MALAIKA WA MBINGUNI WANAZUNGUKAZUNGUKA JUU YA SAYARI YETU

na Tony Alamo

“Magari ya MUNGU ni ishirini elfu, maelfu maelfu: BWANA yumo kati yao” (Zaburi 68:17). Ni dhahiri zaidi kwamba magari ya Mungu ni vitu vipaavyo angani siku hizi, ambavyo hujulikana kama UFO. Havitoki sayari nyingine yoyote ile bali ni malaika wa MUNGU, ambao kwa karne nyingi wamekuwa askari walinzi wa dunia kwa uhalifu dhidi ya sheria ya MUNGU na dhidi ya warithi wa wokovu.1

Waebrania 1:10-14 inasema, “Na tena, WEWE BWANA, hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi; na mbingu ni kazi ya mikono YAKO: Hizo zitaharibika, nazo zote zitachakaa kama nguo, na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; Lakini WEWE u yeye yule, na miaka YAKO haitakoma. Je! Yuko malaika ALIYEMWAMBIA wakati wo wote, Uketi mkono WANGU wa kuume [kama ALIVYOMWAMBIA KRISTO pekee], hata nitakapoweka adui ZAKO chini ya nyayo ZAKO? Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?”

Kama si kwa magari ya MUNGU (ambayo watu wengi huyaita UFO), ingewezekana vipi  roho watumikao wa MUNGU kufuatilia matendo yote mema ya watu wa Mungu na uharibifu unaofanywa duniani na waovu kwa muda wa saa ishirini na nne kila siku? Je! Ni kwa jinsi gani MUNGU angejua, ingawa ni MUNGU anayejua kila jambo, kwamba ni malaika gani atumwe na wakati gani atumwe kuwabariki watakatifu au kuonya, kulaani au kuwaharibu kabisa waovu?

Kwa mfano, katika kitabu cha Mwanzo 32:12 MUNGU anamwambia Yakobo, ambaye baadaye ALIMWITA Israeli, “Hakika nitakutendea mema, nami nitaufanya uzao wako uwe kama mchanga wa bahari, usiohesabika kwa kuwa mwingi.” Hata hivyo, MUNGU alijua yaliyomo ndani ya akili ya Mfalme Daudi wakati mfalme alipoamua kuwahesabu wana wa Israeli wote. Kwa jinsi hii alianza.1 Mambo ya Nyakati 21:1-2 inasema, “Tena Shetani akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli [ambao MUNGU alisema wasihesabiwe kwa sababu hawahesabiki (Ebr. 11:12)]. Basi Daudi akamwambia Yoabu, na wakuu [watawala] wa watu, nendeni, kawahesabu Israeli toka Beersheba mpaka Dani; mkanipashe habari nipate kujua jumla yao.” Kwa kumtii Shetani, Mfalme Daudi alifuata kile moyo wake ulivyomtuma, kama Hawa alivyokuwa akiongozwa na moyo wake, kwa mioyo yao walisema, “Nitakuwa kama ALIYE JUU ZAIDI, na nitaijua hesabu yao kama MUNGU anavyojua hesabu yao.” Kama Mungu alikuwa na hasira juu ya Hawa na Adamu kwa kutomsikiliza au kumtii  YEYE, akalaani kwamba kila nafsi itakayoishi katika dunia itakumbwa na mauti, kuzimu, na katika ziwa lile liwakalo moto wa milele, ni kwa namna gani MUNGU aliruhusu Daudi kuvunja sheria ZAKE kwa kuasi na kufanya dhambi na kutii amri ya Shetani?2 MUNGU hana UPENDELEO.3 Kama aliwalaani Adamu na Hawa kwa sababu walimwasi, na vivyo hivyo alimlaani Mfalme Daudi, mboni ya jicho LAKE, kwa sababu naye pia alifanya uasi, ATAKULAANI wewe na mimi na kila awaye yeyote yule atakayeasi sheria YAKE.4

Baada ya Daudi kumwamuru Yoabu kuwahesabu Israeli, Yoabu alimjibu Daudi akisema, “BWANA na awaongeze watu WAKE mara mia hesabu yao ilivyo; lakini, bwana wangu mfalme, si wote watumishi wa bwana wangu? Mbona basi bwana wangu analitaka neno hili? Mbona awe sababu ya hatia kwa Israeli? Lakini neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu. Kwa hiyo Yoabu akaenda zake, kati ya Israeli wote, na akafika Yerusalemu. Naye Yoabu akamtolea Daudi jumla ya hesabu ya watu wote. Na hao wote wa Israeli walikuwa watu elfu mara elfu, na mia elfu [1,100,000], wenye kufuta panga; na wa Yuda walikuwa mia nne na sabini elfu [470,000], wenye kufuta panga. Lakini Lawi na Benyamini hakuwahesabu miongoni mwao; kwa sababu neno la mfalme lilimchukiza Yoabu [kama ilivyokuwa kwa MUNGU].

“Neno hilo likawa baya machoni pa MUNGU; kwa hiyo akawapiga Israeli. Naye Daudi akamwambia MUNGU, Nimekosa sana, kwa kuwa nimelifanya jambo hili; lakini sasa uuondolee mbali nakusihi, uovu wa mtumwa wako; kwani nimefanya upumbavu kabisa. Naye BWANA akanena na Gadi, mwonaji wa Daudi [nabii], akisema, Enenda ukanene na Daudi, ukisema, BWANA asema hivi, Nakuwekea mambo matatu [laana tatu – chagua moja] ujichagulie moja nikutendee hilo. Basi Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, BWANA asema hivi, kubali upendavyo; miaka mitatu ya njaa; au miezi mitatu ya kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga na watesi wako; au siku tatu upanga wa BWANA, yaani tauni katika nchi, na malaika wa BWANA akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya basi ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma. Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na niangukie katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema ZAKE ni nyingi sana; wala nisiangukie katika mkono wa wanadamu.

“Basi BWANA akawaletea Israeli tauni; nao wakaanguka Waisraeli watu sabini elfu. Naye MUNGU akatuma MALAIKA [chombo kimoja kipaacho (UFO) kinachothibitiwa na MALAIKA mmoja tu] aende Yerusalemu ili auangamize; naye [MALAIKA] alipokuwa tayari kuangamiza, Bwana akatazama, AKAGHAIRI katika mabaya, akamwambia MALAIKA aharibuye [Mlinzi], basi yatosha; sasa ulegeze mkono wako. Na MALAIKA [Mlinzi] wa BWANA akasimama karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna, Myebusi. Daudi akainua macho yake, akamwona huyo MALAIKA wa BWANA [Mlinzi] amesimama kati ya nchi na mbingu naye alikuwa na upanga wazi mkononi, umenyoshwa juu ya Yerusalemu.

“Ndipo Daudi na wazee wakaanguka kifudifudi, nao wamevaa nguo za magunia [inamaanisha walikuwa wamefunga]. Naye Daudi akamwambia Mungu, Je! Si mimi niliyeamuru watu wahesabiwe? Naam, mimi ndimi niliyekosa, na kufanya yaliyo maovu sana; lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Mkono wako, nakusihi, Ee BWANA MUNGU wangu, na uwe juu yangu, na juu ya nyumba ya babangu; wala si juu ya watu wako, hata wao wapigwe. Ndipo MALAIKA wa BWANA akamwamuru Gadi [nabii] kwamba amwambie Daudi, ya kuwa Daudi akwee, akamwinulie BWANA madhabahu katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi. Basi Daudi akakwea sawasawa na neno la Gadi, alilolinena kwa jina la BWANA.

“Arauna alipogeuka na kumwona yule MALAIKA; ndipo yeye na wanawe wanne waliokuwa pamoja naye wakajificha [kama watu wa leo wafanyavyo wanapoona vitu virukavyo na vyombo kama visahani, UFO, MALAIKA  wa MUNGU, vikizungukazunguka juu yao; hawa hawatoki kwenye sayari nyingine kama inavyodhaniwa, bali wanatoka Mbinguni!] Naye Arauna alikuwa akipura ngano. Basi Daudi alipokuwa akimjia Arauna, Arauna akatazama, akamwona Daudi, akatoka katika kile kiwanja, akamsujudia Daudi kifudifudi hata nchi [Arauna alipomwona MALAIKA, kisha Daudi, alihisi uhusiano mkubwa kati ya Daudi na MALAIKA. Arauna alipatwa na hofu akamwangukia Daudi hata chini]. Ndipo Daudi akamwambia Arauna, Unipe mahali pa kiwanja cha kupuria, ili kwamba nimjengee BWANA madhabahu hapa; kwa thamani yake kamili utanipa; ili tauni izuiliwe katika watu. Arauna akamwambia Daudi, Ujitwalie, na bwana wangu mfalme na afanye yaliyo mema machoni pake; tazama, ng’ombe kwa sadaka za kuteketezwa, na vyombo vya kupuria kwa kuni, na ngano kwa sadaka ya unga, nazitoa; zote nazitoa. Mfalme Daudi akamwambia Arauna, La, sivyo; lakini kweli nitazinunua kwa thamani yake kamili; Kwani sitamtwalia BWANA kilicho chako, wala kutoa sadaka ya kuteketezwa isiyo na gharama. Kisha Daudi akamjengea BWANA madhabahu huko, akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akamlingana BWANA; NAYE [MUNGU] akamwitikia kutoka mbinguni kwa moto juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. BWANA naye akamwamuru MALAIKA; naye akaurudisha upanga wake alani mwake tena.

“Wakati huo, Daudi alipoona ya kwamba BWANA amemwitikia katika kiwanja cha Arauna, Myebusi, ndipo hutoa dhabihu huko. Kwa maana ile Maskani ya BWANA, aliyoifanya Musa jangwani, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, vilikuwapo wakati huo pahali pa juu pa Gibeoni. Wala Daudi hakuweza kwenda mbele yake ili kumwuliza MUNGU; kwa sababu aliona hofu kwa ajili ya upanga wa yule MALAIKA wa BWANA” (1 Mambo ya Nyakati 21:3-30). Yapo maandiko mengine mengi yanayoonyesha kwamba MUNGU hutumia malaika WAKE kulaani na kuangamiza.5
Nabii wa kale, Nahumu alielezea barabara kuhusu magari haya kwa namna alivyoyaelewa yeye binafsi. Nahumu 2:4 inasema, “Magari ya vita yanafanya mshindo njiani, yanasongana-songana katika njia kuu; Kuonekana kwake ni kama mienge, Yanakwenda upesi kama umeme.” Huu ni unabii wa siku za mwisho wa magari na barabara kuu.

Hakuna maisha katika sayari nyingine yoyote, katika uumbaji wowote wa MUNGU. Hivyo basi, ni ujinga uliokithiri kabisa kufikiri kwamba vitu hivi kama visahani na UFO vinatoka sayari nyingine yoyote. Vitu hivi vinatoka Mbinguni.

Zaidi kuliko kitu kingine chochote, MUNGU anataka kuaminiwa, na anatambua kuwa humwamini mara unapovunja amri ZAKE. Hili ndilo anenalo MUNGU kuhusu mbingu ZAKE na nchi YAKE. Katika Mwanzo 1:14-15, “MUNGU akasema, na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka [kwa ajili ya dunia na si kwa ajili ya sayari nyingine yoyote ile]; tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi [na si juu ya Mirihi, Mshtarii, Utaridi, au sayari nyingine yoyote]; ikawa hivyo.” Usidhani kwamba utaweza kuepuka uharibifu na vurugu ambayo inatokea sasa na itaendelea kujikuza katika kile unachokiita “dunia mama.” Usije ukadhani kwamba utakwenda kuishi kwenye sayari nyingine, maisha hayawezi kuwepo kwenye sayari nyingine tofauti na hii. Hutapata amani katika dunia kwa sababu sisi tu watu wa kutenda dhambi na BWANA AKIWA hayumo ndani ya mioyo yetu, tutakuwa watu wa dhambi daima. Pia, tafadhali ondoa kabisa kwenye akili yako kuwa vitu hivi vipaavyo angani UFO, ambavyo ni WALINZI, MALAIKA vinatoka kwenye sayari nyingine. Kama unaamini mambo hayo ambayo hayapo, MUNGU amekutumia nguvu ya upotevu kama anavyoeleza katika 2 Wathesalonike 2:8-12: “Hapo ndipo atakapofunuliwa yule muasi [Ibilisi, Shetani, mpinga Kristo], ambaye BWANA YESU atamwua kwa pumzi ya kinywa CHAKE, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo KWAKE; yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote na ishara na ajabu za uongo [waovu wote na wanaotegemea Nguvu za Kishetani]; na ishara za ajabu za uongo [uongo kama ule wa kusema kwamba MALAIKA au UFO wanatoka kwenye sayari nyingine, na kwamba kuna uhai katika sayari nyingine, na kwamba hivi karibuni utaweza kutoroka uharibifu mbaya wa dunia hii kwenda katika sayari nyingine], na katika uongo wote wa udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuupenda ule ukweli, wapate kuokolewa [kufunga ndoa za jinsia moja ni sawa, kutoa mimba, mauaji ya silaha, yote ni sawa,6 usagaji na ushoga ni sawa,7 uzinzi8 na uasherati ni sawa,9 matumizi ya pombe na madawa ya kulevya ni sawa,10 vichekesho ni sawa,11 wizi12 na makufuru ni sawa,13  kutokumpenda BWANA MUNGU wako, kwa moyo wako wote, akili zako zote, na kwa nguvu zako zote, ni sawa,14 kutomtumikia BWANA ni sawa, na kutamani, ni sawa15] kwa udhalimu ndani yao wanaopotea; kwa sababu hawakupokea upendo wa ukweli, ili waokolewe. Kwa hiyo MUNGU awaletea nguvu ya upotevu wauamini uongo [uongo kama ule wa kusema kwamba UFO ni viumbe kutoka sayari nyingine, kana kwamba kuna maisha kwenye sayari nyingine]: Ili wahukumiwe wote ambao hawakuuamini ukweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu”

Hebu turejee katika Mwanzo 1: “MUNGU akafanya mianga miwili mikubwa; ule mkubwa utawale mchana [jua], na ule mdogo utawale usiku [mwezi]: AKAFANYA na nyota pia. Na MUNGU akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya NCHI [si sayari nyingine yeyote ile], na kutawala mchana na usiku, na kutenga nuru na giza; MUNGU akaona ya kuwa ni vyema” (Mwanzo 1:16-18).

Sasa ni nini unachokiamini? Je, unaamini lililo jema au lililo ovu? Je, unaamini kwamba MUNGU alitufinyanga kutoka katika mavumbi ya ardhi, au unawaamini wanasayansi? Je, unamwamini MUNGU au mashine za kaboni za kutambua tarehe za mambo ya kale? Kwa maneno mengine, je, unaamini kwamba dunia ina umri wa miaka 6,000 kama BWANA asemavyo, au unaamini uongo kwamba ilikuwepo mamilioni au mabilioni ya miaka kama wanaomkana MUNGU wasemavyo? Iwapo unaamini uongo badala ya NENO la MUNGU, umepokea nguvu ya kupotea, na umehukumiwa.16 Natumai, kwako haiko hivi. Kama unapenda kuokolewa na kuishi milele na MUNGU mbinguni, BABA, MWANA, na ROHO MTAKATIFU, pamoja na wale wote waliomwamini MUNGU kupitia mwanawe YESU KRISTO, sali sala hii:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Haki ya kunakili Machi 2013  Haki zote zimehifadhiwa World Pastor Tony Alamo   ® Tarehe ya Usajili  Machi 2013
SWAHILI—Vol. 17700—Heavenly Angels Hovering Over Our Planet


footnotes:

1. Mwa. 18:20-22, 19:1-25, Hes. 22:21-35, 2 Sam. 24:10-16, 2 Fal. 6:8-17, 2 Nya. 20:1-29, 32:1-22, Zab. 34:7, 35:4-5, 68:17, Dan. 6:21-22, Zek. 1:7-21, 2:1-5, sura. 4, Mat. 28:1-7, Mdo. 5:17-24, 12:1-12, 21-23, Ufu. 7:1-2, sura. 8, 9:1-5, 13-21, 14:6-11, 15-20, 15:1, 5-8, sura. 16, 18:1-6, 21, 19:17-18, 20:1-3 return

2. Mwa. 2:16-17, 3:1-19, Rum. 5:12-18, 1 Kor. 15:22, 47 return

3. Law. 19:15, Kum. 1:17, 16:19, 1 Sam. 26:23, 1 Fal. 8:32, 2 Nya. 6:23, 19:7, Zab. 9:8, Mit. 24:23, 28:21, Isa. 45:21, Mdo. 10:34, Rum. 2:11, Efe. 6:9, Col. 3:25, Yak. 2:1-10, 1 Pet. 1:17, Ufu. 15:3 return

4. Mwa. 3:1-19, Kut. 23:20-21, Kumb. 11:26-28, 28:61-63, 1 Sam. 12:14-15, 15:22-23, 2 Sam. sura. 11, 12:1-23, Ayu. 36:7-12, Yer. 12:16-17, 18:9-10, Rum. 2:5-13, 6:12-16, Efe. 5:3-6, 2 The. 1:7-9, Ebr. 2:1-4 return

5. Mwa. 19:1-25, Hes. 22:1-35, 25:1-9, 2 Sam. 24:1-17, 2 Fal. 19:35, 1 Nya. 21:9-30, 2 Nya. 32:19-22, Ufu. 7:1-2, sura. 8, 9:1-5, 13-21, 14:8-11, 15-20, sura. 16, 18:1-2, 21, 19:17-21, 20:1-3, 21:9 return

6. Mwa. 9:5-6, Kut. 20:13, 21:12-15, 22-23, Law. 24:17, Hes. 35:16-21, 30-33, Kum. 5:17, 27:24-25, Zab. 139:13-16, Mit. 1:10-16, 6:16-18, Yer. 1:5, Mat. 19:18, Mk. 10:19, Lk. 18:20, Rum. 13:9, Gal. 5:19-21, 1 Tim. 1:9-10, Yak. 2:11, 1 Yoh. 3:15, Ufu. 9:20-21, 21:8, 22:14-15 return

7. Mwa. 19:1-13, 24-25, Law. 18:22, 20:13, Kum. 22:5, 23:17, Amu. 19:22-25, Rum. 1:20-32, 1 Kor. 6:9-10, 1 Tim. 1:9-10, 2 Tim. 3:1-5, Yud. 7 return

8. Kut. 20:14, Law. 18:20, 20:10, Kum. 5:18, 22-24, 1 Fal. 14:24, 15:11-12, Mit. 6:29, 32-33, Yer. 5:8-9, Eze. 18:10-13, 22:11, Mal. 3:5 Mat. 5:27-28, 15:19-20, 19:18, Mk. 7:21-23, Lk. 18:20, Rum. 13:9, 1 Kor. 6:9-10, Yak. 2:10-12 return

9. 1 Kor. 5:9-11, 6:9-10, 13-18, 7:2, 10:7-8, 2 Kor. 12:21, Efe. 5:3, Kor. 3:5-6, 1 The. 4:3-5, Yud 7, Ufu. 2:14, 20-22, 9:20-21 return

10. Kum. 21:20-21, Mit. 23:21, 29-35, 31:4-5, Isa. 5:11, 22-23, 28:1-4, Nah. 1:9-10, Lk. 21:33-36, Rum. 13:12-14, 1 Kor. 5:10-12, 6:9-10, Gal. 5:19-23, 1 The. 5:6-8, 1 Tim. 3:8-9, Tit. 1:7-9, 2:1-5, 1 Pet. 4:1-5, 2 Pet. 1:5-8 return

11. Mhu. 2:1-3, 7:2-6, Mat. 12:36, Efe. 5:3-4, 1 Tim. 2:9-10, 15, Tit. 2:1-8, 12, 1 Pet. 1:13-16, 4:7, 5:8 return

12. Kut. 20:15, 22:1-4, Law. 19:11, 13, Kum. 5:19, Zek. 5:3, Mat. 15:19-20, 19:18, Mk. 7:21-23, Lk. 18:20, 19:45-46, Rum. 13:9, 1 Kor. 6:10, Efe. 4:28, Ufu. 9:21 return

13. Ufu. 24:11-16, 23, Mat. 12:22-32, 15:19-20, Lk. 12:9-10, Ufu. 13:1-9, 14:8-11, 17:1-9 return

14. Kum. 4:29, 6:5, 10:12, 11:13, 13:3-4, 26:16, 30:6, Yos. 22:5, Mat. 22:37-40 return

15. Kut. 18:21, 20:17, Kum. 5:21, Zab. 10:3, Mik. 2:1-3, Mk. 7:21-23, Rum. 1:28-32, 13:8-9, 1 Kor. 5:9-11, 6:9-10, Efe. 5:1-5, Kol. 3:5-6, 2 Tim. 3:1-5, 2 Pet. 2:1-3, 12-14, 1 Yoh 2:15-17 return

16. Isa. 66:3-4, 2 The. 2:3-12 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return