zako zinapopakwa matope na watu kusema maneno ya uchungu na yasiyo haki kukuhusu wewe. Huoni jinsi MUNGU mwenye haki ANGETAZAMA tu wakati unateswa, lakini alisema, “Nakuita ili uende ukapate uzoefu wa jangwani,” umeomba, na kuomba, mpaka ukaishiwa vya kuomba, na hata  maombi yako yamekuwa Jangwa. Moyo wako unaumia sana kiasi cha kukaa kanisani na kulia. Huwezi kumwona MUNGU katika nyimbo. Huwezi kumwona MUNGU kwa kucheza. Huwezi kumwona MUNGU katika ibada. Umeishiwa na kila kitu. Umefanya kila jema unalolijua, umetoa fungu la kumi na kuamini NENO la MUNGU. Unaangalia salio lako la Benki na kuona una madeni kuliko mapato. Umeeneza NENO la MUNGU kwa watu na kuwa mtoaji kadiri ya uwezo wako, umeonyesha upendo kwa watu, na malipo yako yamekuwa ni maneno makali ya kejeli. Uko kwenye jangwa. Lakini hapo ndipo MUNGU anapokuja, atachoma yote yaliyo rohoni mwako na ambayo yangekuwa mabaya kwako. MALAIKA wa BWANA (BWANA MWENYEWE) anakuja kuzungumza nawe nyikani katika kichaka kiwakacho, Na kusema “unaweza kwenda sasa. Unayo maneno ya uzima wa milele kwa watu WANGU. Unalo neno la tumaini, neno la wokovu.” Hapo ndipo utakapoanza kuwa na shukrani za milele kwa MUNGU kwa kukushughulikia , na unajenga Madhabahu jangwani kwa ajili YAKE. Hutasahau kamwe sehemu ambayo wewe na MUNGU mlionana ana kwa ana. Utaelewa ni nini maana ya kuongozwa na ROHO wa MUNGU kwa ukamilifu na Maji ya Uzima uliyopata yatabadilisha Jangwa kuwa Bustani yenye mazao mengi. Haya yote ni kwa sababu ya Utii kwa MUNGU ukiwa katika jangwa.

MUNGU anasema “Nataka kutembelea watu WANGU. Kilio cha wanadamu kimekuja KWANGU na sina mtu wakumtuma. Sitamtuma Nabii asiye tayari. Sitamtuma muhubiri asiyeongozwa na ROHO. Sitamtuma mtu kuhubiri toba ambaye yeye mwenyewe hajatubu. Sitatuma mtu asiyepitia jangwani”

Kisha unaweza kusema, “MUNGU, sasa ninaelewa kuwa kila kitu kipo kama kilivyo, na sasa ninaelewa kwa nini ULIYAACHA haya mambo yanitokee na hukutuma hata Mvua jangwani, mahali penye upweke, hali ya kukata tamaa, kukataliwa, kukosa, na kutoeleweka, kwani ni WEWE uliyenipeleka pale.

Mwanzo hukuelewa; ukasema, “Kwa nini, nimefanya nini? Nimekosea wapi MUNGU? Kwa nini MUNGU hanifungulii mlango? Kwa nini nipo kwenye hali hii?” Upo hapo kwa sababu MUNGU anamuandaa mwanamume au mwanamke kupeleka ujumbe wa wokovu, upendo, huruma isiyo na mwisho na neema kwa wanadamu. MUNGU atakulinda na utakubali  uzoefu huu wa jangwa. Na utamshukuru MUNGU kwa jambo hilo. Wakati mzuri ambao utawahi kupata ni pale MUNGU anaposhuka chini jangwani, na hapo mbele yako kuna kichaka kinachochomeka, katika ile sehemu ya upweke. Wakati ukiwa na hamu ya kurudi nyumbani, na mwenye uchovu, ghafla MALAIKA wa MUNGU anatokea na unaanza kumshukuru MUNGU kwa mlima wa upweke unaopigwa na upepo. Kisha atakuongoza katika ROHO WAKE kugusa nyoyo za watu, waume kwa wake kwa ukombozi WAKE mkuu wa kiungu.
Anza sasa kwa kusali hii sala kwa MUNGU.

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Haki ya kunakili Agosti 2011 Haki zote zimehifadhiwa World Pastor Tony Alamo ® Tarehe ya Usajili Agosti 2011
SWAHILI—Vol. 13200—Desert Warriors


footnotes:

1. Mdo. 8:26-40 return

2. Mwa. 6:14-22, 12:1-4, 15:1-8, 22:1-18, 1 Fal. 17:1-7, 19:2-4, Yoh. 4:5-8, Mat. 4:1, Rum. 4:16-21, Ebr. 11:7-19 return

3. Zab. 34:18 return

4. Mit. 3:3, Yer. 31:33, Ebr.. 8:10, 10:16 return

5. Zab. 81:10, Yer. 20:9, Mat. 10:19-20, 13:23, Mk. 16:15, 1 Kor. 1:17-18, 21, 2 Tim. 3:16-17, 4:2 return

6. Rum. 12:1, 2 Kor. 5:18-20, 9:8, Flp. 1:6, Ebr. 4:10-16, 13:21 return

7. Rum. 5:3-5, 2 Kor. 12:9 return

8. Kut. 2:1-10, Mdo. 7:22 return

9. Mwa. 2:15-22, Ebr. 11:24-27 return

10. Mdo. 7:29-34 return

11. Kut. 3:2-10 return

12. Kut 3:10-22, Mdo. 7:34-36 return

13. Kut. 4:1-9, 28, 6:13-37, Kur. 7-14 return

14. Mwa. 30:22-24, 37:2-3 return

15. Mwa. 37:5-10 return

16. Mwa. 37:4-11, 17-20, Mdo. 7:9 return

17. Mwa. 37:4-11 return

18. Mwa. 39:6-20, Zab. 105:18 return

19. Mat. 3:1, Lk. 1:13-17, 67-80 return

20. Mat. 3:4 return

21. Mdo. 9:3-22 return

22. Gal. 1:17 return

23. Mat. 13:35, Yoh. 17:24, Ebr. 5:8-9, 9:24-28, 1 Pet. 1:18-21 return

24. Mat. 4:1-2 return

25. Mat. 4:2-11, Mk. 1:12-13, Lk. 4:1-14, Yoh. 1:14 return

26. Mat. 6:6, Lk. 18:1-8, Efe. 6:18, Flp. 4:6, Kol. 4:2, 1 Thes. 5:17, 1 Tim. 2:8, Ebr. 4:16, 11:6, 1 Yoh. 3:22, 5:14-16, Yud. 20-21 return

27. Zab. 42:2, 63:1, 143:6 return

28. 1 Sam. 30:6 return

29. Mat. 5:10-12, 10:16-18, 21-28, 20:18-19, 23:23-39, 24:8-10, 26:1-4, 47-54, 57-68, Lk. 21:12-19, Yoh. 15:18-19, 16:1-2, Mdo. 6:7-15, 7:51-60, Rum. 8:35-37, 1 Kor. 4:9-13, 2 Kor. 4:8-12, 11:23-26, Gal. 4:28-29, Ebr. 11:32-38, Yak. 5:6, 1 Yoh. 3:1, 13, Ufu. 2:10, 6:9-11, 7:13-17, 11:3-12 return

30. 2 Kor. 4:8-11, Yak. 1:2-3 return

31. Mat. 3:12, 13:3-9, 18-30, 47-50, 21:44, 1 Pet. 1:6-7, Ufu. 3:18-19 return

32. Mat. 5:11-12, Lk. 6:20-23, 2 Kor. 5:1, 1 Thes. 4:14-18, Ebr. 4:9, 11:16, Ufu. 22:12-14 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return