USHINDI DHIDI YA PONOGRAFIA!

Mifupa Mikavu

na Tony Alamo

ENO LAKO. Kwa moyo wangu wote NIMEKUTAFUTA, usiniache nipotee mbali na maagizo YAKO. Moyoni mwangu nimeliweka NENO LAKO, nisije NIKAKUTENDA dhambi.”

“Ee BWANA umehimidiwa, nifunze amri ZAKO. Kwa midomo yangu, nimezisimulia hukumu zote za kinywa CHAKO. Nimeifurahia njia ya shuhuda ZAKO kana kwamba ni mali nyingi. Nitayatafakari mausia YAKO, nami nitaziangalia njia ZAKO. Nitajifurahisha sana kwa amri ZAKO. Sitalisahau NENO LAKO.”

Zaburi 120:1 inasema hivi, “Katika shida zangu nalimlilia BWANA, naye AKANIITIKIA.” Ee BWANA, uiponye nafsi yangu kutokana na Ponografia. Ponografia ni uongo! 

Kunalo tumaini la ukombozi kutokana na ponografia ndani ya BWANA na NENO la MUNGU. Tuko katika nyakati za mwisho na shetani anajua kwamba muda wake ni mfupi.1 Ana hasira nyingi na ndiyo sababu anazidi kutupa mishale kwa wateule na wale ambao wangependa kuwa wateule, wale ambao wangependa kuwa huru kutokana na “mishale ya mtu hodari iliyochongoka, pamoja na makaa ya mteremu” (Zaburi 120:4).

Sote tumeitwa na MUNGU kupigana na shetani. Lakini, vita ambavyo2 haviishi ukitaka afueni ya kila siku kutokana na mshale huu wa ponografia utokao kwa Ibilisi ambaye angependa uishi naye milele Kuzimu ukichomeka kwenye lava inayochemka ya salfa na kiberititi kule Jehanamu.3 Lakini, ni vipi waume na wake wa kizazi hiki wataweza kumshinda shetani na silaha hii yenye nguvu ya mawazo machafu ya uchi na usinzi, ambayo ni ponografia?

Katika Zaburi 119:9 (BETHI), Daudi anauliza swali hilo hilo: “Jinsi gani kijana [mwanamke] aisafishe njia yake? [Anatupa sisi sote njia ya pekee ambayo ni NENO la MUNGU.4 Na jibu lake ni:] Kwa kutii, akilifuata NENO LAKO. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, usiniache nipotee mbali na MAAGIZO YAKO. [Na hapa ndipo kuna siri kuu:] Moyoni mwangu, nimeliweka NENO LAKO, nisije NIKAKUTENDA DHAMBI. EE BWANA umehimidiwa, nifunze AMRI ZAKO. [Kariri maneno haya kila wiki. Zaburi sio hadithi tu, bali ni uwezo wa MUNGU wa kukusaidia wewe kumshinda shetani! Daudi aliyatenda haya na kama sio hivyo hangesema:] Kwa midomo yangu nimezisimulia hukumu zote za kinywa CHAKO. Nimeifurahia njia ya SHUHUDA ZAKO kana kwamba ni mali nyingi. [Kutoroka nguvu ovu za mawazo machafu ya ngono na mawazo yaliyobuniwa ya ngono ni kutenda alivyotenda mzaburi Daudi.] Nitayatafakari mausia YAKO, nami nitaziangalia njia ZAKO. Nitajifurahisha sana kwa amri zako SITALISAHAU NENO LAKO” (Zaburi 119:9-16).

Afueni kutoka kwa tamaa zoea za mwili, kutokana na mawazo machafu ya ngono, kutokana na uovu, hali ya kugandamiza ya ponografia na uhalifu wa kila aina ya ngono inahitaji mtu kuweka akili safi, ambayo inawezekana tu kwa kutafakari kila wakati juu ya NENO la MUNGU!5 Ukombozi kutoka kwa pombe, dawa za kulevya na dhambi zote hupatikana kwa njia hiyo hiyo; kwa NENO LA MUNGU!

Kuwa mwaminifu kwa mke au mume wako wakati yeye hayupo karibu na kuponya majeraha ya uzoefu wa uzinzi hupatikana TU kwa akili safi iliyooshwa na NENO la MUNGU; ambayo imejijaza uponyaji, tumaini na afueni kutoka kwa uzoefu wa ngono; ponografia.6 Unafaa kupambana na jambo hili kila siku. “Tukiangusha [kwa NENO la MUNGU] mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya MUNGU na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii KRISTO [kunyenyekea chini ya NENO la MUNGU]” (2 Wakorintho 10:5).

Zaburi 119:1-3 (ALEFI): “Heri walio kamili katika njia zao, waendao katika SHERIA ya BWANA. [Shetani ambaye huleta mawazo ya picha mbaya za uchi ndiye shetani akuambiaye kuwa sheria na maadili ya MUNGU imemalizika!7 Huu ni UONGO, kama vile ni uongo wa Shetani wakati anakuambia ya kwamba unapata faida fulani kutokana na ponografia. YESU alisema, ‘Msidhani ya kuwa nimekuja kutangua SHERIA, au manabii: La, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka Mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, mpaka yote yatimie’ (Mathayo 5:17-18). Shetani hapendi wewe uamini katika nguvu za ukombozi katika NENO la MUNGU, lakini jaribu jambo hili na utaona kwamba NI KWELI!] Heri wenye kuweka shuhuda ZAKE na WAMFUATAO kwa moyo wote. Wao pia hawatendi uovu bali wanatembea katika njia ZAKE.”

Shetani ataweza, ikiwa utamruhusu, kuleta kumbukumbu ya zamani ya ngono akilini mwako. Wakati huo  ndio unaofaa kupambana naye papo hapo kwa NENO la MUNGU. Tafuta Biblia yako KJV, [toleo la Kiswahili la The Bible League, waenezaji wa Neno la Mungu tangu mwaka wa 1938] na uanze kusoma ZABURI hapo hapo. Usisubiri. Shetani anatafuta nafsi yako. Katika vita, ikiwa unatupiwa risasi,  lazima urushe yako pia. Shetani anakutupia risasi, nawe unastahili kumtupia yako pia ukitumia NENO la MUNGU.8 “(Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo [KIROHO] kwa njia ya MUNGU hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya MUNGU na tukiteka nyara kila mawazo ya utii wa KRISTO” (2 Wakorintho 10:4-5).

Shetani yule yule ambaye anakutupia mishale ya moto ya ponografia anakwambia kwamba NENO la MUNGU halifanyi kazi na kwamba SHERIA ya MUNGU, SHERIA ya maadili, si lazima izingatiwe kwa sababu haina ukweli wowote tena. Huyu ndiye shetani yule yule ambaye anakusingizia wewe, kukushutumu kwa njia ya uongo, na pia, kumsingizia MUNGU. Tunafaa kukumbuka kwamba yeye ni mwongo na baba wa waongo wote na ni lazima kupigana naye (Yohana 8:44).

BIBLIA ya KJV inasema kwamba sisi tu katika vita. Hii ina maana kuwa sisi lazima kupambana kwa njia ya halali, tukitumia NENO la MUNGU.9 Shetani anaiambia dunia nzima kwamba MUNGU tayari ameshughulikia mambo yote, kumaanisha kwamba sisi hatutakiwi kufanya kitu chochote kamwe! Huu ni uongo. Sisi tutahukumiwa kwa MATENDO yetu.10 Soma kitabu cha Yakobo na hata Biblia nzima.

Je, sisi tunafaa kumheshimu MUNGU kivipi? Je, sisi tunadhibitisha UPENDO wetu KWAKE vipi? “MKINIPENDA, mtazishika amri ZANGU” (Yohana 14:15). “Yeye anayesema, namjua YEYE, na HAZITENDI amri ZAKE, ni mwongo, na UKWELI [KRISTO] HAUMO ndani yake” (1 Yohana 2:4).

Ungama dhambi zako kwa MUNGU na kutubu kwa kusema sala hii:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Haki ya Kunakili Oktoba 2011, 2015 Haki zote zimehifadhiwa Mchungaji wa Ulimwengu Tony Alamo® Tarehe ya Usajili Oktoba 2011, 2015
SWAHILI—VOLUME 13600—VICTORY OVER PORNOGRAPHY!


footnotes:

1. Ufu. 12:9-12, 20:10 return

2. Eze. 33:12-13, 18, Lk. 9:23, 62, Mdo. 14:22, Rum. 11:22, Efe. 6:10-18, 1 Thes. 5:22, 2 Thes. 2:13-15, 1 Tim. 4:16, 6:12, Ebr. 3:12-14, 1 Pet. 1:13-17, 2 Yoh. 8 return

3. Isa. 30:33, Mat. 13:24-30, 37-43, 47-50, Mk. 9:43-48, Lk. 3:17, 16:19-31, Ebr. 10:26-31, Ufu. 14:9-11, 19:20, 20:10-15, 21:8 return

4. Mit. 6:22-23, Mat. 4:3-11, 8:16, Yoh. 8:31-32, 14:6, 17:17, 2 Tim. 3:14-17, Ebr. 4:12, Yak. 1:21-22 return

5. Yos. 1:8, Zab. 1:1-3, 19:7-11, 63:5-6, 119:48, 55, 97, 148, 143:5, Mit. 3:1, 6:20-23, 23:12, Mat. 4:4, Lk. 11:28, Yoh. 8:31-36, 15:3-7, 17:17, Mdo. 20:32, Efe. 5:25-27, Kol. 3:16, 2 Tim. 2:15, Yak. 1:21-22, 1 Yoh. 2:14 return

6. Isa. 26:3-4, Mat. 5:6, Yoh. 6:63, 14:23-24, 15:3, Kol. 3:1-2, 16 return

7. Zab. 111:7-8, 119:89, 152, 160, 138:2, Mhu. 3:14, Isa. 24:5, 40:8, Yer. 31:31-33, Mat. 5:17-48, Mk. 13:31, Lk. 10:25-26, Rum. 3:31, Ebr. 10:16, 13:8, Ufu. 22:18-19 return

8. 2 Kor. 10:3-6, Efe. 6:10-18, 1 Tim. 6:12, Yak. 4:7, 1 Pet. 5:8-9 return

9. Mat. 26:52, 2 Kor. 10:3-6, Efe. 6:10-18, Flp. 1:27-30, 1 Tim. 6:12, 2 Tim. 2:3-5, Ebr. 4:12, 1 Yoh. 2:13-17, 4:3-4, 5:4 return

10. Mwa. 17:1, 26:4-5, Kut. 15:26, Law. 22:31, Hes. 15:40, Kum. 4:2, 40, Ayu. 34:11, Isa. 56:1-2, Eze. 3:17-21, 33:1-9, Mat. 25:31-46, 1 Kor. 3:9-17, Gal. 6:7-9, 2 Tim. 4:5-8, Tit. 2:11-14, Yak. 2:12-26, 1 Pet. 1:17, Ufu. 3:2, 15-19, 20:12-13 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return