UNYAKUO?

na Tony Alamo

Biblia inasema watu pekee watakaonyakuliwa kutoka kwenye mapigo makuu saba ya kwanza, au hata yale makuu saba ya mwisho ya kipindi cha Dhiki Kuu, ni mashahidi wawili wa Mungu waliotajwa katika sura ya kumi na moja kitabu cha Ufunuo sura ya nne ya Zekaria.1

Mashahidi wawili si Musa na Eliya, kama wengi wanavyofundisha. Musa alikufa na alizikwa.2 Yesu alisema Yohana Mbatizaji alikuwa Eliya.3 Alichinjwa akiwa gerezani, alikatwa kichwa, na alizikwa.4 Wote, Eliya na Musa (roho zao), ziliongea na Yesu katika mlima uliogeuka sura!5 Naamini Henoko na mkewe watakuwa mashahidi wawili. Henoko anapaswa kufa! “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Waebrania 9:27).

Yesu alisema, “Nami nitawaruhusu [mamlaka] mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia” (Ufunuo 11:3). (“Kuvikwa magunia” inamaanisha watakuwa wakifunga.6) “Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za bwana wa nchi” (Ufunuo 11:4, Zekaria 4:11-14).

Mashahidi hawa wawili wa Mungu wametajwa pia katika Agano la Kale kitabu cha Zekaria 4:2-3, 11-14. Malaika wa Bwana alimuuliza nabii Zekaria nini kile alichokiona. Naye nabii akamwambia malaika, “Nimeona, na tazama, kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli [uzima wa milele, Neno] juu yake, na taa zake saba [Roho saba za Mungu: (1) “Roho ya Bwana…(2) Roho ya hekima na (3) Roho ya ufahamu, (4) Roho ya ushauri na (5) Uweza, (6) Roho ya maarifa na (7) Kumcha BWANA” (Isaya 11:2, Ufunuo 1:4)] juu yake; tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwa taa zote zilizo juu yake; na mizeituni miwili [ishara ya mashahidi wawili] karibu yake, mmoja upande wa kuume wa lile bakuli [la uhai], na mmoja upande wake wa kushoto” (Zekaria 4:2-3).

“Ee Bwana wangu, vitu hivi ni nini?” Zekaria alimuuliza malaika. “Ndipo malaika aliyesema nami [Zekaria] akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo wala, si kwa nguvu, bali ni kwa Roho Yangu, asema Bwana wa Majeshi” (Zekaria 4:4-6). Mashahidi hawa wawili wa Mungu hawatendi kwa nguvu zao wenyewe, au uweza wao wenyewe, bali kwa nguvu ya Mungu, Kristo, Roho Mtakatifu.7

Zerubabeli ndiye aliyesaidia kuwaongoza wana wa Israeli kurudi toka utumwani wa miaka sabini kule Babeli hadi Israeli.8 Wote walifikishwa kwa Roho Mtakatifu wa Bwana. “Nani wewe, Ee mlima [majaribu na dhiki] mkubwa [ugumu]? Mbele ya [Roho Mtakatifu] Zerubabeli utakuwa tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa [Jiwe la kuwekwa juu, Jiwe Kuu la Pembeni la jengo la Mungu, kanisa, ni Kristo katika Israeli ya kiroho, kichwa cha mwili wa Kristo] pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie” (Zekaria 4:7).

Roho ni sawa na mashahidi wawili wa Mungu, wanaosimama mbele ya mungu wa dunia (ibilisi). “Si [kutendeka] kwa uwezo, wala si kwa nguvu [zao], bali kwa Roho Yangu, asema Bwana wa Majeshi” (Zekaria 4:6).

Zekaria akauliza, “Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni, ambayo kwa njia ya ile mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta ya dhahabu [Neno la Mungu kupitia kwa Roho Mtakatifu] kutoka ndani yao?...Ndipo akasema [malaika], Hawa ni wale wawili waliopakwa  mafuta, wasimamao karibu na bwana wa dunia yote [ibilisi]” (Zekaria 4:12, 14).

Ufunuo, sura ya kumi na moja inasema, “Hao [mashahidi wawili] ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za bwana wa nchi [ambaye ni ibilisi]. Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao` na kuwala adui zao. Na akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa. Hao wana mamlaka ya kuzifunga mbingu ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.

“Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu [roho ya ibilisi, ambaye kiti chake ni Roma, Uroma, iliyopewa mamlaka na shetani, dunia-moja, mpinga Kristo, mpinga dini za Marekani na mfumo wake wa serikali, serikali ya kidunia na dini9] atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua. Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu, uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulubiwa. [Dunia nzima  imekuwa kama Sodoma, Misri, na mahali ambapo Bwana anasulubishwa kila siku, na siri hii ya Babeli.10] Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu unusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini. [Huu ni unabii wa setilaiti ya televisheni miaka elfu mbili kabla ya televisheni au Televisheni ya setilaiti kufikiriwa, isipokuwa kufikiriwa na Mungu.]

“Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia [kama wafanyavyo leo, wanapowaona Wakristo wakiteswa au kuuawa kwa sababu ya shutuma za uongo – kashfa – kwa kumwabudu na kumtumikia Mungu11]. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi. [Wanateswa nao wanaposikia Neno la Kweli la Mungu likihubiriwa nao, ambalo huwaambia kwamba watateswa katika Ziwa la Moto milele, kwa sababu wao (walio waovu wa dunia) ni wapingaji wa nidhamu ya Kikanisa, wapinzani wa mafundisho ya kweli ya neno la Mungu, wapinga Sheria ya Mungu na hukumu ya mwisho ya Sheria ya Mungu. Wale wanaokinzana na mahubiri ya Injili – watu hawa wa dunia – ni maadui wa Mungu.12]

“Na baada ya siku hizo tatu unusu, Roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia [mashahidi wawili], wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama. Wakasikia sauti kuu kutoka Mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda Mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama” (Ufunuo 11:4-12). Walikufa (waliuawa kama Yesu), kisha wakafufuka baada ya siku tatu unusu, kama ilivyokuwa kwa Yesu Bwana wetu. Kisha, kama Bwana, walitwaliwa Mbinguni katika wingu.13 ASANTE MUNGU BABA! ASANTE, YESU!!

Usiruhusu manabii wa uongo wakudanganye tena. Hakuna unyakuo isipokuwa huu!! Na baada ya watumishi wa Bwana kutiwa muhuri, ndipo mateso makuu saba na ya mwisho yatakapoanza (Ufunuo 7:3-8).14

Manabii wa uongo hukwambia kwamba Bwana atakuja kuwachukua ninyi nyote mliodanganyika, watu waovu kabla ya mateso, lakini Yesu husema kinyume kabisa.15 Yesu anasema, “Mwamini BWANA YESU KRISTO [aliye Njia, na KWELI, na Uzima (Yohana 14:6)], nawe utaokoka” (Matendo 16:31). Hupaswi kuwaamini manabii wa uongo ambao wanakwambia ni sahihi kutenda dhambi, nawe utaokoka.16

Kama unawaamini manabii wa uongo, utatupwa milele jehanam pamoja nao, na katika Ziwa la Moto pamoja nao, na hii ni hakika.17

Hiki ndicho Bwana Yesu asemacho katika Mathayo 24:29-31: “Lakini mara, BAADA ya dhiki ya siku zile [siyo kabla], jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.” 

Ikiwa umeokoka na ukafa, utakuwa pamoja na Bwana, lakini kama ukiishi, utapitia mateso.18 Hakuna mwenye uhakika kama utakuwa hai saa moja ijayo.19 Kama hujaokoka, Sali sala hii kwa Mungu nawe utakuwa umeokoka:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Hatimiliki, Desemba 2010  Haki zote zimehifadhiwa Mchungaji wa Ulimwengu Tony Alamo ® Imesajiliwa Desemba 2010
SWAHILI—VOLUME 11500—RAPTURE?


footnotes:

1. Dan. 7:24-25, Zek. 4:3, 11-14, Mat. 24:3-31, Mk. 13:19-27, Lk. 21:10-12, 16, 23, 25-36, Ufu. 7:13-14, 11:3-12 return

2. Hes. 31:2, Kumb. 32:48-50, 34: 1-8 return

3. Mat. 11:13-15, 17:11-13, Mk. 9:11-13, Lk. 1:13-17 return

4. Mat. 14:2-12, Mk. 6:17-29 return

5. Mat. 17:1-13, Mk. 9:2-13, Lk. 9:28-36 return

6. Mwa. 37:34, 2 Sam. 3:31, 1 Fal. 21:27, Neh. 9: 1, Esta 4: 1-3, Zab. 35:13, Dan. 9:2-3, Yona 3: 5 return

7. Isa. 59:19-21, Zek. 4:6, Yoh. 14:12, 15-20, 16:33, Mdo. 1:8, Rum. 8:11, 1 Yoh. 4:4, Ufu. 11:3 return

8. Ezr. 2:1-2, 3:1-2, 8, 5:2, Neh. 7:6-7, 12:1, Hag. 1:1-14, 2:1-4, 20-23 return

9. Dan. 7:3-8, 16-27, 11: 6-45, 2 Thes. 2:3-10, Ufu. 13:1-18, 16:13-14, 17:1-18, Sura ya 18 return

10. Dan. 11:30-33, Mat. 24:9-13, 21-24, 37-39, 2 Thes. 2:3-12, 2 Tim. 3:1-5, 13, 2 Pet. 3:3-7, 1 Yoh. 2:18-19, Ufu. 13:3-8, 14:8-11, 16:4-7, 17:1-6, 18:1-19, 24, 19:1-2 return

11. Mat. 23:34-35, Lk. 21:12-17, Yoh. 15:18-21, 16:1-2, 17:14, 1 Kor. 4:9-13, 2 Kor. 4:8-11, 6:4-5, 2 Tim. 3:12, 1 Pet. 1:6-7, 3:14-17, 4:12-14, Ufu. 2:10 return

12. Dan. 7:19-25, Mat. 5:1-12, 10:16-18, 21-25, 23:34-35, Mk. 8: 33-38, Lk. 21:12-17, Yoh. 15:18-25, 17:14, Gal. 4:28-29, Flp. 3:18-19, 2 Thes. 2:10-12, 2 Tim. 3:12, Yak. 4:4, 1 Yoh. 2:15-17 return

13. Lk. 24:50-51, Mat. 1:9-11, 1 Kor. 15:3-6 return

14. Ufu. 7:2-8, 9:4, 15:1,6-8, 16:1-12, 17-21 return

15. Dan. 7:24-25, 11:32-35, Mat. 24:3-44, Mk. 13:19-20, 24-27, Lk. 21:20-28, 1 Thes. 4:14-18, 5:2-9, Ufu. 6: 8-11, 7:13-17, 20:4 return

16. Eze. 18:4, 33:12-13, Mat. 5:13, 12:43-45, Lk. 9:62, Yoh. 15:6, Kol. 1:21-23, 2 Thes. 2:3, 1 Tim. 1:19, 2 Tim. 2:12, Ebr. 3:6-19, 4:1-11, 6:4-8, 10:25-31, 38-39, 2 Pet. 2:20-22, 1 Yoh. 3:6-10, 2 Yoh. 9, Yuda 5-6, Ufu. 2:4-5, 3:2-3 return

17. Hes. 16:1-35, Kumb. 13:1-4, Zab. 9:17 Yer. 5:26-31, 14:14-15, 23:25-27, 30-32, Mat. 5:19-20, 7:15-27, 15:7-9, 14, 23:13-15, 23-33, 24:48-51, 1 Thes. 5:2-3, 2 Tim. 4:1-4, 2 Pet. 2:1-9, Yuda 3-16, Ufu. 20:10-15 return

18. Dan. 7:21-25, 12:1-12, Mat. 24:13-22, 29-31, Lk. 21:25-36, 1 Thes. 4:13-18, Ufu. 6:8-11, 7:13-17, 13:7-10, 20:4 return

19. 2 Sam. 14:14, 1 Nya. 29:15, Ayu. 8: 9, 14:1-2, Zab. 22:29, 49:7, 90:3-10, 102:11, 103:15-16, 144:4, Isa. 40:6-8, Lk. 12:16-21, Yak. 1:9-11, 4:13-15 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return