KUJIUA NI DHAMBI

na Tony Alamo

Msichana mmoja alimwomba mama yake amruhusu kuishi kwenye kanisa letu kwa sababu alimpenda Bwana sana na pia alilipenda kanisa letu. Alikuwa na umri wa miaka 13. Kaka yake alikuwa akiishi kanisani yapata miaka minane kufikia wakati huo. Msichana huyu alipenda kumtembelea Kaka yake kipindi cha majira ya joto. Kaka yake alikuwa akiitwa Ed Mick. Kabla ya Sue na mimi kumleta kwa Bwana, Ed alikuwa ni mmoja wa wauzaji mashuhuri wa madawa ya kulevya katika Hollywood, California.

Siku moja Ed alipokea simu kutoka hospitalini. Inasemekana mama yake alimfanya baba yake (Ed) kuwa mwenda wazimu, jambo ambalo lilimfanya baba yake kujipiga risasi kichwani. Alikuwa amejiua. Yule muuguzi aliyempigia Ed simu alisema, “baba yako amekwisha.”

Mamake Ed alikataa kumruhusu bintiye kuishi kanisani, hivyo basi, hata baada ya sisi kumuonya kuhusu kujiua, alijipiga risasi kichwani. Alijiua kwa sababu alikuwa na huzuni nyingi wakati alipokuwa akiishi na mamake kule Blytheville, Arkansas. Msichana huyu hakufa papo hapo. Alipelekwa hospitalini Memphis na kwa hiyo mimi na Sue tukapanga jinsi ambavyo Ed Mick angeweza kwenda huko kumuona kabla hajafa. Niliambatana na Sue kutoka Nashville mpaka hospitalini. Hospitali haikuturuhusu kuingia chumbani mwake kwani hatukuwa ndugu zake. Ed peke yake ndiye aliyekubaliwa kuingia mle ndani. Ed alituambia kuwa alipoingia chumbani, machozi yalikuwa yakimtiririka usoni dada yake. Ghafla, akaketi chini, akiwa na tabasamu usoni mwake na mikono yake ikiwa imeinuliwa juu. Kisha akaanguka nyuma tena kitandani akafa.

Msichana huyu alijiua kwa sababu mama yake alimkataza kumtumikia Bwana. Kwa tukio kama hilo, ilikuwa wazi kwamba Bwana alimhurumia msichana huyu na kumkubalia kuingia mbinguni. Kama sio hivyo, hangelikuwa na tabasamu usoni mwake wakati Bwana alipokuja kumchukua. Hata hivyo, jambo kama hili halitendeki katika matukio mengi ya kujiua. Ni wazi msichana huyu alitubu na ndio sababu uso wake ulijaa machozi. Ndugu yake alianza kuongea naye lakini bwana akamwangalia kwa ukali, MUNGU alikuwa akimwambia binti huyu kuhusu jambo hilo baya alilokuwa amelitenda. Alikuwa muuaji – muuaji ambaye amejiua. Miili yetu si mali yetu wenyewe. Yesu alitununua kwa damu yake!1 Wakati Yesu anapokimiliki kitu, kinakuwa chake, na huna ruhusa ya kukichukua au kukiua.

Baada ya miaka michache ndugu Ed alijiua pia. Kulikuwa na pepo la kujiua ambalo lilitawala familia ile. Walimlaumu mama yao, lakini mtu yeyote anayejiua atasimama hukumuni kwa yote aliyotenda.2

Waebrania 9:26-28 inasema hivi, “kama ni hivyo, ingalimpasa [YESU] kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu, kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.”

Babake Ed Mick alikuwa afisa wa Polisi kule Blytheville, Arkansas, ambako ni mwendo wa saa chache kutoka Nashville, Tennessee. Tukio lake pamoja na mwanawe Ed Mick lilikuwa tofauti na binti yake. Ed alimwacha Bwana akawa mwizi na mzinifu. Kuna uwezekano kwamba alijiua kwa sababu ya kukata tamaa. Inawezekana pia babake alijiua kutokana na kukata tamaa kwa sababu ya mkewe.

Mnamo mwaka 1964, Bwana aliniita katika huduma hii kuuambia ulimwengu kwamba Yesu yuarudi duniani mara ya pili hivi karibuni. Mwaka wa 1964, nilijua ya kwamba mambo si mazuri, lakini sikuwa nimewahi kusikia mtu akihubiri na kusema kwamba Yesu anarudi duniani tena.

Baada ya tukio langu lisilo la kawaida, la kiungu, MUNGU kwa nguvu zake aliniunganisha na Sue. Pamoja tumehubiri jambo hili (kwamba Yesu anarudi tena duniani) mpaka imefika kiwango ambacho sasa, kila mtu anaamini kuwa Bwana Yesu anarudi duniani tena. Hizi ni nyakati za mwisho, na ulimwengu mzima unaonekana kutambua jambo hili! Dunia nzima imejawa na kukata tamaa kwa sababu tunaishi nyakati ambazo Yesu alisema ni za “mwanzo wa utungu” (Mathayo 24:8). Wakati huu tuna muda mfupi kabla ya kutokea kwa dhiki kuu iliyotajwa katika kitabu cha Mathayo 24 na katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana.

Watu wengi siku hizi wanajitoa uhai. Huu umekuwa kama ugonjwa. Watu wanaamini kuwa wanapitia nyakati ngumu, na wengi wetu tunapitia wakati mgumu mno. Wengi wanaamini kwamba hakuna maisha ya siku za usoni hapa duniani kwa sababu dunia imehukumiwa na itateketezwa.3

2 Petro 3:10-12 inasema hivi, “lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya MUNGU, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?”

Kuna mabilioni ya watu ulimwenguni ambao wanateseka na kugandamizwa na viumbe vya asili vya kishetani na giza. Watu hao wanaishi maisha ya kukata tamaa. Wanaomba wafe na kutoka kwenye ulimwengu huu. Wengi wao hujiua na kuna uwezekano kwamba wengine wengi wanafikiria kujiua, lakini NENO la MUNGU, KRISTO, linatuambia ya kwamba ALIKUFA na kumwaga damu yake kwa ajili yetu.4 DAMU yake ndio bei ALIYOTUMIA kutununua. Je, unayadharau mambo haya yafanywayo na mabilioni ya watu? Hebu fikiria, ikiwa kuzimu si kubaya jinsi wengi wanavyosema, kwa nini MUNGU alikuja duniani kama mwanadamu, akaishi maisha matakatifu bila dhambi, na kufa kifo kikatili kushinda vyote duniani kwa ajili yetu, ili tunapomwamini, tusiende kuzimu?5 Kristo alikwenda kuzimu kwa ajili yetu.6

MUNGU hakuniambia tu ya kwamba YESU atakuja duniani tena. Ujumbe huu uliambatana na ndoto na maono ya Mbinguni na Kuzimu. Watu husema, “unajuaje kuna Kuzimu na ilhali hakuna mtu aliyewahi kuiona?” Mimi nimewahi. Wengine wanauliza, “tutajuaje kwamba kuna mbingu na ilhali hakuna mtu aliyewahi kuiona?” Nimewahi na nina uhakika ya kwamba kuna watu wengi wanaoishi sasa ambao wameiona pia. Mbinguni ni mahali pa kupendeza,7 na Kuzimu ni mahali pa kutisha zaidi ya vile yeyote angeweza kudhania au kusema.8 Hakuna maneno yanayotosha kuelezea uzuri na mvuto wa Mbinguni na jinsi Kuzimu kunavyotisha (1 Wakorintho 2:9). Hii ndio sababu MUNGU anatuambia katika kitabu cha 2 Timotheo 2:3-4, “Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Yesu Kristo. Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.”

Mambo ni mabaya na yanazidi kuwa mabaya duniani, lakini ukilinganisha na Kuzimu, hii ni kama matembezi katika mapumziko ya Jumapili. Jambo la kipumbavu ambalo unaweza kulitenda ni kujiua. Wengi wetu tunateseka kwa sababu ya msimamo wetu kwa Bwana, kwa sababu ya NENO LA MUNGU, lakini mabilioni ya watu wengine wanapitia ugumu kwa sababu wako upande wa chuki, dini za uongo, au kwa sababu ya tamaa za mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima (1 Yohana 2:16). MUNGU hataturuhusu kuwa na mafundisho yetu binafsi na kutenda yaliyo mapenzi yetu wenyewe bila kuwajibika.9

Waebrania 12:5-7 na 9 inasema hivi, “Tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, wala usizimie moyo ukikemewa naye; maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; MUNGU awapenda kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? ….Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya BABA wa roho zetu na kuishi?”

Waebrania 12:13-15 inasema hivi, “Mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe. Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, hofu, na utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao. Mkiangalia sana mtu asiipungukie neema [nguvu] ya MUNGU; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengine wakatiwa unajisi kwa hilo.”

Watu wengi wamenajisika na kujawa na uchungu. Hii ni kwa sababu MUNGU amemruhusu shetani kuwatesa watu wasiomcha MUNGU akiwa na matumaini kwamba jambo hili litawafanya watubu.10 Kumbuka, MUNGU anaruhusu haya kwa sababu YEYE anatupenda na anapenda tufanye toba, kutoka kwenye uasi wetu na kumsujudia yeye ili tuweze kuingia mbinguni na si Kuzimu.11

Kuna njia mbili wanazopitia watu. Njia ya kwanza ni kumkasirikia MUNGU, kuonyesha uchungu mbele zake na kumshambulia, na njia ya pili ni kutubu, na kumwomba MUNGU atusamehe na atukomboe kutoka kwenye mateso ambayo amemruhusu shetani kutupa.

Ufunuo wa Yohana 9:3-6 inasema hivi, “nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi. Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu chochote kilicho kibichi, wala mti wowote, ila wale watu wasio na muhuri ya MUNGU katika vipaji vya nyuso zao. Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao ilikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu. Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia.” Mstari wa 10 unasema hivi, “Nao [nzige] wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.”  
Ilikuwa kama mateso kwangu nikiwa mtoto wakati nilipopokea kichapo cha fimbo. Ilikuwa mateso wakati huo, lakini ikiwa wazazi wako wakikristo wanakupenda, lazima watakuchapa wakati wowote itakapobidi uchapwe kwa sababu hawataki uende Kuzimu.12

Kitabu cha Ufunuo wa Yohana 9:6 kinazungumzia kuhusu wale ambao wanaomba kufa kwa sababu ya mateso makali lakini hawawezi kufa. Hebu fikiria majuto yatakayokuwa Kuzimu wakati nyoyo za watu zitakapotamani kuzimia au kufa, ingawaje watakuwa wakijua ukweli kwamba haitawezekana wao kuzimia au kufa. Mateso wakati huo hayatakuwa mara bilioni bali mara trilioni mbaya kuliko mateso yote ya dunia kama yangewekwa pamoja.

Sasa, tufanyeje juu ya haya? Hakika hatuwezi tu kulalamika. Hesabu baraka zako wakati ungali hai, wakati una uwezo wa kutubu na si kuzimu. Hesabu Baraka zako zilizo nyingi mno. Zihesabu moja moja, na kwa furaha utashangaa yale BWANA aliyokutendea.13

Ikiwa unataka kuzaliwa mara ya pili katika ROHO, sali sala hii, kisha pata muda wa kusoma NENO la MUNGU (Biblia Takatifu), na umtumikie MUNGU kwa moyo, roho, akili na nguvu zako zote.

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Hatimiliki Oktoba 2012 Haki zote zimehifadhiwa World Pastor Tony Alamo  ® Imesajiliwa Oktoba 2012
SWAHILI—Vol. 16600—Suicide Is Sin


footnotes:

1. Isa. 53:10-12, Mdo 20:28, 1 Kor. 3:16-17, 6:19-20, 7:23, Ebr. 9:12, 13:12, 1 Pet. 1:18-19, Ufu. 5:9-10 return

2. Kut. 20:13, Mit. 24:12, Eze. 18:4, Dan. 7:9-10, Mat. 16:27, 19:16-18, Mdo 10:42, 17:31, Rum. 2:4-16, 14:10-12, 2 Kor. 5:10, Gal. 6:7, Ebr. 10:30-31, Yud. 14-15, Ufu. 2:23, 11:18, 20:12-13 return

3. Isa. 24:17-23, Sef. 1:14-18, 3:8, Mal. 4:1, Mathayo sura ya. 24, 2 Pet. 3:7, 10-12 return

4. Zab. 22:12-18, Isa. 53:3-12, Mdo. 5:30-32, 13:38-39, Rum. 5:6-11, 1 Kor. 15:3-8, Efe. 1:3-12, Kol. 1:12-14, 1 The. 5:9-10, Ebr. 2:9-10, 9:11-15, 1 Pet. 1:18-21, 2:21-25, 1 Yoh. 2:2, Ufu. 1:5 return

5. Yoh. 3:14-18, Rum. 3:21-26, 2 Kor. 5:17-21, Ebr. 4:14-15 return

6. Efe. 4:7-10, 1 Pet. 3:18-20 return

7. Zab. 31:19, Isa. 64:4, 65:17-19, Mat. 5:10-12, Yoh. 14:2-4, Rum. 8:16-23, 1 Kor. 2:9, 2 Kor. 5:1, 1 Pet. 1:3-5, 2 Pet. 3:13-14, Ufu. 7:15-17, 21:1-5, 9-27, 22:1-5 return

8. Kum. 32:21-22, Zab. 9:17, Mit. 9:13-18, 15:11, 24, 23:13-14, Isa. 5:11-15, 14:4-20, 28:15-18, 33:10-14, Eze. 31:15-18, 32:17-32, Mat. 5:21-22, 29-30, 7:13, 8:12, 10:28, 13:36-42, 47-50, 18:6-9, 22:8-13, 23:33, 24:44-51, 25:14-46, Lk. 3:17, 13:24-28, 16:19-28, 2 The. 1:6-9, Ebr. 6:4-8, 2 Pet. 2:1-9, Yud 5-7, 12-13, Ufu. 14:9-11, 19:20, 20:10-15, 21:8 return

9. Zab. 34:15-16, Mat. 7:13-19, 2 Pet. 2:1-6, 9-22, Yud. 3-7, 14-15, Ufu. 20:11-15 return

10. Law. 26:13-46, Kum. 8:2-5, Zab. 94:12-13, Hos. 5:15, Rum. 2:4-11, 1 Kor. 11:32, 2 Kor. 7:9-11 return

11. 2 Sam. 7:14-15, Mit. 13:24, 19:18, 22:6, 15, 23:13-14, 29:15, 17, Ebr. 12:5-11, Ufu. 3:19 return

12. 2 Sam. 7:14-15, Mit. 13:24, 19:18, 22:6, 15, 23:13-24, 29:15, 17, Ebr. 12:5-11, Ufu. 3:19 return

13. Zab. 68:19, 103:2-18, Efe. 1:3-12, Kol. 3:15 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return