AGANO LA PALESTINA

na Tony Alamo

Mwishoni mwa Zama za Shaba (Bronze Age) mnamo miaka ya (1500-1200 KK), wana wa Israeli walienda Kanaani. Waliuteka Palestina mnamo mwaka 1400 K.K. kwa mujibu wa Utaratibu wa miaka na matukio wa Kimasoreti (Masoretic Chronology).1 Wapalestina walikuwa sehemu ya Kanaani. MUNGU aliwaamuru wana wa Israeli kuharibu Kanaani (Wakanaani), pamoja na mataifa mengine. Kama wana wa Israeli wasingewaangamiza, kila waliyemruhusu kuishi angekuwa mwiba kwao.2

Historia ya Wapalestina inarejea nyuma hadi kwa Kanaani, mwana wa Hamu. Kanaani aliye mwana wa Hamu ni baba wa Sidoni (Mwanzo 10:15-20), yaani, ujamii wa Kifoeniki [Phoenician race] (ulio asili ya watu weusi), Hethi (yaani Wahiti), na Wayebusi, na Waamori, na Wagirgashi, na Wahivi, Waferai:Waarki (watu wa Arka), na Wasinai, na Warvadi, watu wa Tarto,  Wazemari, watu wa Sumra, Wahamathi, Wakanaani wote – kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, Sodoma na Gomora, vilevile Adma, Seboimu, Lasha, na Warefai – hawa wote walikuwa watu wakubwa (Kumbukumbu 2:11, 20). Waamori, Waemu (majitu makubwa), Wazamzumi au Wazuzimu-zuzim, Waamoni (au Hamu), na Waanaki, (au Waanakimu) pia walikuwa majitu makubwa (Kumbukumbu 03:11, Hesabu 13:33).3 Kanaani ni baba wa vizazi vyote hivi vya kiafrika, au vyote vya Palestina.4

Agano, ambalo waweza kuliita agano la Palestina, au mkataba kwa mataifa yote, ni tu kwamba Mungu amewaahidi Wapalestina, Waarabu, Iraki, Irani, Lebanoni, Korea, na mataifa yote kwamba ardhi ya Israeli ni mali ya Israeli (Wayahudi)!!5 Hili pia ni agano la Urusi, agano la China, agano la Amerika ya Kaskazini, agano la Amerika ya Kusini, agano la Amerika ya Kati, na agano la mataifa yote. Hili ni agano la MUNGU kwa Israeli, Palestina, Marekani, Urusi, Uingereza, China, Waarabu na dunia yote!!

UMUHIMU WA AGANO HILI LA DUNIA

Kuna umuhimu mkubwa unaohusishwa na agano hili: (1) Linaithibitisha Israeli kwa mara nyingine, bila masharti yoyote, kwamba hati miliki ya nchi ya ahadi bado ni mali ya Israeli (Wayahudi). Haijalishi kuwa kipindi chote kilichopita wamekuwa wazembe katika kumtumikia MUNGU. MUNGU anajua  mioyo yao, na kile alichoahidi kitakuja kutokea.6 MUNGU anajua kutokuamini kwao kutageuka kuwa imani:7 Hili linatokea sasa!  Nchi hii bado ni mali ya Israeli, kwa mujibu wa ahadi ya MUNGU. (2) Zaidi ya hayo, kuanzishwa kwa agano lililo na masharti ambalo kwalo Waisraeli waliishi, hakukuweza wala hakukuitenga ahadi asilia ya neema yenye kuhusiana na kusudi la MUNGU. Ukweli huu ndio msingi wa hoja ya Paulo wakati aandikapo, “agano, lililothibitishwa kwanza na MUNGU [katika KRISTO], torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye, hailitangui wala kuibatilisha ile ahadi” (Wagalatia 3:17). (3) Agano hili ni uthibitisho na upanuzi wa agano la awali la Ibrahimu.8 Agano hili la Palestina au agano la dunia linaongeza sehemu ya ardhi ya agano la Ibrahamu. Ongezeko, linalokuja baada ya kutokuamini na kuasi kwa makusudi katika uhai wa taifa hili, linaunga mkono hoja kuwa ahadi ya awali ilitolewa ili itimizwe licha ya uasi.

UTOLEWAJI WA AGANO LA WAPALESTINA NA LA DUNIA

Hili liitwalo agano limetajwa katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 30:1-3, 5-9: “Tena itakuwa, mambo haya yote yatakapokujilia, Baraka na laana nilizoweka mbele yako, nawe utakapozikumbuka kati ya mataifa yote, huko atakapokupeleka BWANA MUNGU wako, nawe utakapomrudia BWANA MUNGU wako, na kuitii sauti yake, mfano wa yote nikuagizayo leo, wewe na wanao kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; Ndipo BWANA MUNGU wako atakapougeuza utumwa wako, naye atakuhurumia, tena atarejea na kukukusanya kutoka mataifa yote, huko alikokutawanyia BWANA, MUNGU wako. [Hii ilitokea mwaka 1948, na inaendelea hadi leo hii.] ... Na BWANA, MUNGU wako, yuakuingiza katika nchi waliyomiliki baba zako, nawe utaimiliki ... Na BWANA, Mungu wako, atautahiri moyo wako, na moyo wa uzao wako, ili umpende BWANA MUNGU wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, upate kuwa hai. Na laana hizi zote, BWANA, MUNGU wako, atawatia adui zako ... Nawe utarudi, uitii sauti ya BWANA, na kuyafanya maagizo YAKE yote nikuagizayo leo. Na BWANA, MUNGU wako, atakufanya uwe na wingi wa uheri katika kazi yote ya mkono wako…kwa kuwa BWANA atafurahi tena juu yako kwa wema.”

Wakati tuchambuapo kifungu hiki cha Maandiko, hapa tunaona kuna sehemu kuu saba za kusudi la Mungu: (1) Taifa litaondolewa kwenye nchi [ya ahadi] kwa sababu ya ukosefu wa uaminifu  (Kumbukumbu la Torati 28:63-68; 30:1-3). (2) Kutakuwa na toba ya Waisraeli katika wakati ujao (Kumbukumbu la Torati 30:1-3). (3) MASIHI wao atarudi (Kumbukumbu la Torati 30:3-6). (4) Waisraeli watarejeshwa katika nchi yao (Kumbukumbu la Torati 30:5). Hili lilitokea mnamo mwaka 1948. (5) Israeli itaokolewa kama taifa (Kumbukumbu la Torati 30:4-8, Warumi 11:26-27). (6) Maadui wa Israeli watahukumiwa (Kumbukumbu 30:7). (7) Kisha taifa litapokea baraka zake kamilifu (Kumbukumbu 30:9).

Ninapojifunza kifungu hiki, naona ahadi mbalimbali zilizotolewa mahali hapa zikieleza (au zinakusudia kueleza) lengo la agano hili, si tu kwa Wapalestina, bali  kwa dunia nzima. Kila mmoja anapaswa kuamini kuwa MUNGU hafanyi mchezo na agano lake, na ni la muhimu sana KWAKE. Si tu kwamba MUNGU anawahakikishia Waisraeli miliki ya nchi, bali pia anajiwajibisha MWENYEWE kuwahukumu na kuwaondoa maadui wote wa Israeli na kuwapa Israeli moyo mpya, na uongofu kabla ya kuwarejesha katika nchi.9

Agano hili hili linathibitishwa katika kifungu kingine cha historia ya Israeli, katika unabii wa Nabii Ezekieli. MUNGU anathibitisha upendo wake kwa Israeli wakati wa uchanga wake (Ezekieli 16:1-7). Analikumbusha [taifa la] Israeli kuwa lilichaguliwa na linahusiana na YEHOVA kwa ndoa (mstari wa 8-14). Hata hivyo, taifa la Israeli lilifanya ukahaba (mstari wa 15-34). Kwa sababu hiyo, adhabu ya kutawanywa ilitolewa juu yake (mistari 35-52). Hili si tangazo la mwisho au kuwekwa kando kwa Israeli, kwa sababu kutakuwa na urejesho (mistari 53-63). Marejesho haya ni msingi wa ahadi ya Mungu: “Walakini nitalikumbuka agano langu nililofanya pamoja nawe, katika siku za ujana wako, nami nitaweka imara agano langu pamoja nawe; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA” (Ezekieli 16:60-62).

Hivyo Bwana anaithibitisha ahadi yake kwa Israeli, kwa dunia, na Wapalestina. Kwa kupitia kwa kina ahadi ya BWANA ya awali, ya mambo ambayo ni lazima yatokee ili ahadi hizi zitimizwe – zishuudiwe zikitimia – tunaona kwamba (1) Israel lazima ibadilishwe kama taifa.10 (2) Ni lazima wakusanyike warudi tena Israeli kutoka pembe nne za dunia.11 (3) Ni lazima Israeli wawe imara katika nchi yao, ambayo walipewa kuimiliki. Ni lazima Israeli ashuhudie hukumu ya adui zake, na lazima apokee Baraka za kimali alizoapiwa.12

Agano hili linapaswa kuwa na ushawishi mkubwa kwa yeyote asomaye unabii huu wa siku za mwisho. Mengi ya mambo haya yameshatimia. Si Waisraeli wote ni Waisraeli.13 Watu wake wamekusanyika. Maelfu yao wanamwamini YESU kama MASIHI wao. Bado hawajashuhudia kuharibiwa kwa adui zao, lakini agano hili ni la milele na lisilo na masharti, na linahitaji utimilifu uliokamilika. Ni dhahiri kwamba wao ni taifa kamili lililoimarika. Jinsi ninavyoona, kutakuwa na mabadiliko zaidi, mateso zaidi na kisha uharibifu kamili kwa wale wote ambao ni maadui wa wateule wa MUNGU na sehemu ya dunia aipendayo MUNGU, Israel (Isaya 11:11-12, 27:12 -13, 43:1-8, 49:8,16, 66:20-22, Yeremia 16:14-16, 23:3-8, 30:10-11, 31:1-19, 31-37, Ezekieli 11:17-21, 20:33-38, 34:11-16, 39:25-29, Hosea 1:10-11, Yoeli 3:17-21, Amosi 9:11-15, Mika 4:01 -8 Zefania 3:14-20, Zekaria 8:1-8). Hii ni ahadi kwa watakatifu hao wote. Haijalishi kama hawataweza kuishi hadi waone utimilifu wa ahadi hizi; wataiona kwa pamoja katika asubuhi ya ufufuo, wataona marudio ya kila kitu. Kama MUNGU alivyoahidi: Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu (kupumzika na kumwangalia MUNGU akitimiza mambo yote), na si mwanadamu kwa ajili ya Sabato (pumziko): Basi MWANA wa ADAMU ndiye BWANA hata wa Sabato (wa mapumziko, na utimilifu) (Marko 2:27-28).

Kutakuwa na amani katika Israeli wakati Mungu atakapoharibu adui zake wote, jambo ambalo liko karibu sana sana!14

Amani itakuwa yako kama ukimkubali YESU MASIHI wa Wayahudi kama BWANA na MUNGU. Itakuwa uharibifu wako kama utapambana NAYE au watu WAKE kama ilivyokuwa kwa Yeriko.15
Mpokee MUNGU kwa kusema sala hii:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Hatimiliki Septemba 2011 Haki zote zimehifadhiwa World Pastor Tony Alamo  ® Imesajiliwa Septemba 2011
SWAHILI—Vol. 13400—The Palestinian Covenant


footnotes:

1. Kamusi Mpya ya Biblia ya Unger, ukurasa. 954 return

2. Kut. 23:27-33, Hes. 33:53-55, Yos. 23:12-13, Amu. 2:1-5 return

3. Kamusi Mpya ya Biblia ya Unger, ukurasa. 956 return

4. Kamusi Mpya ya Biblia ya Unger, ukurasa. 956 return

5. Mwa. 12:1-7, 13:14-17, 15:7, 17:7-8, 26:1-5, 28:1-5, 10-14, 18-19, 35:10-12, 48:3-4, Kut. 6:2-4, 8, 32:13, Law. 20:23-24, Kum. 1:8, Yos. 13:1-6, 1 Nya. 16:12-19, 2 Nya. 20:7, Neh. 9:7-8, Zab. 105:5-11 return

6. Mwa. 17:5-8, 48:3-4, Law. 26:40-45, Kum. 4:29-31, 30:1-5, Zab. 9:10, 105:6-11, 145:18, Isa. 27:6, Eze. 47:13-20, Mik. 7:18-20 return

7. Rum. 9:25-27, 11:19-24 return

8. Mwa. 12:1-3, 7, 15:7, 17:1-8 return

9. Kum. 33:26-29, Isa. 59:18-19, Yer. 31:31-34, Eze. 6:8-10, 11:17-20, 36:24-36, Ebr. 8:10-12 return

10. Zek. 12:1-10, Rum. 11:26-27 return

11. Isa. 11:12, Eze. 39:23-29, Amo. 9:14-15, Zef. 3:17, 19-20, Zek. 8:7-8 return

12. Mwa. 12:1-3, 26:1-5, Kum. 8:18, 28:1-14, Mhu.. 5:19, Isa. 49:26, 66:20-24, Yer. 30:16-24, Eze. 39:1-21, Yoe. 2:18-21, 3:16-21 return

13. Yoh. 4:23-24, Rum. 1:16-17, 9:6-8, 11:2-15, Gal. 3:7-9, 28, Efe. 2:11-22, Ufu. 7:9, 13-15 return

14. Eze. 38:14-23, Sura ya. 39, Zek. 12:1-9, Ufu. 20:7-10 return

15. Yos. 6:2-17, 20-21, 24-25 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return