AJABU KATIKA MBINGU JUU NA ISHARA KATIKA NCHI CHINI

na Tony Alamo

Mamilioni ya watu wametoa taarifa za kuonekana kwa UFOs, ambao pia wanaitwa visahani vinavyoruka. Hakuna haja yoyote kubisha uwepo wa UFO kwa sababu wapo.

Wanafunzi wa YESU walimuuliza YESU, “Twambie, mambo haya yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? YESU akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni KRISTO; nao watawadanganya wengi. Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita [kamusi ya Webster inasema kwamba vita, kwa upande mwingine, ni tauni, yaani ‘janga la ugonjwa wa kufisha, pigo; kitu chochote kinachotazamiwa kuleta madhara; kiwezacho kusababisha mauti; hatari kwa jamii (tishio la uharibifu wa vita)’]; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa na tauni [vita, magonjwa, ukame, vimbunga, mafuriko], na matetemeko ya nchi mahali mahali. Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu.”

“Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi [Wakristo waliozaliwa-mara-ya-pili-kwa-ROHO] mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana” (Mathayo 24:3-10).1 “Chuki,” katika kamusi ya Webster, inamaanisha “kuwa na chuki kuu au kuwa na nia mbaya, kutaka kuepuka [kama ilivyo, kumchukia MUNGU, kuchukia Biblia, kuchukia Wakristo].”

Mtume Petro anarudia maneno ya unabii wa Yoeli wa mwisho wa dunia, kwa sehemu, kwa kusema kutakuwa na “ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini” (Matendo 2:19). Je, unajua kwamba muundo wa mbingu umebadilika kwa kiasi kikubwa? Pia, je, umewahi kufahamu kwamba hao UFOs au visahani virukavyo angani ambavyo watu wamekuwa wakiviona ni malaika wanaofanya uchunguzi yakinifu duniani kabla ya kumwaga ghadhabu ya MUNGU juu ya nchi na kuiharibu? Daima MUNGU amekuwa akiwatuma malaika WAKE kumwaga ghadhabu YAKE kwa wenye dhambi duniani.2

Mwanzo 6:6-7 inasema “BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.”

YESU pia alisema katika Mathayo 24:37-39, “Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake MWANA wa Adamu. Kwa maana kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake MWANA wa Adamu.”

Kama MUNGU alighairi kuwa amemfanya mwanadamu katika siku za Nuhu, kiasi cha kuwapeleka malaika ZAKE kuangamiza kila kiumbe kilicho hai kwa gharika juu ya nchi isipokuwa Nuhu, mkewe, wanawe watatu, na wake zao, hudhani kwamba MUNGU angeweza kutumia malaika ZAKE kufanya vivyo hivyo leo kwa halaiki ya watu dunia nzima, wakati Aonapo watu wa dunia wakifanya uovu kuliko watu walioishi nyakati za Nuhu?

Hakuna malaika wa kike. Malaika wote wa MUNGU ni wa kiume. Wote walio marubani wa visahani virukavyo ni malaika wa kiume, wakifanya uchunguzi yakinifu wa maovu yanayofanyika duniani leo, na hapa na pale, kuwapa watu duniani sampuli ya uharibifu ambao punde utakuja kutokea katika dunia nzima.

Tangu mwanzo wa saa, MUNGU amekuwa akiwatumia malaika wema kuharibu kazi za Shetani kwa wanadamu duniani, kama vile katika Sodoma, na Gomora, na maeneo mengine mengi katika maandiko.3 Katika uharibifu wa pili na wa mwisho wa dunia ya sasa, MUNGU anatuambia katika Ufunuo kwamba watakuwa ni malaika ambao watakaomimina mapigo kumi na nne ya mwisho juu ya nchi hadi itakapokuwa imeharibiwa kabisa.4

Ufunuo 8:2 hadi 9:21 inasema, “Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za MUNGU, nao wakapewa baragumu saba. Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi. Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za MUNGU pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika. Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa na radi na sauti na umeme na tetemeko la nchi. Na wale malaika saba wenye baragumu saba wakajifanya tayari ili wazipige.

“Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya nchi; theluthi ya nchi ikateketea, na theluthi ya miti ikateketea, na majani mabichi yote yakateketea. Malaika wa pili akapiga baragumu, na kitu, mfano wa mlima mkubwa uwakao moto, kikatupwa katika bahari; theluthi ya bahari ikawa damu. Wakafa theluthi ya viumbe vilivyomo baharini, vyenye uhai; theluthi ya merikebu zikaharibiwa.

“Malaika wa tatu akapiga baragumu, nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, iliyokuwa ikiwaka kama taa, ikaanguka juu ya theluthi ya mito [na kabla ya hii, jeshi la MUNGU la anga, visahani virukavyo, vijulikanavyo kama UFOs, vilikuwa vikichunguza ufisadi ulio juu ya nchi, na vinafurahi kumwaga ghadhabu ya MUNGU juu ya wanadamu waovu, wenye maudhi], na juu ya chemchemi za maji. Na jina lake ile nyota yaitwa Pakanga; theluthi ya maji ikawa pakanga, na wanadamu wengi wakafa kwa maji hayo, kwa kuwa yalitiwa uchungu. Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, wala usiku vivyo hivyo.

“Kisha nikaona, nikasikia tai mmoja akiruka katikati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya nchi! Kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu za malaika watatu, walio tayari kupiga [Maandiko haya yanatuonyesha yale yote ambayo malaika — malaika wa uharibifu wa MUNGU — wanajua vizuri sana nini kitatokea siku zijazo. Ubaya ni kwamba watu walioko duniani, walio waovu, hawawezi kufahamu jambo hilo!].

“Malaika wa tano akaipiga baragumu, nikaona nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Akalifungua shimo la kuzimu; moshi ukapanda kutoka mle shimoni kama moshi wa tanuru kubwa; jua na anga vikatiwa giza kwa sababu ya ule moshi wa shimoni. Nzige wakatoka katika ule moshi, wakaenda juu ya nchi, wakapewa nguvu kama nguvu waliyo nayo nge wa nchi. Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya nchi, wala kitu chochote kilicho kibichi, wala mti wowote, ila wale watu wasio na muhuri wa MUNGU katika vipaji vya nyuso zao. [Je, si jambo la kushangaza watu wasemapo ghadhabu ya MUNGU ni kubwa zaidi kipindi cha Agano la Kale kuliko wakati wa Agano Jipya? Haionekani hivyo hapa, sivyo?] Wakapewa amri kwamba wasiwaue, bali wateswe miezi mitano. Na maumivu yao yalikuwa kama kuumwa na nge, aumapo mwanadamu. Na siku zile wanadamu watatafuta mauti, wala hawataiona kamwe. Nao watatamani kufa, nayo mauti itawakimbia. [Katika Agano la Kale, adhabu haikuwahi kutolewa katika dozi ngumu kiasi hiki. Hebu fikiria - huwezi kuipigia kura au kuipinga kwa sababu MUNGU ni DIKTETA, daima yupo ofisini, iwe watu wa dunia wanapenda ama la. Hakuna usahihi wa kisiasa na hakuna demokrasia — ila theokrasia (yaani utawala wa MUNGU mfumo wa utawala wa serikali ya makuhani tu)!] Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu. Nao walikuwa na nywele kama nywele za wanawake. Na meno yao yalikuwa kama meno ya simba. Nao walikuwa na dirii kifuani kama dirii za chuma. Na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari, ya farasi wengi waendao kasi vitani. Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao. Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.

“Ole wa kwanza umekwisha pita. Tazama, bado ziko ole mbili, zinakuja baadaye. Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za MUNGU, ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati. Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu. Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa elfu ishirini mara elfu kumi [milioni mia mbili]; nilisikia hesabu yao. Hivyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, kama za moto, na za samawi, na za kiberiti; na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vichwa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti. Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo [Iwapo kungekuwa na watu bilioni saba juu ya nchi wakati huu, kama waliopo leo, na theluthi ya wanadamu walikufa kwa mapigo haya, ingekuwa hesabu ambayo haiwezi kulinganishwa katika historia kadiri ya hesabu ya watu waliouawa kwa wakati mmoja. Hata hivyo, hatujui ni watu wangapi waliuawa katika gharika siku za Nuhu, ingawa twajua wote waliangamia wakafa kwa maji isipokuwa Nuhu na familia yake, watu nane.5], kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao. Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwa hivyo. Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda. Wala hawakutubia uuaji [utoaji mimba] wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.”

Ufunuo 11:14-19: “Ole wa pili umekwisha pita, tazama ole wa tatu unakuja upesi. Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa Ufalme wa BWANA wetu, na wa KRISTO WAKE; NAYE atamiliki milele na milele. Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za MUNGU katika viti vya enzi vyao wakaanguka kifulifuli, wakamsujudia MUNGU, wakisema, tunakushukuru WEWE, BWANA MUNGU MWENYEZI, uliyeko, na uliyekuwako, kwa sababu Umeutwaa uweza WAKO ulio mkuu, na kumiliki. Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa WAKO manabii na watakatifu, na hao walichao jina LAKO, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi. Kisha Hekalu la MUNGU lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano LAKE likaonekana ndani ya hekalu LAKE. Na kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi.”
Jeshi la Anga la MUNGU, visahani virukavyo, UFOs, wanafanya uchunguzi yakinifu duniani wasaa huu kwa ajili ya maandalizi ya hukumu hizi za mwisho za MUNGU. Cheka kama unataka kucheka, lakini ni kweli vipo visahani virukavyo vikiendeshwa na malaika. Mamilioni ya watu wameviona, na havitoki kwenye sayari nyingine.

Kila wakati MUNGU anapofanya jambo, Shetani anajaribu kulifanya lionekane kana kwamba anaweza kulirudufu. Hata hivyo, Shetani hawezi kurudufu hili. Shetani anatuma maono ya uongo ya UFO, na kufanya mapepo yanayoviendesha yaonekane kama watu wadogo, wenye kasoro, na vichwa vikubwa vilivyokwenda kombo. Uigaji huu ni ili kukufanya udharau ukweli kwamba MUNGU anatuma Jeshi LAKE la anga la kimbingu katika eneo kabla ya malaika WAKE kuiangamiza dunia, pamoja na watu wote wanaompinga MUNGU na wanaochukia  serikali ya MUNGU, ambayo si serikali moja-ya-dunia, Umoja wa Mataifa (U.N.), Mpango Mpya wa Dunia (New World Order). Mpango Mpya wa Dunia ni serikali ya Shetani. Ni mnyama anayeongozwa na nabii wa uongo katika Roma, na inaongozwa kwa roho ya Shetani.6 Vatican ni kiti cha Shetani.7 MUNGU hakuumba watu au viumbe wowote wengine kwenye sayari nyingine yoyote ile. Watu wanafanya upumbavu kwa kufikiri hivyo!

Ufunuo 15:5 hadi 16:21 inasema, “Na baada ya hayo nikaona, na hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa; na wale malaika saba, wenye mapigo [ya mwisho] saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung’aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi [mikanda] ya dhahabu. Na mmoja wa wale wenye uhai wanne [wa mbinguni] akawapa wale malaika saba vitasa saba vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya MUNGU, aliye hai hata milele na milele. Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa MUNGU na uweza wake. Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo [ya mwisho] saba ya wale malaika saba. Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu vya MUNGU juu ya nchi. Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya, bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.

“Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa. Na huyo wa tatu akakimimina kitasa chake juu ya mito na chemchemi za maji; zikawa damu. Nami nikasikia malaika wa maji akisema, WEWE u mwenye haki, uliyeko na uliyekuwako, MTAKATIFU, kwa kuwa umehukumu hivi; kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, NAWE umewapa damu wainywe; nao wamestahili. Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, BWANA na MUNGU MWENYEZI, ni za kweli, na za haki, hukumu zako. Na huyo wa nne akakimimina kitasa chake juu ya jua, nalo likapewa kuwaunguza wanadamu kwa moto. Wanadamu wakaunguzwa kwa muunguzo mkubwa, nao wakalitukana jina la MUNGU aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubutu wala kumpa utukufu. Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama [Vatican ya Roma]; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao sababu ya maumivu, wakamtukana MUNGU wa mbingu kwa sababu ya maumivu yao, na kwa sababu ya majipu yao; wala hawakuyatubia matendo yao [kama ilivyo leo]. Na huyo wa sita akakimimina kitasa chake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika mawio ya jua. Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka [Shetani], na katika kinywa cha yule mnyama [mpinga Kristo, serikali moja ya dunia, Umoja wa Mataifa “U.N”, Mpango Mpya wa Dunia wenye makao yake makuu Roma, ambayo ni Vatican], na katika kinywa cha yule nabii wa uongo [Vatican, dini ya kishetani ya Katoliki ya Kirumi]. Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya MUNGU MWENYEZI.

“Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake [wokovu wake8], asiende uchi hata watu wakaione aibu yake. Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni. Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga, sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa. Pakawa, na sauti, na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za MUNGU, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira YAKE. Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana MUNGU kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno” (Ufunuo 16:14-21).

Ulimwengu wa Kikristo na idadi ya watu wote duniani kwa ujumla inahitaji sana kuwa na ufahamu wa ulimwengu usioonekana, ulimwengu wa malaika. Kuna malaika wema, na kuna malaika waovu. Malaika wema ni malaika wa MUNGU, nao huitwa “Walinzi.” Wao huchunguza kila mwenendo ambao mimi na wewe tunafanya, na wanasikia kila neno ambalo wewe na mimi tunasema.

Katika kitabu cha Mwanzo, Baba Abrahamu alimwelekeza mtumishi wake kwenda katika nchi ya asili ya Abraham, Mesopotamia, kumtafutia mwanawe Isaka mke. Alimwambia mtumishi wake, “BWANA, MUNGU wa mbingu, aliyenitoa katika nyumba ya babangu, na kusema nami katika nchi niliyozaliwa, aliniapia akisema, nitawapa uzao wako nchi hii; yeye atampeleka malaika wake [Mlinzi WAKE] mbele yako” (Mwanzo 24:7). Naye [MUNGU] alimtuma malaika WAKE mbele ya mtumishi wake [Mtumishi wa Abrahamu], na mtumishi akakutana na binti wa Bethueli, Rebeka, ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi kulingana na kitabu cha Jasher, sura ya 24, aya ya 40. Isaka alikuwa na umri wa miaka arobaini, kulingana na kitabu cha Jasher, sura ya 24 aya ya 45. Pia imethibitishwa katika kitabu cha Mwanzo 25:20. Ni Rebeka aliyemzaa Israeli kwa Isaka. Alimzaa Esau na Yakobo. MUNGU alibadili jina la Yakobo kuwa Israeli alipomshinda alipopigana NAYE miereka kule Mahanaimu (Mwanzo 32:24-28).

Alikuwa malaika wa BWANA aliyeliongoza taifa la Israeli kuvuka Bahari ya Shamu juu ya nchi kavu, na kabla ya tukio hili, alikwenda nyuma ya taifa la Israeli, kuja katikati ya  kambi ya Wamisri na kambi ya taifa la Israeli (Kutoka 14:15-20).

Mwanzo 19:1 inasema, “Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni.” Katika Mwanzo 19:12-13, wale watu wawili (malaika) wakamwambia Lutu, “Je! Unaye mtu [ndugu] hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa; maana [sisi malaika] tutapaharibu mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za BWANA; naye BWANA ametupeleka tupaharibu.”
Walikuwa malaika wawili tu walioiharibu Sodoma na Gomora na miji iliyoizunguka (Mwanzo 19:12-29). Na alikuwa ni malaika mmoja tu aliyeliua jeshi lote la askari wa Senakeribu. Baada ya Senakeribu kujigamba kwa Israeli jinsi gani jeshi lake lilikuwa na nguvu, 2 Wafalme 19:35 inasema, “Ikawa usiku uo huo MALAIKA WA BWANA [malaika mmoja] alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na themanini na tano elfu [185,000]. Na watu walipoondoka asubuhi na mapema, kumbe hao walikuwa maiti wote.”

Malaika mmoja aliharibu jeshi zima la Wamisri, na malaika mmoja aliharibu jeshi zima la Senakeribu. Malaika saba wataharibu dunia nzima. Kiasi gani watu wanapaswa kuogopa mamia ya UFO wanaoonekana, visahani virukavyo vikiendeshwa na malaika wa MUNGU, ambao kwa sasa, wapo kama ishara za onyo, wakiharibu sehemu mbalimbali duniani kama New York; New Jersey; New Orleans, Louisiana; Joplin, Missouri; Haiti; Indonesia; na Japan? Wanaharibu mamia ya sehemu nyingine kote duniani. BWANA anawapeleka malaika kuharibu miji na watu ulimwenguni kote.

Mathayo 24:21-22 inasema, “Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.”

Hivi sasa ni mwisho wa dunia. Wengine wamesema ulikuwa mwisho wa dunia, na walitoa tarehe kama vile walijua wakati sahihi aliochagua MUNGU. Mimi sifanyi hivi, bali nawaambieni huu ndio mwisho. Hudhani kwamba huu ni wakati mwafaka kwako kutubu dhambi zako na kuzaliwa tena kwa ROHO ili uweze kuishi milele katika Ufalme wa Mbinguni? Kama hii ni shauku yako, basi sali sala hii:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Hatimiliki Machi 2013, 2015 Haki zote zimehifadhiwa, Mchungaji wa Dunia Tony Alamo ® Imesajiliwa Machi 2013, 2015
SWAHILI—VOLUME 17600—WONDERS IN HEAVEN ABOVE AND SIGNS IN THE EARTH BENEATH


footnotes:

1. Mk. 13:12-13, Lk. 12:51-53, Yoh. 16:1-3 return

2. Mwa. 19:1, 13, 2 Sam. 24:15-17, 24:15-16, 2 Fal. 19:35, 2 Nya. 32:21, Zab. 78:49, Mat. 13:41-42, Mdo. 12:23, 2 Thes. 1:7-9, Ufu. 7:1-2, 9:15, 15:1, sura ya 16 return

3. Mwa. 19:12-25 return

4. Ufu. 8:7-13, 9:1-19, 11:19, 14:15-20, 15:1, 5-8, 16:1-12, 17-21 return

5. Mwa. 7:11-23, 1 Pet. 3:20 return

6. Dan. 2:40, 7:19-25, 12:1, Ufu. 13:2-8, 14:8, 16:13-14, 19-20, 17:1-9, 18:2-24 return

7. Ufu. 13:1-12, 17:1-9 return

8. Mat. 8:10-12, 13:37-43, 47-50, 22:8-14, 24:42-51, 25:1-13, Lk. 9:23-26, 62, 12:35-48, 14:15-35, Rum. 8:35-39, 2 Kor. 5:1-4, Ufu. 3:1-3, 8-22 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return