USHUHUDA WA TONY ALAMO

Mifupa Mikavu

na Tony Alamo

Nabii wa Agano la Kale aitwaye Ezekieli, alipewa maono na Mungu. Aliona bonde la mifupa mikavu lililowakilisha hali ya kifo cha kiroho cha Israeli na dunia yote. Maono haya yalitabiri ujio wa kwanza wa Kristo, kuhubiri kwake injili, na matokeo yake; na ufufuo wa kwanza kutoka mautini kuelekea uzima wa milele kwa wote waaminio “Neno la Bwana.”1

Mungu akamwambia Ezekieli, “Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi?” (Je, waliokufa kiroho wanaweza kuishi?) Ezekieli akajibu, “Ee Bwana MUNGU [uliyewaumba], wajua wewe.”2 Mungu akamwambia tena nabii, akasema, “Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie,

Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana. Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi.”3

Israeli, kama taifa, walijua kwamba wamekwisha.4 Hadi leo wamegawanyika pasipo matumaini. Lakini Mungu alimwambia Ezekieli kwamba ataliinua taifa lingine kubwa zaidi ya taifa la kwanza la Israeli, ambalo halikukoma kutenda dhambi. Taifa la pili la Israeli lingekuwa la watu kutoka kila taifa ulimwenguni,5 masalio ya Wayahudi wateule, kusanyiko kubwa la watu wa Mataifa waliopandikizwa kwenye Mzabibu wa Kweli (yaani, Kristo).6 Lingekuwa taifa kubwa, takatifu la wale waliofufuliwa kutoka kwenye maisha ya mauti ya dhambi hadi kwenye uzima wa milele.7 Hawatatenganishwa kamwe mbali na Mungu. Huu ndio uliokuwa ufufuo wa kwanza kupitia kwa njia ya nguvu ya ufufuo ya Kristo.8

Katika mwaka wa 1964, kabla ya ufufuo wangu wa kwanza kupitia Kristo, mimi, Bernie Hoffman, pia ninayefahamika kama Tony Alamo, nilifahamika vizuri sana kwa utendaji dhambi na kwa mambo machafu, na sikuwa na ufahamu wowote kumhusu Mungu. Sikuwa na wazo kwamba Mungu yupo. Maneno ya Mungu kwangu yalikuwa kama hekaya na visasili, na sikuweza kuelewa jinsi watu wanavyoweza kumwamini Mungu au Mwana wake. Sikuweza kuwaamini wale ambao walisema walimwamini Mungu kwa sababu walikuwa wanafiki. Walitenda dhambi kama mimi, au hata zaidi yangu. Najua hayo kwa sababu tulijuana kwa karibu. Sote tulikuwa kundi la mifupa mikavu iliyokufa. Ningepandwa na hasira kama yeyote angethubutu kunigeuza niingie kwenye Ukristo kwa sababu, kwangu mimi Biblia ilikuwa ni upotezaji wa muda tu. Maisha niliyoishi hayakunipa muda wa michezo wala hadithi za kubuni.

Katika ulimwengu wa kibiashara nilichukuliwa kuwa namba moja. Nilikuwa nikihusika katika ufanikishaji wa shughuli za waimbaji na waigizaji wengi wa kimataifa, na pia kutangaza kwa mafanikio bidhaa nyingi za matumizi ya nyumbani. Nilichoogopa kabisa wakati huo kilikuwa kwamba kama ningeokoka ningesambaza kwenye kona mitaani vipeperushi vya injili inavyomhusu Yesu, ningeishi kwenye misheni duni na yenye kelele, ningehubiri injili na kupanga watu wenye njaa kwenye mistari ili wapate chakula.

Mnamo katikati ya miaka ya 60, dunia haikuonekana nzuri kwangu. Sikupenda madawa ya kulevya au watu wachafu waliokuwa na maadili ya nguruwe. Nilichukia sana kile ambacho vuguvugu la Hipi lilikuwa likifanya kwa Hollywood, Sunset Strip na dunia nzima. Kwangu mimi mwenyewe, sikuwa mtakatifu. Sikujali kile watu walichokuwa wakikifanya hasa katika kutenda dhambi, ila tu wasikifanye hadharani kwa lengo la ushawishi mbele ya familia yenye watoto. Kwangu mimi, dunia ilikuwa imekwisha, imekufa, imekauka, ya kuchukiza na isiyo na matumaini.9 Hakukuwa na kitu kilichokuwa na thamani yoyote tena. Naamini watu wengine hapa dunia waliyafahamu haya kama mimi nilivyoyafahamu, na ndiyo sababu walitumia madawa ya kulevya ili waweze kuepuka uhalisia wa hayo. Makanisa yalikuwa manafiki; kila mmoja alionekana kufahamu hilo pia. Dunia nzima ilikuwa imekufa katika dhambi na makosa yake.10 Dunia ilikuwa bonde kubwa la mifupa mikavu, sawasawa na lile aliloliona Ezekieli.11

Nilikutana na Yesu nikiwa katika ofisi ya Beverly Hills kwa  njia isiyokuwa ya kawaida. Hakuna mtu anayeweza kufikiria namna nilivyokuwa na hofu na bado nikawa na furaha pia wakati Mungu aliponithibitishia kuwa yeye na Mwana wake wapo na wanaishi. Nilisisimka kukutana na Roho Mtakatifu wake wa ajabu na kuisikia sauti yake yenye nguvu ikipita kila sehemu ya kiungo cha mwili wangu kana kwamba nilikuwa kichujio; ambapo maneno yake yalikuwa yakienda mbele na kurudi nyuma. Uwepo wake ulijawa na utukufu na joto. Roho wake alinigandamiza kwa nguvu sana kama vile nilikamatwa kwa nguvu na mkono wa Mungu. Kisha akaniambia maneno haya, “Simama kwa miguu yako mwenyewe na uwaambie watu walio kwenye chumba hiki habari ya Bwana Yesu Kristo, na kwamba anarudi tena ulimwenguni, usipofanya hivyo kwa hakika utakufa.” Wakati Roho wake alipokuja ofisini na kunigandamiza, nilipewa ufahamu wa hekima yake ya ajabu isiyoweza kuelezeka.12 Alikuwa kila chembechembe na molekuli kwangu. Alikuwa [kama] hewa. Alijua kila kitu cha siku zilizopita na kila kitu ambacho kingetokea katika siku zijazo.13 Niliteseka kwa kuwa nilijua kwamba alifayahamu yote niliyokuwa nimeyatenda. Kisha akanionesha kwamba, Mbingu na Jehanamu kwa hakika zipo. Katika sehemu hizi mbili nilifahamu ni ipi niliyokuwa nikielekea kama sitafanya alichoniambia…na haikuwa Mbinguni.

Ingawa lilikuwa jambo la kuniogofya,14 pia lilikuwa jambo la ajabu na la kustaajabisha kujua kwamba, kwa hakika Mungu yupo na anaishi na kila kitu walichosema manabii na mitume kumhusu yeye ni kweli. Hajabadilika kamwe tangu siku alipoumba mbingu, dunia na vyote vilivyomo.15 Kwa haraka nilijua kwamba, daima nitamhofia, nitamhusudu, nitamheshimu, nitampenda na kumtumikia. Nilijua kwamba nitakuwa tayari zaidi ya kuishi, kuteswa na kufa kwa ajili yake na kufanya hivyo kwa uchangamfu na furaha yote.16

Baada ya Mungu kuniondoa kutoka kwenye ofisi ile, nilianza kumwuliza, “Unataka nifanye nini? Nitafanya chochote utakachosema.” Sikupata jibu, hivyo nikaanza kufikiria kuwa alitaka niende kanisani. Nilifikiria kanisa kubwa ndilo bora; hivyo nikaenda huko, lakini sikumpata huko. Basi nikaenda kwenye makanisa mengine, lakini hata huko pia sikumpata. Kisha nikasoma vitabu ambavyo majalada yake yalikuwa na picha za watu walioonekana wenye hekima na wamchao Mungu, wenye ndevu ndefu na mavazi ya kidini, lakini nilijua vitabu hivi vilikuwa na kasoro kwa maana vilisema kuwa Mungu si wa kuogopwa,17 kwamba Mungu hawatishi watu, na kwamba unaweza kutenda dhambi na usiende Jehanamu.18 Sikumwogopa Mungu wa aina hiyo; nilimwogopa Mungu aogofyaye,19 Mungu aliyenionesha Mbingu na Jehanamu; akanifanya nitende kitu ambacho hakuna mwanadamu yeyote ambaye angenifanya nikitende, kitu ambacho sikutaka kukitenda.

Sikuwahi kufikiria kwamba ukweli ungeweza kupatikana kwenye Biblia, kwani zilikuwepo kweli nyingi na zilipatikana kila mahali. Nilihisi kwamba kitu ambacho watu wengi walivutiwa nacho hakikuwa kizuri, kwani niliamini kuwa watu wote walikuwa wapumbavu. Hatimaye nilianza kusoma Biblia, na humo ndani niligundua mpango wa wokovu na maelekezo ya uzima wa milele ambayo yalieleza namna ya kukua katika Kristo na kukua kiroho ili niwe chombo kikuu cha kuleta watu kwa Yesu.20

Wakati nilipoanza kusoma Biblia, nilihisi kuwa nguvu zile zile za Mungu zilikuwa zikinigandamiza, ambazo nilizihisi nilipokuwa kwenye ofisi huko Beverly Hills. Kisha Mungu akanionesha maono mengine ya Mbinguni na Jehanamu.21

Nikamlilia Mungu, “Bwana, usinipeleke Jehanamu!” Kisha nikapaona Mbinguni na kujisikia amani ya Mbinguni.22 Ingawa nilikuwa kipofu, uchi na mchanga kiroho, nilimwambia Mungu kuwa ningependa kubakia kipofu, uchi na nisiye na umuhimu wowote kama daima nitaendelea kuisikia amani hii ya mbinguni. Kwa mara nyingine tena nikaiona Jehanamu na nikamlilia Mungu anirehemu na kunisamehe. Kisha  nguvu za Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ziliingia mwilini mwangu.23 Kwa imani yangu katika Yesu na damu aliyotoa kwa ajili yangu, na kwa imani yangu katika Neno la Mungu nililolisikia na kulitii;24 nilijisikia kila dhambi niliyokuwa nimeitenda ikiondolewa rohoni mwangu.25 Nilijisikia msafi na niliyetakasika.26 Kitu cha ajabu sana kilikuwa kimenitokea, na kilifanywa kwangu na kwa ajili yangu na Kristo Yesu, “Mtakatifu wa Israeli.”27 Nilikuwa mwenye furaha sana kuwa huru kutoka dhambini na kumiliki nguvu hizi mpya ambazo zilinifanya nisitende dhambi ambazo nilitaka kuiambia dunia yote ili nao waweze kumjua yeye na kupata uzima wa milele.

Hata baada ya kuwa kwenye huduma ya Kristo tangu mwaka 1964, kila nisomapo Biblia ninahisi afya ya kiroho ikitiririka kutoka mbinguni na kuingia kwenye mifupa hii ambayo wakati mmoja ilikuwa mikavu. Neno la Mungu limeweka mishipa ya kutia nguvu ya kiroho kwenye mifupa hii ambayo wakati mmoja ilikuwa mikavu, na kuiwekea nyama na ngozi ambayo ni silaha ya kiroho. Kila Neno la Mungu limempandikiza Yesu zaidi moyoni mwangu. Bado ninaweza kuhisi kila Neno la Mungu likipumua pumzi ya Roho Mtakatifu nafsini mwangu, likinipatia nguvu za kusimama na kuzima mishale yote ya Shetani aliyonirushia kwa miaka mingi. Kila siku ninazidi kufahamu kwamba “sisi ni zaidi ya washindi” katika Kristo Yesu,28 na “tumekamilika ndani yake.”29 Na pia ninafahamu jinsi ilivyo muhimu sana kufuata kila Neno la Yesu; ambaye alisema, wakati mfupi kabla tu ya kupaa kwenda Mbinguni mawinguni, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe.” 30 (Hubiri kwa kila mfupa mkavu, yaani wale ambao ni wafu kiroho ili wapate kusikia “Neno la Bwana” 31)
“Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.”32

Iwapo wewe ni kama mimi na hungetaka kuangamizwa bali uokolewe, omba sala hii kwa Mungu:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Haki ya kunakili Novemba 1995, Machi 2012, 2013, 2014  Haki zote zimehifadhiwa World Pastor Tony Alamo   ® Tarehe ya Usajili Novemba 1995, Machi 2012, 2013, 2014
SWAHILI—Vol. 06000—Tony Alamo’s Testimony—Dry Bones


footnotes:

1. Eze. 36:1, 4 return

2. Eze. 37:3, asili yake ni Kiebrania return

3. Eze. 37:4-5, asili yake ni Kiaramu return

4. Eze. 37:11 return

5. Mwa. 17:4-16; 22:18; 26:4; 46:3; 48:19; 49:10; Kut. 19:6; 32:10; Zab. 22:27; Isa. 2:2; Yoh. 11:51-52; Mdo. 10:34-35; Efe. 1:10; Ebr. 8:8-12; 1 Pet. 2:9-10; Ufu. 5:9; 14:6 na vifungu vingine vingi. return

6. Yoh. 15:1; Rum. 11:17; 19, 23, 24; Ufu. 7:4 return

7. 1 Pet. 2:9 return

8. Rum. 15:12; 1 Kor. 15:15, 16; Kol. 2:12; 3:1; 1 Thes. 4:16; Ufu. 20:5-6 return

9. Mat. 13:39, sura 24; 1 Kor. 15:24; Ebr. 9:26; 1 Petro 4:7 return

10. Efe. 2:1, 5; Kol. 2:13 return

11. Eze. 37:1 return

12. Hes. 24:16; 1 Sam. 2:3; Ayu. 21:22; Zab. 32:8; Mit. 2:6; 3:20; 9:10; Lk. 1:77; Rum. 11:33; 1 Kor. 1:25; 2:16; 3:19; 2 Kor. 4:6 return

13. Zab. 44:21; 94:11; Isa. 46:9-10; 1 Kor. 3:20; 1 Yoh. 3:20; Ufu. 21:6, 22:13 return

14. Mwa. 35:5; Law. 26:16; Ayu. 31:23; Yer. 32:21; Eze. 32:32; 2 Kor. 5:11 return

15. Mwa. 1:1; Mal. 3:6; Mdo. 4:24; 2 Kor. 5:11; Ebr 13:8 return

16. Zab. 5:11; 35:19; Isa. 51:11; 61:10; Yoh. 16:33; Mdo. 2:28; 20:24; Rum. 12:8; 15:13; 2 Kor. 8:12 return

17. Mwa. 22:12; Zab. 112:1; Mit. 13:13; 14:16; 28:14; 31:30; Mhu. 7:18 return

18. Mit. 8:36; Eze. 18:2, 4; Ufu. 19:20; 20:10, 14, 15; 21:8 return

19. Mwa. 2:17; 6:7, 9, 13; Kut. 20:5; 32:33; 34:7; Eze. 3:18; 18:20; Mat. 8:12; 22:13; Mk. 16:16; Ufu. 2:5, 16, 22-23; 3:3; 20:15 return

20. Yoh. 4:35-36; 15:5, 8, 15-16; Ufu. 14:18 return

21. Isa. 5:14; 14:9; Lk. 16:22-31; Mdo. 7:55-56; Ufu. 4:1-11; 14:10-11; 15:1-4; 20:10; 21:2-5, 10-27; 22:1-5 return

22. Rum. 5:1; Efe. 2:14; Flp. 4:7; Kol. 3:15; 1 Thes. 5:23; 2 Thes. 3:16 return

23. Law. 26:11-12; Yoh. 14:16; 2 Kor. 6:16; 1 Pet. 2:5; 1 Yoh. 3:24 return

24. Hab. 2:4; Mat. 17:20; Lk. 7:50; Mdo. 20:21; 26:18; Rum. 1:17; 3:28; 5:2; 10:17; 11:20; Gal. 2:16; 3:11; Efe. 2:8; 3:17; Ebr. 10:38 return

25. Mk. 14:24; Yoh. 6:53; Mdo. 20:28; Rum. 3:25; 5:9; Efe. 1:7; 2:13; Kol. 1:14, 20; Ebr. 9:12, 14, 22; 1 Pet. 1:18-19; Ufu. 1:5, 5:9 return

26. Ebr. 10:19-22; 1 Yoh. 1:7; Ufu. 1:5; 7:14 return

27. Zab. 89:18; Mdo. 3:13-14 return

28. Rum. 8:37; 1 Yoh. 4:3-4 return

29. Kol. 2:10 return

30. Mk. 16:15; Lk. 14:23 return

31. 2 Fal. 20:16; Isa. 1:10; Yer. 2:4; Eze. 37:4 return

32. Mk. 16:16; 2 Thes. 2:12 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return