KUWA NA KRISTO NDANI YAKO

na Tony Alamo

Jinsi tunavyozidi kumfahamu YESU zaidi, tunafahamu kwamba YEYE ni zaidi ya kila kitu. Kama tukimfuata KRISTO, tutaishi maisha tofauti na yale ulimwengu unaoyataka. Mateso tunayopata ni beji yetu ya heshima.

Kumwona YESU ni kumwona BABA.1 “Filipo AKAMWAMBIA, BWANA, utuonyeshe BABA, yatutosha. YESU akamwambia, Mimi nimekuwepo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona MIMI amemwona BABA; unasemaje sasa, utuonyeshe BABA?” (Yohana 14:8-9).

Sisi wanadamu tunapaswa kuuliza kila jambo kwa kupitia NENO la MUNGU.2 “Yeye anikataaye MIMI, na asiyeyakubali maneno YANGU, anaye amhukumuye; NENO hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho” (Yohana 12:48).

Daima mshukuru MUNGU kwa kila ulicho nacho.3 Mwombe MUNGU akutie nuru kama alivyo YEYE. NENO LAKE hututia nuru kuhusu jinsi tunavyofaa kutembea katika NENO la MUNGU, ROHO MTAKATIFU, si tu siku ya Sabato pekee, lakini kila siku, kwa sababu kila siku ni Sabato.4 Tunapumzika, Sabato, katika BWANA daima tukiacha njia zetu mbaya za kale (Waebrania 4:1-11).

Moyo wangu u katika Moto Mtakatifu kwa ajili ya ROHO MTAKATIFU. Uwe radhi kuwasaidia wengine kuubeba msalaba (Wagalatia 6:2). YESU alikuja kwa ajili ya wagonjwa na wala sio wenye afya! YESU alisema, “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuwaita wenye haki, bali wenye dhambi” (Marko 2:17). 

Wakatoliki wanaamini kuwa kuna hukumu mbili, ya kwanza ikiwa ni pagatori. Hii si kweli. Hakuna pagatori!5 NENO LA MUNGU linasema, “Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja na baada ya kufa hukumu [hukumu moja, hakuna kuzaliwa katika mwili mwingine]” (Waebrania 9:27). Maisha ya milele ni milele. Wakatoliki wanaamini mno katika umizimu na uzushi.

Ikiwa tumezaliwa upya, hatutendi dhambi, kwa sababu yeye atendaye dhambi ni wa Ibilisi.6 “Atendaye dhambi, ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo” (1 Yohana 3:8). Sisi si watenda dhambi, bali wana wa MUNGU, uzao wa kifalme na kikuhani! “Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU” (Warumi 8:14). “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya MUNGU, mpate kuzitangaza fadhili ZAKE yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru YAKE ya ajabu” (1 Petro 2:9).7

YESU anasema katika Mathayo 10:40, “Awapokeaye ninyi, anipokea MIMI; naye anipokeaye MIMI ampokea YEYE aliyenituma.” YESU anasema, kama hunipokei mimi, Tony Alamo, ninayehubiri ukweli ambao NENO la MUNGU linasema, humkubali YESU, na humkubali BABA. Ukiangalia maneno anayosema YESU, wapo watu wengi wanaotupokea!

Watu hujidanganya kwa kusema kwamba MUNGU HAJIONDOI kamwe kutoka kwa watu ambao WAMEMFAHAMU;8 lakini wapo wengi ambao wamemruhusu Shetani kuingia ndani yao na kuwatumia.9 Uwepo wa MUNGU, ROHO WAKE, vimeondoka kwao bila ya wao kutambua!10

Mema huwajia wenye subira. “Ninyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu” (Luka 21:19).

Kwa nini Wakatoliki wengi wanasema lugha ya Kilatini ni lugha takatifu wakati Biblia HAIKUANDIKWA na Warumi, ila wale waliokuwa Waebrania, waliozungumza Kiebrania, Kiaramu na Kiyunani cha Kiheleni, Kiyunani kilichokuwa kikizungumzwa na Wayahudi? Wayahudi ni watu ambao MUNGU aliwatumia kupokea ROHO ili kuandika Maandiko Matakatifu, SI Warumi hata kidogo! Petro hakuwahi kuwa Papa; alikuwa mmoja wa wanafunzi wa KRISTO, na pia mtume wa KRISTO.11 YESU ametuonya kukaa mbali na manabii wa uongo na dini za uongo.12 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wenye njaa kali” (Matayo 7:15).

MUNGU hakusema kamwe kwamba ndoa ni lazima iwe ya mke mmoja.13 Watakatifu wengi walikuwa na mke zaidi ya mmoja.14 Mwanamke anaweza kuwa na mume mmoja tu.15 MUNGU, KRISTO, kamwe halaani hili, lakini analaani ushoga na ndoa za jinsia moja na kila aina ya ushoga!16

YESU ni NENO la MUNGU (Yohana 1:1, 14). Kumjua YESU ni kulijua NENO la MUNGU. YESU, NENO, pia ni ROHO MTAKATIFU na Uzima wa Milele. Ili upate Uzima wa Milele, lazima KRISTO awe ndani yako kupitia ROHO MTAKATIFU. Ili hili litokee, Sali sala hii:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Hatimiliki Aprili 2011 Haki zote zimehifadhiwa World Pastor Tony Alamo ® Imesajiliwa Aprili 2011


footnotes:

1. Yoh. 8:19, 10:30, 38, 14:7-11, 20, 23, 15:24, 17:21 return

2. 1 Kor. 2:12-16, 6:1-4 return

3. Zab. 100:4, Rum. 1:21, Efe. 5:2-5, 17-20, Kol. 1:10-13, 3:15-17, 1 Thes. 5:18, Ebr. 13:15 return

4. Mat. 11:28-30, Rum. 8:1-6, Ebr. 4:9-10 return

5. Mat. 25:31-46, Ebr. 9:27, 10:26-29, Ufu. 20:12-15 return

6. Rum. 6:1-4, Gal. 2:16-20, 1 Yoh. 3:9 return

7. Ufu. 1:6, 5:10 return

8. Kumb. 31:16-18, Yos. 24:20, 1 Sam. 15:16-28, 1 Nya. 28:9, Eze. 33:12-13, Mat. 12:43-45, Lk. 9:62, Yoh. 15:6, Kol. 1:21-23, 2 Tim. 2:12, Ebr. 3:6-19, 4:1-11, 6:4-8, 10:25-31, 38-39, 2 Pet. 2:20-22, 2 Yoh. 9, Yud. 5-6, Ufu. 2:4-5, 3:2-3 return

9. 1 Sam. 15:11, 16:14, 28:7-19, 31:1-6, 1 Fal. 3:3-14, 9:1-9, 11:1-34, Mat. 10:1-4, 26:14-16, Yoh. 13:1-2, 21-27, 18:1-5, 2 Pet. 2:18-22 return

10. Amu. 16:20 return

11. Mat. 10:2, Lk. 6:13-14, 1 Pet. 1:1, 2 Pet. 1:1 return

12. Mat. 16:6-12, 24:11, 24, Mk. 8:15-21, 12:38-40, 13:21-23, Lk. 12:1-2, 20:46-47, 2 Pet. 2:1 return

13. Kut. 21:10, Kumb. 21:15-17, 25:5-6, Amu. 8:30, 12:8-9, 13-14, 2 Sam. 3:2-5, 5:13-16, 12:7-8, Isa. 4:1, Mat. 5:17, 1 Tim. 4:1-3 return

14.Mwa. 16:1-3, 25:6, 29:20-29, 30:4, 9-10, Kut. 2:21, Hes. 10:29, 12:1, Amu. 8:30-31, 1 Sam. 1:1-3, 25:39-44, 2 Sam. 3:2-5, 5:13, 15:16, 1 Nya. 1:32, 2:46-48, 14:3, 2 Nya. 13:21, 24:2-3, Hos. 1:2-3, 3:1-2 return

15. Law. 20:10, Matt. 5:32, 19:3-9, Rum. 7:1-3, 1 Kor. 7:39 return

16. Mwa. 19:1-13, 24-25, Law. 18:22, 20:13, Kumb. 23:17, Amu. 19:22-25, 1 Fal. 14:24, 15:11-12, Rum. 1:20-32, 1 Kor. 6:9-10, 1 Tim. 1:9-10, 2 Tim. 3:1-5, Yud. 7 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return