MAGARI YA MOTO

na Tony Alamo

Watu wanapoona neno “gari,” wanadhani lina maana moja tu, “gari linalokokotwa na farasi, lenye magurudumu mawili lililotumika nyakati za kale kwa ajili ya vita, mashindano, n.k.”  Kamusi ya Webster pia linasema “tazama motokaa.” Tunapotazama “gari,” tunaona neno hili linatokana na neno la Kilatini “carrus,” ambalo lina maana ya “gari la kuvutwa na farasi.” Gari pia linamaanisha “(1) gari lolote lenye magurudumu; (2) gari linalokwenda juu ya reli, kama gari la kubeba watu mitaani linalovutwa na farasi (wakati mwingi linatumiwa na maharusi); (3) motakaa; na (4) kizimba cha lifti.” Ufafanuzi wa kisasa ni pamoja na ndege, UFO, visahani vinavyopaa, na chombo chochote cha uchukuzi wa watu, malaika, nk. Tafsiri ya Kiebrania ya “gari” inaweza kuwa “umati wa watu” au magari yanayovutwa na farasi. Hivyo basi neno “gari” lina maana nyingi.

Katika 2 Wafalme 6:15, Hata asubuhi na mapema mtumishi (au mjakazi) wake yule mtu wa MUNGU (Elisha) alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule (haya hayakuwa magari ya moto, kwa sababu yalikuwa yamebeba watu tu). Mtumishi (mjakazi) wake akamuuliza, “Ole wetu! Bwana wangu, tutafanyaje?” Akamjibu, “Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.” Elisha akaomba akasema, “Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona.” BWANA akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote. Magari haya ni tofauti kuliko yale ya Washamu kwa sababu magari haya yamebeba malaika. Ni “magari ya moto,” na yasiyoonekana kwa macho ya kibinadamu MUNGU asipotuwezesha kuyaona. Anaruhusu watu zaidi na zaidi kuona visahani vya Mbinguni vipaavyo angani leo. Vinaikagua dunia kabla YESU hajarudi duniani tena, na vinatenda kulingana na agizo la MUNGU, kwa kusababisha maafa hapa na pale duniani kwa sababu ya makufuru ya wanadamu, ibada ya sanamu, na aina nyingine za maovu.1

Baadhi ya watu wanaamini kwamba tunachopaswa kufanya ni kuamini maneno “YESU KRISTO” nasi tutaokolewa. Katika uhalisia, anachomaanisha MUNGU ni kwamba tunapaswa kuamini kila kitu alichosema BWANA wetu YESU, alichofanya, na kile anachofanya kupitia MWILI WAKE, ambao ni Kanisa LAKE, Bibi arusi WAKE. Hii ndiyo sababu anatueleza katika kitabu cha Ufunuo kwamba ni lazima tuwe na bidii tukijishughulisha kumfuata YEYE.2

Watu wengi hutangaza kwamba wanaamini jina LAKE, Shetani naye anaamini pia jina LAKE, na kutetemeka (Yakobo 2:19). Hata hivyo, YESU anatuambia anahitaji tumfuate YEYE na kushika amri ZAKE zote, kwa bidii!3 Kama tukivunja hata moja ya amri ZAKE, tutakuwa tumevunja zote, kwa sababu kama tukivunja hata moja ya amri ZAKE, yatosha kupeleka roho zetu kwenye Jehannamu ya milele na Ziwa la Moto milele.4 Hii ndio sababu YESU anatuonya kwamba YEYE hafanyi utani. Anasema, “Nayajua matendo yako [Anajua kila jambo tunalosema na tunalotenda], ya kuwa hu baridi wala hu moto. Basi kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa CHANGU” (Ufunuo 3:15-16).

Jinsi gani ambavyo BWANA anajua kila jambo tunalosema na kutenda? Tunajua kwamba kila kitu tulichosema na tulichofanya, au tutakachosema na tutakachotenda, kimeandikwa kitabuni.5 Tunajua kwamba MUNGU yupo kila mahali, namna ambavyo ulimwengu haumtoshi.6 Pia YEYE ni Mwenyezi, jambo linalomaanisha kuwa ana nguvu na mamlaka yasiyo na kikomo. YEYE ni mwenye nguvu-zote.7 YEYE yupo kila mahali, ikimaanisha kuwa anapatikana kila mahali kwa wakati mmoja.8 Si kitu kwa MUNGU kujua kila jambo tunalosema na kufanya, na ni jambo lisilowezekana kwake kudanganya (Waebrania 6:18 ).

Ni muhimu mno kumwamini YESU pale anaposema tutahukumiwa kwa kila neno lisilo na maana.9 Mathayo 12:36 inasema, “Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.” Ufunuo 20:11-12 inasema, “Kisha nikaona kiti cha enzi kikubwa, cheupe, na yule aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake; na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi cha MUNGU; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.”

Nimeandika katika kipande kingine cha maandiko kuwa MUNGU hutuma malaika ZAKE kuwaangamiza wenye dhambi na sehemu za maovu duniani.10 Kitabu cha Ufunuo kinaelezea seti ya mapigo saba ya kwanza na ya pili ambayo malaika watayamimina kuangamiza dunia nzima inayofanya sana dhambi (Ufunuo 8:6 kupitia 9:21, 11:14-19, 16:1-21).

Malaika mmoja pia aliangamiza jeshi la Senakeribu, watu 185,000, kwa usiku mmoja tu. “Ikawa usiku uo huo malaika wa BWANA alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga [kuua] watu mia na themanini na tano elfu [185,000]. Na watu walipoondoka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia” (2 Wafalme 19:35).11 Wakati Daudi alipofanya dhambi kwa kuwahesabu Israeli, kinyume na alivyotaka MUNGU, MUNGU alituma malaika mmoja kutoa mapigo juu ya wana wa Israeli, ambayo yaliua 70,000 ya watu hao (2 Samweli 24:15).

MUNGU, kuwa kila mahali kwa wakati uo huo, anatuma malaika ZAKE, ambao ni wafanya kazi wake, kulaani watu duniani, kuleta uharibifu kwa waovu. Malaika pia ni wajumbe ambao wametumwa kuleta habari ya furaha kwa watu kama Maria na Elizabeth.12

Sasa, kuna moto kutoka kwa MUNGU uchomao kama ndimi za moto ambao Mtume Petro anauzungumzia katika 2 Petro 3: 7-14: “Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa NENO lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha MUNGU. Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa BWANA siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. [Kwa lugha rahisi inamaanisha kwamba si lazima MUNGU awe na haraka kukuhukumu wewe na mimi kwa sababu maisha yetu ni mafupi sana.13 MUNGU ni wa milele; ANAISHI milele.14 ANAJUA kwamba wewe na mimi tutasimama mbele ZAKE katika mpepeso mmoja au miwili ya macho.15 ANA muda mwingi. Muda utakapokwisha, ATAKUONA wewe na mimi – hivi karibuni sana]. BWANA hakawii kutimiza ahadi YAKE [hukumu YAKE], kama wengine wanavyodhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana HAPENDI mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba [kabla mipepeso miwili ya hukumu yetu kuwa imekwisha].

“Lakini siku ya BWANA itakuja kama mwivi; ambayo katika hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya MUNGU, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani YAKE. Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele YAKE.”

Kuna moto wa Mungu ambao hauchomi kama moto ulioelezwa hapo juu, ambao huchoma mbingu na nchi yote. Hapa ni baadhi ya mifano ya aina hii ya moto. Ufunuo 1:13-14 inasema kwamba kulikuwa na mtu mmoja katikati ya vinara saba vya taa, ishara ya makanisa saba, “mfano wa MWANANADAMU [YESU], amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini. Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji [ishara ya yeye kuwa MWANA KONDOO wa MUNGU, aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu kwa ajili ya dhambi ya wale wote ambao watatubu16]; na macho YAKE kama MWALI WA MOTO...’’

“Malaika wa BWANA akamtokea [Musa], katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea” (Kutoka 3:2).
“BWANA naye akawatangulia [taifa la Israeli] mchana ndani ya wingu mfano wa nguzo, ili awaongoze njia; na usiku ndani ya moto mfano wa nguzo ili kuwapa nuru; wapate kusafiri mchana na usiku” (Kutoka 13:21).

“Na kuonekana kwake ule utukufu wa BWANA kulikuwa kama moto uteketezao, juu ya mlima machoni pa wana wa Israeli” (Kutoka 24:17).

Katika Mathayo 3:11, Yohana mbatizaji anasema, “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali YEYE [YESU] ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; YEYE atawabatiza kwa ROHO MTAKATIFU, na kwa MOTO.”

“Ikawa alipokuwa [YESU] ameketi nao chakulani, ALITWAA mkate, AKAUBARIKI , AKAUMEGA , AKAWAPA. Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko?” (Luka 24:30-32).

Katika 2 Wafalme 6:17, Elisha alimwomba MUNGU kufungua macho ya mtumishi wake, mjakazi wake, “mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari [magari yanayovutwa na farasi, UFO, visahani vipaavyo] ya MOTO [sawa na ROHO MTAKATIFU, MOTO ambao YESU hutubatizia tunapojazwa na nguvu kutoka juu, tukibatizwa kwa ROHO MTAKATIFU na MOTO] yaliyomzunguka Elisha pande zote.”

Katika Matendo 1:7-9, YESU aliwaambia wanafunzi WAKE, “Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, BABA aliyoyaweka katika mamlaka YAKE mwenyewe. Lakini mtapokea nguvu [MOTO na ARI], akiisha kuwajilia huyo ROHO MTAKATIFU; nanyi mtakuwa mashahidi WANGU katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.”

ROHO MTAKATIFU alimchukua YESU Mbinguni. Ni ROHO MTAKATIFU anayeziendesha UFO, visahani vipaavyo au magari ya MOTO yakiwa na malaika ndani yake. Havitoki kwenye sayari yoyote ile. Ni za kimbingu - toka Mbinguni - kuchunguza dunia kabla ya ule mwisho wa wakati, kabla YESU hajarudi tena duniani. Pia wanatekeleza mwanzo wa uchungu ambao YESU ameuzungumzia katika kitabu cha Mathayo sura ya 24. Haya ni maneno ya YESU: “Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni KRISTO; nao watadanganya wengi. Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na tauni [tauni ni magonjwa ya mlipuko au kitu chochote kinachodhaniwa kuwa kibaya] na matetemeko ya nchi mahali mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu” (Mathayo 24:4-8).

Je, unafikiri kwamba tumekwenda zaidi ya mwanzo wa utungu? Mstari wa 9 unasema, “Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki [na MUNGU na malaika wanaangalia!], Nao watawaua [kama walivyowaua wanaume, wanawake na watoto katika mauaji-ya-Waco (Wakristo asili waliouawa kinyama kule Texas) na MUNGU na malaika zake wakiangalia. Janet Reno na Bill Clinton walisema kwenye runinga ya kitaifa kwamba wote wanachukua wajibu kamili kwa ajili ya jambo hilo. Bill Clinton alisema, ‘Hili linapaswa kuwafundisha watu kutojiunga na dini za kishetani.’ Hii ilikuwa kinyume cha sheria sana, tendo la kinyume na katiba, dhidi ya Marekebisho ya kwanza ambayo Bill Clinton alifanya na akasema kuwa alifanya]. Nanyi [Wakristo wa kweli] mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu [kwa sababu unampenda YESU. YESU na walinzi wanaangalia kila kinachotokea hapa]. Ndipo wengi watakapojikwaa [kwa sababu ya mateso yajayo kwa kuwa Mkristo wa kweli (si Katoliki)], nao watasalitiana [kama walivyofanya], na kuchukiana [kama wanavyofanya]. Na manabii wengi wa uongo [kutoka kwa Shetani] watatokea, na kudanganya wengi. [Ufunuo 12:9 inasema, ‘Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa (kutoka mbinguni) hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.’] Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. [MUNGU na magari ya MOTO wanaangalia na kusikiliza kila jambo.] Tena habari njema [kweli yote] ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho [wa dunia] utakapokuja. Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu)” (Mathayo 24:9-15).

Chukizo la uharibifu ambalo huifanya dunia nzima ukiwa ni hatua ya Papa katika Roma, Vatican, kukusanya wakuu wa mataifa pamoja kuunda Serikali Moja ya Dunia, Mpango Mpya wa Dunia (New World Order) ambayo ni mnyama. Hii ni kwa roho ya Shetani.

Hii hapa ni makala ya tarehe 10 Desemba 2012, kuhusu vyombo vya habari kutoka Vatican: “Vatican inataka Serikali ya Dunia na Mpango Mpya wa Dunia,” iliyoandikwa na Andrew Puhanic, mchangiaji wa gazeti la Activist Post. “Kiongozi wa Kanisa Katoliki [dhehebu], Papa Benedict XVI, ametoa wito wa kuanzishwa kwa Serikali ya Dunia na Mpango Mpya wa Dunia. Katika hotuba aliyoitoa katika Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na Amani Jumatatu, Desemba 3, 2012, Papa ameagiza ‘ujenzi wa jumuiya ya kimataifa, na mamlaka inayolingana,’ kutumikia manufaa ya familia ya binadamu.’ ”

Manufaa? Katika Ufunuo 16:1-2, MUNGU alisema kama tukijiunga na shirika hilo la kishenzi kama mnyama huyu, Serikali hii Moja ya Dunia, Mpango Mpya wa Dunia, kwamba tutakuwa tumefunga hatima yetu wenyewe: “Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya MUNGU juu ya nchi. Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama [ambayo tena ni alama ya Serikali Moja ya Dunia, Mpango Mpya wa Dunia], na wale wenye kuisujudia sanamu yake [ambayo ni dunia yote ya waliodanganywa, watu wasiookoka].” 

Ufunuo 19:20 inasema, “Yule mnyama [Serikali Moja ya Dunia, Mpango Mpya wa Dunia inayoongozwa na Rumi17] akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye [ambayo ni kanisa la kishetani la katoliki] yeye aliyezifanya hizo ishara [ishara za uongo, kama kutokea kwa Maria na sanamu za YESU zikitiririsha damu msalabani, na sanamu za Maria akitiririsha damu mikononi mwake] mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama [dunia nzima ya watu ambao Shetani aliwadanganya], nao walioisujudia sanamu yake [wale walioitumikia serikali yake, na wapo katika orodha yake ya malipo]; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo na kiberiti.”
Kile anachofanya papa huyu na kusema kwa haraka kinaiongoza dunia iliyodanganyika kupokea alama ya mnyama katika mkono wao na paji la uso.Wale wote wanaopokea alama hii ni sawa na wanaomkufuru  ROHO MTAKATIFU, na papa huyu hudanganya wengi kwa jina la amani na usalama.18 Ufunuo 13:16-17 inasema, “Naye [Shetani ndani ya papa, kanisa lake la uongo, na Mpango Mpya wa Dunia na Serikali yake Moja ya Dunia] awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa masikini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Katika matoleo yake ya kwenye vyombo vya habari, Papa Anaongeza kuwa hii ni, “njia ya kutetea amani ya kimataifa na haki [‘Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo’ (Yohana 8:44).]. Maono ya Papa ya kuanzishwa kwa serikali ya Dunia na Mpango Mpya wa Dunia inasemekana kwamba si ya kutengeneza taifa lingine lenye nguvu, bali chombo kipya cha uongozi [ambacho ni kwa ajili ya wenye hatia, ulimwengu usiookoka (lakini kuna ukombozi wa watakatifu)] ambacho hutoa kwa wale (wanasiasa wajanja) ambao wanawajibika kufanya maamuzi, vigezo kwa ajili ya hukumu, na miongozo. Papa alinukuliwa akisema “Chombo kilichopendekezwa (Serikali ya Dunia) hakitakuwa taifa kubwa, mikononi mwa wachache, ambacho kitatawala watu wote, kuwanyonya walio wadhaifu.’ [Hiki ndicho hasa wanachopanga kufanya na wanachofanya.] Papa pia alielezea maono yake kama ‘ya kimaadili [kifisadi] nguvu’ au mamlaka ya kimaadili [kama yeye ana maadili, kwa nini serikali hii isiruhusu Amri Kumi katika shule za umma au kwenye majengo ya serikali kama vile vyumba vya mahakama?] iliyo na ‘nguvu ya kushawishi kwa mujibu wa sababu, yaani, mamlaka ya kushiriki, inayozuiliwa na sheria katika mamlaka yake.’”19

MUNGU anatuambia tukae mbali kabisa na mashirika yote ya Shetani, kimsingi Serikali Moja ya Dunia ya Shetani, ambayo imepewa mamlaka kutoka kwa Shetani kupitia Mpango Mpya wa Dunia.20 Utamwamini MUNGU, au dini ya kishetani ya Katoliki ya Kirumi ya Vatican na Papa? Hakuna faida ya kumwamini Papa wa Shetani. Mwisho wa wale wanaomwamini  na kumfuata ni katika Ziwa la Moto milele.

Mwamini MUNGU ambaye anasema wazi kuwa hakuna maisha kwenye sayari nyingine yoyote ile. Pia amini kwamba UFO ni malaika kutoka Mbinguni, Walinzi, na umwamini MUNGU MWENYEZI, tena ambaye yupo kila mahali kwa wakati mmoja.

Kama chaguo lako ni MUNGU, basi Sali sala hii. Kisha ubatizwe, kwa kuzamishwa ndani ya maji, kwa jina la BABA, la MWANA, na la ROHO MTAKATIFU.21 Jifunze Biblia Takatifu Toleo la The Bible League, Waenezaji wa Neno La  Mungu Tangu 1938 na ufanye asemalo.22

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Hatimiliki Februari 2013, 2015 Haki zote zimehifadhiwa Mchungaji wa Dunia Tony Alamo ® Imesajiliwa Februari 2013, 2015
SWAHILI—VOLUME 17500—CHARIOTS OF FIRE


footnotes:

1. Mwa. 19:1-25, Hes. 22:1-35, 25:1-9, 2 Sam. 24:1-17, 2 Fal. 19:35, 1 Nya. 21:9-30, 2 Nya. 32:19-22, Ufu. 7:1-2, sura ya. 8, 9:1-5, 13-21, 14:8-11, 15-20, sura ya. 16, 18:1-2, 21, 19:17-21, 20:1-3, 21:9 return

2. Mat. 3:7-10, 7:13-23, Yoh 14:12, 15, 21-24, 15:1-14, Rum. 12:5-21, Gal. 5:14-26, Efe. 4:20-32, Tit. 2:11-15, Ebr. 2:1-3, Yak. 1:21-27, 1 Pet. 4:7-8, 2 Pet. 1:3-11, 1 Yoh. 2:3-11, 15-17, 3:4-12, Ufu. 3:14-22 return

3. Ufu. 3:14-22 return

4. Yak. 2:10-11 return

5. Kum. 31:21, 1 Fal. 8:39, 2 Fal. 19:27, 1 Nya. 28:9, Ayu. 31:4, 34:21-22, 25, Zab. 44:21, 69:5, 139:1-16, 23-24, Isa. 29:15-16, Eze. 11:5, Lk. 16:15, Mdo. 15:18, Ebr. 4:13, 1 Yoh. 3:20, Ufu. 20:12-13 return

6. 1 Fal. 8:27, 2 Nya. 2:6, Zab. 139:7-16, Mit. 15:3, 11, Yer. 23:23-24 return

7. Mwa. 17:1, 35:11-12, 1 Nya. 29:11-12, 2 Nya. 20:6, Ayu. 42:2, Zab. 104:1-32, Isa. 26:4, 40:12-18, 21-28, Mat. 19:26, 24:30, 28:18, Lk. 1:37, Yoh. 17:2, Mdo. 26:8, Efe. 1:19-22, Kol. 1:12-19, 2:10, Ebr. 1:1-12, Ufu. 4:11, 16:9, 19:6 return

8. Zab. 139:3-10, Yer. 23:23-24, Mdo. 7:48-49, 17:24 return

9. Zab. 19:14, Mat. 12:36-37 return

10. “Jeshi na Jeshi la Anga la Mungu (Walinzi),” “Malaika wa Mbinguni Wanajivinjari Juu ya Sayari Yetu,” Mwa. 19:1-25, Kut. 33:1-3, 2 Sam. sura ya. 24, 2 Fal. 6:8-17, 19:1-35, 2 Nya. 20:1-24, 32:1-22, Zab. 34:7, 35:4-6, Zek. 1:7-21, Mat. 13:36-43, 47-50, 16:27, Mdo. 12:21-23, Yud. 14-15, Ufu. 7:1-2, sura ya. 8, 9:1-5, 12-21, 14:8-11, 15-20, 15:1, sura ya. 16, 18:1-2, 21, 19:17-21, 20:1-3, 21:9 return

11. 2 Nya. 32:19-21, Isa. 37:36 return

12. Mwa. 16:6-15, 21:14-21, Amu. sura ya. 13, 1 Fal. 19:1-8, Dan. sura ya. 6, Mat. 1:18-25, 28:1-8, Lk. 1:5-20, 26-38, 2:7-16, Mdo. 1:9-11, 10:3-6, 12:1-11, 27:9-44 return

13. 1 Nya. 29:15, Ayu. 4:17-21, 7:6-10, 9:25-26, Zab. 22:29, 39:4-6, Isa. 2:22, 40:6-7, Yak. 1:10-11, 4:14, 1 Pet. 1:24 return

14. Kut. 15:18, Kum. 32:39-40, Ayu. 36:26, Zab. 9:7, 10:16, 29:10, 45:6, 90:1-4, 93:2, 102:12, 24-27, 146:10, Isa. 44:6, Omb. 5:19, Dan. 4:34, Lk. 1:33, Ebr. 1:10-12, 1 Tim. 1:17, 6:15-16, Ufu. 1:8, 17-18, 4:8-11 return

15. Zab. 73:18-19, Mhu. 12:13-14, Dan. 7:9-10, Mdo. 17:30-31, Rum. 2:5-13, 16, 14:10-12, 1 Kor. 15:52, 2 Kor. 5:10, Ebr. 10:26-31, Ufu. 11:18, 20:11-15 return

16. Isa. 53:4-12, Yoh. 1:29, 1 Pet. 1:18-19, Ufu. sura ya. 5, 6:16, 7:9-17, 12:11, 13:8, 14:1-4, 15:3, 17:14, 19:7-9, 21:9-27 return

17. Ufu. 17:1-9, 15-18, 18:1-10, 15-19, 24, 19:1-3 return

18. Yer. 6:13-14, 8:11, Eze. 13:9-10, Mat. 10:34, 1 The. 5:1-9 return

19. http://www.activistpost.com/2012/12/vatican-calls-for-world-government-and.html return

20. 2 Kor. 6:14-18, 2 The. 2:3-12, Ufu. 2:18-25, 14:8-11, 16:1-2, 10-11, sura ya. 17, 18:1-8, 19:1-3, 17-21, 20:4, 10 return

21. Mat. 28:19-20, Yoh. 3:5, Mdo. 2:38, 19:3-5 return

22. 2 Tim. 2:15, 3:14-17, Yak. 1:22-25, Ufu. 3:18 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return