Muhtasari wa Kipindi cha Redio Jarida la Upelelezi na Greg Anthony Marekebisho ya kwanza ya Redio

Agosti 7, 2014

Greg anaanza kwa kusema Tony Alamo yuko gerezani tangu 2008 kutumikia kifungo cha miaka 175 kwa sababu ya mashitaka ya kuwekelewa ya unyanyasaji wa kijinsia, na namna ambavyo Tony, kwa miaka 40 hadi 50 iliyopita, amekuwa akituambia ukweli kuhusu ushawishi wa Vatican juu ya uhuru wetu wa dini na kwa kutumia njia za kishetani kuingilia mfumo wetu wa kisiasa. Anaelezea jinsi Tony anavyowafikia maelfu kwa maelfu ya watu duniani kote kwa habari hizi za kuipinga – Vatican ambazo watu hawana budi kuambiwa kwa sababu zipo sababu zenye uwezo wa kutoa ushahidi kwamba kile asemacho Tony ni kweli na anateswa kwa ajili yake.

Greg anataja uvamizi wa 2008 katika Arkansas, anasema ulikuwa uvamizi kama ule uliotendeka kule Waco mwaka wa 1992 kwenye huduma hii ambayo yeye amezisikia habari zake kutoka kwenye vyombo vya habari tawala ambavyo vilionekana kuwa na habari za kutosha kuhusu habari hizo. Anadhani nia yao ilikuwa kuizima huduma hii yenye mafanikio makubwa sana ambayo ilikuwa na idadi kubwa ya makanisa katika majimbo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kumpata Tony. Kwa namna walivyofanya ilikuwa ni kuwashambulia watoto wa huduma hii. Anahusianisha kile blogger alichosema kuhusu uvamizi: wakati jimbo na shirikisho la maafisa wa kutekeleza sheria walipoivamia Tony Alamo Ministries, wengi, kama si zaidi, ya waandishi wa vyombo vikubwa vya habari walikuwa katika Texarkana, Arkansas, wakitazama kila jambo wazi wazi, lakini bila kuandika chochote hadi tukio lilipoanza. Hivyo walijua vilivyo kuhusu jambo hili. Uvamizi ulikuwa umepangwa kufanyika Oktoba, lakini ulitokea Septemba. Siku ya Ijumaa, siku moja kabla ya uvamizi huo, mtu mmoja katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Marekani bila kutangaza alituma barua pepe kuhusu uvamizi kwa zaidi ya vyombo 50 vya habari katika jimbo hilo. Barua pepe hiyo ilitumwa wiki kadhaa kabla ya uvamizi uliokuwa umepangwa kutokea. Greg anaamini ulipangwa kumhukumu Tony kabla ya kusikilizwa kwa kesi yake.

Blogger aitwaye Frank Lockwood alisema hivi: “Siri yao ikiwa imejulikana, maafisa wa kutekeleza sheria walisogeza mbele ratiba yao. Ilibidi magazeti kuamua aidha kutoa habari katika toleo la Jumamosi ama kusubiri siku moja au mbili zaidi. Pamoja na Watoto walioripotiwa kuwa kanisani, na kwa madai ya unyanyasaji wa watoto, mashirika ya habari kwa hiari yalishindwa kuandika kuhusu uvamizi hadi ulipokuwa umwekwisha kutokea.” Wamevisisimua vyombo vyote vya habari kuhusu tukio hili: hakuna mtu anayejua ni nini hasa kinaendelea. Ni jambo la kumfanya Tony aonekane mwenye hatia kwa jinsi uvamizi huu unavyofanyika haraka na katika mtindo wa-SWAT [kikundi cha watu kinachotumiwa na serikali kudungua adui mmojammoja kutoka mafichoni kwa kutumia risasi]. Alielezea jinsi timu ya SWAT ilivyokuja ikiwa na bunduki na raifo, wakiwatisha, wakati watoto walipokuwa nje wanacheza, kujaribu kumkamata Tony, hata hivyo Tony hakuwepo pale, alikuwa amekwenda Los Angeles wakati huo. Hapakuwa na dalili kwamba kulikuwa na silaha au kitu chochote kanisani mle. Lilikuwa ni shirika la amani, na kama walitaka kumkamata Tony, wangeweza kufanya hivyo kwa namna ya utulivu, lakini jambo hili lilikuwa lifanyike ili kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari, na hii ilikuwa ni njia ya kumhukumu kabla ya kusikilizwa kwa kesi dhidi yake.

Watoto sita walichukuliwa na serikali siku hiyo. Siku iliyofuata, habari zilikuwa kwenye vyombo vyote vya habari tawala. Nchi nzima ikafahamu, Bw. Alamo alikuwa hatiani tayari. Habari zilirushwa kupitia kipindi cha TV cha Oprah Winfrey na kwenye baadhi ya chaneli nyingine za makosa ya jinai.

Greg anasema kwamba katika mtazamo wa wakili, wao (maadui wa Tony) hawana mengi katika jambo hili, na kile walichonacho tayari kimeharibiwa/vurugwa. Kesi hii ni mfano dhahiri kukuonyesha kile wanachoweza kukufanya endapo utaamua kuanzisha vita dhidi ya kanisa katoliki na Vatican. Greg anaeleza jinsi Marekani ilivyo na unafiki, ilivyoweka viwango viwili, kuyaacha makanisa ya kikatoliki kuendelea wakati kuna ushahidi mwingi wa yaliyotokea kwa watoto shuleni huko Canada, Ireland, mateso na dhuluma duniani kote, na bado kanisa hilo linaruhusiwa kuendelea?! Wanazo pesa na nguvu na uwezo wa kuidhibiti serikali yetu ili waweze kuendelea kuwanyanyasa watoto bila kuulizwa na yeyote. Kama una sauti kubwa kama ya Alamo, wanaweza kukujia kwa madai kama hayo kuwa una hatia, na kwa kutumia vyombo vya habari na, FBI, utekelezaji wa sheria, na rushwa, na kwa kulazimisha watu kuleta mashtaka ya uongo ambao walirudi kubatilisha maneno waliyosema dhidi ya yule wanayemtangaza kuwa ni mkosaji. Anaitaja kesi ya kiraia ya mwezi Machi na hukumu ya dola nusu bilioni.

Greg anamwelezea Tony kama mtu mwenye umri wa miaka 79 na kipofu gerezani. Kisha anaeleza ni nini Tony amesema kutoka gerezani: Kwa karibu miaka 50, wamekuwa wakijaribu kuniweka mbali. Kwanza, wametutuhumu sisi kuwa tu wakomunisti, wametushambulia na kutuweka gerezani sisi na wanachama wetu kikatili ili kutuzima na kunizuia mimi na mke wangu Susan kuhubiri habari za kweli kuhusu Neno la Mungu. Kisha walitaka tuwe “Waco”, na wanaendelea kututuhumu kuwa ni dhehebu hatari na magaidi wa kutumia silaha. Na nilishitakiwa kwa kesi ya kunyanyasa watoto, madai ambayo Mwanasheria wa Wilaya wa Los Angeles aliyatupilia mbali. Baadaye nilishtakiwa kwa kutishia kumteka hakimu wa Shirikisho. Bodi ya mahakimu haikunipata na hatia ya jambo hili pia. Kisha IRS ilitumika kujenga kesi ya uongo ya kutotoa kodi ya mapato, jambo ambalo kamwe halikuwa kweli. Wakili wangu, Jeff Dickstein, mwidhinisha kodi, alibanwa katika namna ambayo ilikuwa sharti aniuze mimi ama aingie gerezani yeye mwenyewe. Nilihukumiwa kifungo cha miaka 6, na kwa sababu ya tabia njema, mwaka 1998 nilikuwa nje baada ya kukaa gerezani miaka minne. FBI waliendelea kunichunguza bila kunipa hata nafasi. Hatimaye, mwaka 2008, walipata mashahidi wachache wa uongo ambao waliasi kanisa miaka ya nyuma na kukubali kushirikiana nao. Toleo la fidia na fedha katika kesi ya kiraia ilikuwa ikivutia. Kesi ya kiraia ilitumia mashahidi watano na wa sita aliongezeka, pia mwanachama mmoja wa zamani alitumika katika kesi hiyo ya jinai, kuimarisha kesi. Lakini wakati huu katika kesi ya madai, alitaka kupata fedha, hivyo aliunda mashtaka mapya kwamba alishurutishwa kuolewa lakini akatoroka. Wa saba alikuwa ndani ya kanisa hadi Juni, 2010, alijua kuwa sina hatia alikuwa na mimi muda wote wa kesi. Kisha aliondoka mwezi Juni. Mwezi agosti alijiunga na kesi ya madai kwa sababu ya fedha. Kesi ya madai ilikuwa katika mahakama ya shirikisho, lakini wakati kesi hiyo ilikaribia kushughulikiwa, hakimu alisoma muhtasari uliojazwa, na mashtaka yote ya shirikisho yalifutiliwa mbali. Hivyo kesi ilifungwa na kisha kufunguliwa tena katika mahakama ya jimbo la Arkansas. Hakimu aliruhusu mashtaka yote yaliyotolewa kufanyika na kurejeshwa kwenye mahakama ya jimbo. Hatukuwa na fedha za kutosha kuendelea na kesi, hivyo tulipoteza kwa sababu ya kukosa kutokea kortini.

Greg alisema walimshambulia Tony na kanisa jambo linalotia uchungu zaidi: walishambulia pia watoto. Walitafuta katika kila sehemu ilipokuwa huduma yake kupata watoto wengine ambao hawakuchukuliwa katika uvamizi wa kwanza. Anafafanua uvamizi wa kwanza na maafisa wa polisi mia, timu ya SWAT, na jinsi walivyowachukua wasichana sita kutoka kwenye bembea. Hakuna hata msichana mmoja aliyethibitika kufanywa jambo lolote baya lisilofaa na Tony. Waliwachukua kwa nguvu kwenye gari wakati wasichana hao wakiwa wanaimba nyimbo za injili. Alielezea mahojiano ya kuchunguza maovu yaliofanyiwa wasichana hawa siku ya pili, jinsi walivyokuja bila kitu, na jinsi mmoja wao alikuwa dada wa mtu mzima mmoja aliyeishi huko, lakini walikataa kumrejesha kwa wazazi wake. DHS kiliendelea kuwashikilia wasichana hao sita, ingawa hawakupata chochote kibaya, na hakimu akatoa amri ya kuchukua kila mtoto kutoka makanisa katika maeneo yote nchini Marekani. Washirika wakakimbia na watoto wao kuwaficha ili kuepuka matatizo- njia kuu ya kuharibu kila kitu. Anaelezea jinsi gari mbili zilizobeba watoto zilivyosimamishwa kwenye barabara kuu. Wakawakamata watoto wachanga na watoto wakubwa na hawakuwarudisha tena. Greg alisema kuwa ule ulikuwa utekaji nyara. Anazidi kueleza kwamba hakuna madhara yoyote yaliyogunduliwa kutendeka kwa watoto, na hakuna hatia yoyote iliyopatikana dhidi ya Tony ambayo ingeweza kutumika kumshtaki kama walivyokuwa wakitarajia. Walijua kuwa ni njia ya kubomoa huduma yote. Greg anaendelea kuuliza kama hii ni nchi ya Gestapo. Greg anasema hii ilifanyika kufunga huduma hii, na kumzuia Tony kuzungumza mabaya dhidi ya Vatican, na kuchukua mali zote za Tony pamoja na fedha. Greg anauliza, “Kwa nini wasichukue fedha kutoka Vatican kwa yote hayo waliyofanya?” Kulikuwa na kesi mahakamani kuhusiana na swala hili, na walisema, “Vatican haifanyi biashara na Marekani.” Walijaribu kubomoa huduma kwa kutawanya watu ambao wamejipanga, kuchapisha, na kusambaza majarida, na ambao waliifanya huduma kusambaa mijini katika Marekani yote kila juma, kusambaza maandiko na kuyatuma nje kwa njia ya barua. Greg alieleza kuwa maandiko ndicho kitu anachozungumzia kwenye kipindi chake, ushawishi wa Vatican juu ya uhuru wetu wa dini na juu ya serikali yetu, na kushawishi kila mtu kuamini kwamba wao ndilo kanisa pekee la kweli. Kama kuliwahi kuwa na kanisa la kishetani, ni Vatican! Greg alisema, wazazi walikuwa na chaguo la kutisha la, aidha kuiacha huduma au kupoteza watoto wao na kupoteza haki yao ya kuwa wazazi. Hakuna maneno yanayoweza kuelezea uharibifu wa wote wawili watoto na wazazi. Kisha watoto wakatiwa kasumba na kufanywa maadui dhidi ya wazazi wao, na kuwachukia na pia kanisa lao walilolipenda.

Hili ni swali la Tony akiuliza kutoka kwenye chumba chake cha gerezani: “Wakati kuna ushahidi mkubwa na uliowazi wa unyanyasaji wa watoto katika dhehebu la kanisa Katoliki, kwanini watoto wasizuiliwe kwenda kwenye shule zao, makanisa yao, vituo vyao vya watoto yatima, jumuiya zao, n.k? Kwa nini wazazi ambao ni waumini wa kanisa Katoliki ambao huwarudisha watoto wao kwa dhehebu hili linalonyanyasa kila siku hawanyimwi haki yao ya kuwa wazazi na kunyang’anywa watoto wao?”

Greg alieleza jinsi mama yake alivyokufa kwa saratani ya damu wakati kaka yake aliyezaliwa kabla ya muda wake wa kuzaliwa akiwa na umri wa miezi 6 na baba yake alikuwa na bili nyingi za kulipa. Kulikuwa na kituo cha watoto yatima cha Kikatoliki ambacho hakikuwa mbali na eneo waliloishi, watoto hawa wote walipelekwa hapo.

Monsinyori alikuja nyumbani kwake, lakini badala ya kumsaidia baba yake Greg, alitaka kuwachukua watoto kutoka kwa baba yake na kuwaweka kwenye kituo hicho cha kulelea watoto yatima. Baba yake alimkamata Monsinyori na kumbamiza ukutani, na kumsukumia nje, na kumpiga mateke hadi kwenye ngazi. Greg alisema, “Hiyo ndivyo ninavyoielewa Vatican. Wapige mateke mgongoni na uwafukuze kabisa nyumbani mwako. Hiyo ndivyo baba yangu alivyofanya, na tulikua vizuri, wenye afya njema na furaha, na ndugu yangu ni mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa sana sasa. ”Baba yake aliapa kutoingiza mguu wake katika kanisa Katoliki kamwe, jambo ambalo kweli hakufanya kamwe. Na kamwe hakuthubutu kumpeleka ndugu yake kwenye shule za kanisa Katoliki. Baba yake alimtaka Greg kumruhusu kumwondoa kwenye shule ya kanisa Katoliki, lakini Greg alimwomba amwache pale tu kwa sababu alikuwa na marafiki wengi na ndio punde tu amemkosa mama yake.

Katika nusu ya pili, Greg anataja magereza aliyowahi kuzuiliwa Tony na jinsi walivyopitia kwa ndani mawasiliano yote na jinsi kumtembelea kulivyoendeshwa; hakuna kitu cha faragha. Serikali iliulipa Mtandao wa Upelelezi wa Dhehebu (Cult Awareness Network) zaidi ya dola za kimarekani 5,000.00 kwa kila moja kati ya mashahidi watatu waliokuwa dhidi ya Tony kwa programu madhubuti ya majuma mawili sehemu iitwayo Wellspring Retreat ili kuwatia kasumba na kuwafunza jinsi ya kutoa ushahidi dhidi ya Tony. Serikali ililipia safari zao zote, pia ililipa dola za kimarekani 1,500.00 kwa mtoto wa mmoja wa mashahidi asimamiwe wakati mama yake akifanyiwa ushauri. Waliwalipa mashahidi kwa kujifanya walikuwa wanawalipia bili kwani hawangeweza kufanya kazi na kujilipia wakiwa mahali hapo, kama vile bima ya gari, n.k. Mkuu wa zamani katika Wellspring, Paul Martin, binafsi aliwafanyia kazi mashahidi hawa. Hii ilifanyika Desemba, 2008, na mara baadaye Bw. Martin kushindwa kwa sababu ya kuugua, alikutwa na ugonjwa wa saratani ya damu na alikufa miezi michache baadaye.

Katika siku za nyuma, ushahidi wa wale walioandaliwa kule Wellspring ulikuwa ukitupiliwa mbali na mahakama. Lakini kwa mtu kutoka upande wa utetezi hata anapothubutu kuongea na mmoja wa mashahidi, anaweza kushtakiwa kuwa anaingilia shahidi. Hata hivyo serikali inaweza kuwasafirisha mashahidi wa washitakiwa hadi mahali hapa ili kuwajaza kasumba. Watu wanaweza kwenda huko wakiwa hawako upande wowote na kutoka wakiwa wamejaa uhasama. Ni hatua muhimu katika kesi hii.

Alisema, Dorothy Curry alisema kuwa kipindi cha Televisheni cha Unsolved Mysteries kilidanganya, na wala Tony Alamo hakumnyanyasa bintiye. Hii ilikuwa mwaka 1991 wakati walipojaribu kumfanyia Tony jambo hilo hilo ambalo halikufanikiwa. Greg anasoma baadhi ya mambo aliyosema Dorothy katika maandishi ambapo anakanusha mashitaka ya Jim Griffin kwamba Tony alimnyanyasa Carissa kijinsia.

Greg anasoma kutoka katika makala Jarida la Utume la Kiprotestanti [Protestant Mission Newsletter] la British Columbia jinsi ndugu kutoka katika huduma walivyokwenda Canada na kusambaza nyaraka za Injili wakati Papa Yohane Paulo II akiwa na ratiba ya kutembelea mahali hapo. Siku aliyowasili Papa, ndugu hao walitiwa nguvuni. Hakuna mashitaka yaliyotajwa, hakuna sababu zilizotolewa, lakini waliamriwa kufungiwa jela hadi Papa alipoondoka Canada waliachiliwa bila maelezo yoyote na hapakuwa na ujumbe wowote wa kuwataka radhi. Greg anaendelea kusema kwamba mwandishi wa makala anasema anajua kwamba usambazaji wa maandiko yanayoweka hadharani uovu wa kanisa katoliki ndiyo sababu hasa inayomfanya Tony Alamo kuwa kizuizini tena. Mamlaka yanajaribu kutengeneza washahidi wa uongo. Kama kweli mamlaka yanakerwa na vitendo vya unyanyasaji wa kimwili na kijinsia kwa watoto, kwa nini hawajafunga taasisi zote za kanisa katoliki ambazo zimethibitika kunyanyasa maelfu ya watoto (Greg anaongeza mia elfu nyingi, mamilioni kwa miaka mingi) kuwanajisi, kuwanyanyasa kimwili, kuwatesa na hata kuuawa na watawa? Anauliza, “Ni mara ngapi umewahi kusikia kuwa mtawa ameshitakiwa kwa kupatikana na hatia ya kubaka na kunyanyasa, ukitarajia haki itendeke, unakuja kujua kuwa huyo mtu mpotovu amehamishwa kwa siri kwenda monasteri nyingine au kwenye kanisa jingine kwa siri ili aendeleze unyanyasaji huo sehemu nyingine? Haki i wapi? Inakuwaje wazazi ambao ni waumini wa kanisa Katoliki na wanafahamu kuwa wananajisiwa na watawa bado wanaendelea kuwapeleka watoto wao kwa wanajisi na wapotovu hawa na wanyanyasaji wa kijinsia? Upendo wao wa asili u wapi? Je, hii si kutojali? Wanafahamu na wanaweza kusoma kuhusu pedofilia kwenye magazeti kila siku. Kwanini mamlaka haziingilii kati ukiritimba huu mkubwa wa unyanyasaji unaoendelea kutokea kwa watoto? Kuna viwango viwili vya kanuni, Kimoja kwa ajili ya Roma, na kingine kwa ajili ya dunia nzima kama hadithi hii ya Tony Alamo inavyoeleza.”

Greg anasoma kitu kilichoandikwa na mtu mmoja aitwaye Shane mwaka 2009 ambaye anaiita DHS [Department of Homeland Security] idara inayohusika na usalama wa nchi] idara ya mateso ya mwanadamu [Department of Human Suffering]. Alisema DHS iliiba watoto 35, ikamtupa gerazani Tony Alamo, na kwa kufanya hivyo, inadhihirisha kuishitaki Biblia. Huduma ya Alamo si dhehebu la kishetani wala vuguvugu la watu wanaoamini mapepo, bali ni Jumuiya ya amani ya wakristo wanaoiamini Biblia na wanaoihubiri Biblia duniani kote bila kuchoka. Sababu yakusikitisha ambayo hakimu alitoa kuamuru watoto wachukuliwe kutoka kwa wazazi wao ni kwamba hawakuwa wamepata chanjo na hawakuwa wamesajiliwa na serikali kwamba walikuwa wakisomea nyumbani. Greg anaendelea kueleza kwamba wangeweza kuweka virusi vya Ebola katika chanjo, hivyo kaa mbali nao na usikubali chanjo za mafua. Anasema wamekuwa wakizifungia tovuti zote zilizokuwa zikipinga- chanjo. Shane anasema kwamba ukweli halisi juu ya utekaji nyara hizi ni kwa sababu Huduma ya Alamo inahubiri “[KWA SIRI] BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI” (Ufunuo 17: 5).

Greg anasema sababu pekee ya kumpata Tony ni kwa sababu amefanikiwa sana. Huduma yake ni maarufu sana, na ujumbe wake unawafikia maelfu na mamia ya maelfu ya watu. Kama angekuwa ameketi nyumbani kwake akihutubia watu 20, wasingejisumbua naye, lakini hawataki siri zao zitajwe nje wazi wazi, na hii ndiyo sababu yote haya yanamtokea. Suluhisho pekee ni si kuamini kile unachokisikia kutoka kwenye vyombo vya habari tawala kuhusu habari hizi kwa sababu hawakuwahi kukwambia kuhusu ushawishi; hawakuwahi kukwambia kuhusu mambo mengi yanayoendelea. Wamemtaja tu kuwa mwenye hatia, na wanataja habari zake katika mtazamo wa mashitaka na ukosaji, na yeyote atakayesikia ataondoka akisema, “Lazima yuko na hatia.” Hivyo ndivyo serikali, vyombo vya habari na Vatican vinavyofanya kazi pamoja.

tonyalamoministries.com