TOFAUTI KATI YA WOKOVU NA DINI

na Tony Alamo

Katika ulimwengu huu, kuna watu wengi wa kidini kuliko waliookoka, waliozaliwa mara ya pili katika ROHO. Biblia, kwa maneno mengi sana, hutueleza kwamba dini ni ya Ibilisi, lakini wokovu ni wa BWANA.1 

Tofauti kati ya kumwamini KRISTO na kuamini dini ni kwamba, kwa kumwamini KRISTO, MUNGU ndiye humtafuta mwanadamu. Kwa maneno mengine, ni MUNGU ambaye amemtafuta mwanadamu na bado amtafuta hadi sasa. Kwanza, MUNGU aliwasiliana kwanza na Adamu, Kaini, Sethi, Henoko, Nuhu, Ibrahimu, Isaka na Yakobo katika Agano la Kale. Katika Agano Jipya, kwanza aliwasiliana na Mathayo, Yohana na Mtume Paulo. Katika mwaka wa 1964, ALIWASILIANA nami, na kulikuwa na wengine wengi tangu nyakati za Biblia hadi sasa. Kwa maneno mengine, MUNGU amewatafuta kondoo wote wa kiume, viongozi wa familia YAKE, akiwatuma ili waende kuwatafuta kondoo ambao katika siku zijazo watakuwa wa mwisho kuokolewa, wale ambao wataishi  milele katika Ufalme wa Mbinguni pamoja na MUNGU BABA, KRISTO, MWANAWE wa pekee na ROHO  MTAKATIFU milele yote.

KRISTO hutuagiza wafuasi WAKE, sisi sote, kuwatafuta wengine ili wawe wafuasi WAKE, ili nao wafanye vivyo hivyo.2 Anafanya  hivi katika Mathayo 28:18-20 kwa maneno yafuatayo: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza [mkiwazamisha ndani ya maji mengi3] kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Amen.” Huyu ni KRISTO akimtafuta mwanadamu, lakini si mwanadamu akimtafuta MUNGU. Mwanadamu kumtafuta MUNGU ni “dini,” lakini wakati MUNGU amtafutapo mwanadamu, ni “wokovu.”

Dini zote humtaka mwanadamu ambaye hajaokoka amtafute MUNGU, au mwingine yeyote ambaye wanamdhania kuwa ndiye MUNGU. Dini ni nini? Dini ni imani ya mtu katika kile anachokidhania kuwa MUNGU na utii wake kwa kitu hicho. Katika kila ufahamu wa mwanadamu kuna mungu wa aina fulani, lakini hakuna wazo la  MUNGU mmoja wa kweli. Hii ndio sababu YESU, katika Mathayo 28:19, aliwaambia wanafunzi WAKE wa wakati huo, wanafunzi wake wote hadi leo, “Basi, enendeni, MKAWAFANYE MATAIFA YOTE [nani aliye MUNGU wa kweli ambaye wanapaswa kumwabudu, na ambaye wanapaswa kumwabudu na kumtumikia YEYE pekee] kuwa wanafunzi, mkiwabatiza [mkiwazamisha ndani ya maji mengi] kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU.’’

Ili tuingie mbinguni, ni lazima tuwe wakamilifu.4 Twaweza kuwa wakamilifu kwa sababu MUNGU ametuamuru tuwe wakamilifu, na MUNGU kamwe hajatuamuru tuwe kitu ambacho hatuwezi kuwa.5 Katika Mathayo 5:48 YESU asema, “Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama BABA yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.” Kama tunatembea katika ROHO MTAKATIFU, tu wakamilifu. Warumi 8:1-2 yasema, “Sasa, basi, hakuna hukumu [hakuna Jehanamu, hakuna Ziwa la Moto] ya adhabu juu yao walio katika KRISTO YESU, wasio tembea katika mwili, bali katika ROHO. Kwa sababu sheria ya ROHO wa uzima ule ulio katika KRISTO YESU imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.”(Imenakiliwa kutoka kwa KJV). Tambua kwamba andiko hili halisemi tunaweza kuwa huru mbali na sheria ya ki-maadili. Tunaweza tu kuwa huru mbali na sheria ya dhambi na mauti. Sheria ya dhambi na mauti husema kwamba ikiwa tutavunja sheria ya ki-maadili baada ya kuzaliwa mara ya pili na ROHO, hakuna dhabihu (msamaha) nyingine zaidi kwa ajili ya dhambi.  Waebrania 10:26-31 husema hili kwa namna hii, “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao [maadui wa MUNGU]. Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga MWANA wa MUNGU, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri ROHO wa neema? Maana twamjua YEYE aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu YANGU, MIMI nitalipa. Na tena, BWANA atawahukumu watu WAKE. Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya MUNGU aliye hai.” Hii ndiyo sababu kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima.6 Tunapaswa kufanya yale ASEMAYO, yaani kukaa mbali na dini, na kuzaliwa mara ya pili na ROHO. Huu ndio ufahamu ANAOUTAKA  kutoka kwetu, na kumcha BWANA ni ufahamu.

Katika Yohana 3:5, YESU alimwambia Nikodemo ni LAZIMA azaliwe kwa ROHO. Kamwe YESU hakusema ni lazima ujiunge na dini fulani. Kumwamini KRISTO kamwe sio sawa na aina yoyote ya dini. Tena, kumwamini KRISTO ni MUNGU anakuja kumtafuta mwanadamu, akitamani mwanadamu amtumikie YEYE.

Mara nyingi watu huuliza, “Kuna tofauti gani kati ya Ukristo na dini?” Wanaweza kuuliza, “Je, Ukristo ni dini?” Ili kujibu swali hili kwa uaminifu, mimi ningesema Ukristo sio dini. Ukristo wa kweli ni wokovu. Ingawa Ukristo huchukuliwa na watu ambao hawajaangaziwa kiroho kuwa mojawapo ya dini kuu tano duniani, ukweli ni kwamba kumwamini KRISTO sio kuamini dini. Tunaweza pia kuelezea jambo hili kwa kusema kwamba, wale wanaomwamini KRISTO kwelikweli, ni Wakristo, na wala sio wafuasi wa kile kinachodhaniwa kuwa dini ya Kikristo. Hadi leo, dini zina historia ya ukatili dhidi ya Ukristo.

Kanisa la Kirumi la Katoliki liliwaua mamilioni ya watu katika nyakati tatu tofauti za mahakama za kanisa za kuzima uzushi. Na wamefanya mauaji mengine mengi katika kipindi cha miaka elfu mbili iliyopita, kama vile mauaji ya Waco, ambapo watoto wengi, pamoja na wazazi wao waliuawa. Vitendo vya aina hii vya Kanisa Katoliki la Kirumi vinaendelea hadi wa leo.

Tunaweza kuangalia nyuma katika mahakama za kanisa za kuzima uzushi kule Uhispania, vilevile na vitendo vingine vya kinyama vilivyofanywa na Vatican. Hii hujumuisha Wayahudi milioni sita waliouawa kule Auschwitz na katika kambi nyingine za mateso za wanazi. Vita vya sasa dhidi ya Ukristo vinakuja kutokea Vatican.7 Mamia ya mamilioni ya dola ya mali zetu kutoka kwa wengi wetu yalichukuliwa. Wamelazimika kuacha mali yao  na wengi wetu ambao ni Wakristo wa kweli waliozaliwa mara ya pili tunatumikia vifungo vya maisha gerezani kwa mashtaka ya uongo kwa sababu ya dini ya Kikatoliki. Sizungumzii kuhusu wale wakongwe wa kike na kiume wa Kikatoliki ambao hushiriki shughuli za kishetani za kidini za Kanisa Katoliki la Kirumi. Hawa, hawana ufahamu wa mambo haya kama ilivyo kwa sehemu kubwa ya watu wanaosalia katika ulimwengu huu. Hata hivyo, haya ninayoyasema ni ukweli mtupu.

Wakati kengele za makanisa ya Katoliki na Kilutheri zilipokuwa zikilia huko Poland, mamilioni ya watu wasio na hatia waliuawa huko Ujerumani kwenye vyumba na majengo ya majiko ya gesi, kisha kuburutwa kwa buldoza na kumwagwa kwenye mashimo makubwa (makaburi ya watu wengi). Nimesimuliwa kwamba baadhi yao walikuwa wangali hai. Watazamaji waliyaona haya yote na kuyasikia yote.8 MUNGU aliyaona yote, na MUNGU aliyasikia yote.9 Mshukuru MUNGU kwa ajili ya Siku ya Hukumu, ambayo iko karibu kuja.10

Luka sura ya 12, mstari wa 1-5 husema, “Wakati huo, makutano walipokutanika elfu elfu, hata wakakanyagana, [YESU] ALIANZA kuwaambia wanafunzi WAKE kwanza, Jilindeni na chachu ya Mafarisayo [Wayahudi wenye kushika dini], ambayo ni unafiki [dhambi]. Lakini hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa ambalo halitajulikana. Basi, yoyote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani [na walinzi na MUNGU]; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari. Nami nawaambia ninyi rafiki ZANGU, msiwaogope hao wauuao mwili, kisha baada ya hayo hawana wawezalo kutenda zaidi. Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni YULE ambaye AKIISHA KUMWUA mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanum; naam, nawaambia, Mwogopeni HUYO [MUNGU MWENYE UWEZO WOTE].”

MUNGU alimjia Adamu, ambaye hakujua lipi la kufanya. MUNGU alimwambia ale matunda ya mti wa UZIMA ili aweze kuishi milele, lakini badala yake alikula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambao MUNGU alimkataza asile.11 Kwa mara nyingine, MUNGU alimjia Adamu na maarifa ya wokovu, lakini Adamu alichagua dini ya Shetani (ujuzi). Pia MUNGU huujia ulimwenguni wote na maarifa ya wokovu, ukiwamo na wewe, lakini kama kupe ambao hung’ang’ania kwenye ngozi ya wanyama na binadamu, kuna uwezekano mkubwa wewe pia kung’ang’ania kwenye dini fulani ya Kishetani, sivyo?

MUNGU alimjia Sethi na maarifa ya wokovu, na kisha Sethi akaanza kumwabudu MUNGU. Kisha MUNGU akamjia Enoko ambaye alitembea na MUNGU, na MUNGU akamchukua mbinguni kuwa pamoja NAYE.12 Kisha tena MUNGU akamjia Nuhu.13  Nuhu hakumjia MUNGU wala hata mmoja wa hao wengine. MUNGU aliwajia. Ibrahamu alikuwa mwabudu sanamu; mwanachama wa dini [fulani], lakini MUNGU alimjia. Ibrahamu hakumjia MUNGU.14 Musa hakumjia MUNGU; MUNGU alimtokea, na akamjia Musa.15 MUNGU aliwajia watu mamia wengine kama vile wanafunzi wa YESU. Alimjia Mtume Paulo, mtu wa dini, na kumfanya aokoke. 16 Paulo akafanyika kuwa mwenye manufaa kwa MUNGU katika wokovu wake, akapigana vita vyema dhidi ya nguvu za giza ambavyo pia vilihusisha maandiko yake yenye wastani wa theluthi mbili ya Agano Jipya lote. Haya yoye yalihusishwa katika wokovu wa kweli.

Katika kitabu cha Danieli, vijana watatu wa Kiebrania (Shadraka, Meshaki na Abednego) wote walitupwa katika tanuru ya moto kwa sababu hawakuabudu sanamu ya dhahabu ya mfalme – kwa sababu walikataa kuwa sehemu ya dini ya mfalme.17  “Ule moto ulikuwa hauna nguvu [juu ya miili yao], wala nywele za vichwa vyao hazikuteketea, wala suruali zao hazikubadilika, wala harufu ya moto haikuwapata hata kidogo. Nebukadreza akanena, akasema, na ahimidiwe MUNGU wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika WAKE, akawaokoa watumishi WAKE waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine [dini yoyote], wala kumwabudu, ila MUNGU wao wenyewe” (Danieli 3:27-28). Katika Agano Jipya, Mtume Yohana alipitia uzoefu uleule. Alichemshwa katika mafuta wala hakuungua. Wala hakufa kutokana na tukio hilo.

Ni ajabu kwamba katika Biblia yote, wakati wowote mwanadamu awapo na mawasiliano na MUNGU, ni kwa sababu daima MUNGU ndiye amewasiliana naye kwanza. Pia MUNGU alimtafuta Ayubu kwanza, na kisha Ayubu akamtumikia. Hakuna habari yoyote katika Biblia ambapo mwanadamu alimtumikia MUNGU kwa sababu kwanza alikuwa na mawazo ya kumtumikia MUNGU.

Biblia nzima huzungumzia MUNGU ajaye kumtafuta mwanadamu. Siku moja, Isaya aliona maono na kusikia sauti ya BWANA ikisema, “…Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili YETU? Ndipo niliposema, mimi hapa, nitume mimi” (Isaya 6:8). Baada ya kuona maono, Yeremia alisimama kuwatabiria wana wa Israeli maneno ambayo YEHOVA alimwamuru kunena (Yeremia 1:4-9). Pia Danieli aliona maono kabla ya hajaamua kuomba na kufunga, akimsihi YEHOVA kuurejesha Yerusalemu (Danieli sura 7-9). Biblia nzima huonesha kwamba MUNGU humjia kwanza mwanadamu kabla mwanadamu hajamtumikia MUNGU.

MUNGU anawasiliana nawe kupitia kwangu na wachungaji wengine ambao wameokoka na wainjilisti, na kwa hivyo hauna udhuru. ROHO wa MUNGU, ambaye anaishi na kutenda kazi ndani yetu na kupitia kwetu sisi ambao tumeokoka, anakutafuta, awasiliane nawe, sio kwa ajili ya dini, bali kwa ajili ya wokovu wako na wokovu wa wengine.

Warumi 10:12-15 husema waziwazi kwamba wahubiri watumwao na MUNGU lazima wapelekwe  duniani  kote ili watu wauamini wokovu kwa kutumia maneno haya: “Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani [mtu wa mataifa]; maana YEYE yule ni BWANA wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka. Basi wamwiteje YEYE wasiyemwamini? Tena wamwaminije YEYE wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!”

Kwa mara nyingine, YESU ametutuma kwako. MUNGU anakutafuta; sio wewe unayemtafuta MUNGU.  Ukweli huu umeelezwa kwako katika Luka 10:1-12 ambayo husema,  “Basi, baada ya hayo BWANA aliweka na wengine, sabini [wanafunzi], akawatuma wawili wawili WAMTANGULIE  kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda MWENYEWE. AKAWAAMBIA, mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni BWANA wa mavuno APELEKE watenda kazi katika mavuno YAKE. Enendeni, angalieni, NAWATUMA kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu. Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. Na nyumba yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na akiwamo MWANA wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu. Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii. Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa MUNGU umewakaribia. Na mji wowote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni, Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa MUNGU umekaribia. Nawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi zaidi Sodoma kuistahimili adhabu yake kuliko mji huo.”
Wale wanaoiamini dini huchukua jukumu la kutumikia kile wanachokidhania kuwa ni mungu, wakati wale wanaomwamini KRISTO humtumikia MUNGU baada ya kushawishiwa na kuguswa na MUNGU. Kwa sababu hii, ninasema kwamba mtu yeyote hapaswi kuwa na haraka ya kumtumikia mungu ambaye ni kitu cha kubuni tu, yaani kutumikia dini tu. Twamtumikia MUNGU tu wakati YEYE, kwa ROHO WAKE, yu ndani yetu.18 Ikiwa tutamtumikia MUNGU bila YEYE kwanza kuishi ndani yetu, tuko ndani ya dini na wala sio ndani ya wokovu. Tukiongea kwa mafumbo, watu wengi leo wanabandika bango la “Mkristo” kwa nje, lakini kwa ndani wanahusika na biashara za kidini. Wao ni Wakristo katika akili zao wenyewe, lakini katika uhalisia wao ni wanadini tu.

Kuwa Mkristo ni nini? Mkristo ni mtu ambaye KRISTO anaishi na kutenda kazi ndani yake kwa njia ya ROHO MTAKATIFU, naye huendeshwa na ROHO MTAKATIFU ili kumtumikia MUNGU.19 Kwa upande mwingine, mtu wa kidini ni yule anayeamini ya kwamba anamtumikia mungu na kutamani kutenda yale ambayo anadhani huyo mungu angemtaka ayafanye. Hii ndio hali ya watu wengi wanaokiri kuwa Wakristo leo. Wanaukiri Ukristo, lakini hawajazaliwa mara ya pili. Hawajaokolewa, kwa hiyo hawamjui KRISTO, na hawana ufahamu wa jinsi ya KUMTUMIKIA. Hawawezi kumfuata KRISTO kwa sababu hawawezi KUMSIKIA.20 Kwa hiyo, wanatenda mambo kwa mapenzi yao, na MUNGU wa kweli hawezi kuwatumia. Hawafai. Walakini, kwa uzoefu wa wale walio Wakristo wa kweli, BWANA NDIYE awaongozaye katika mambo yote. Kwa urahisi wao husema, “Ndio. Amina.” BWANA ndiye kiongozi wao na MUNGU wao. Hii ni tofauti kabisa na njia ya watu wa kidini.

Baada ya Mtume Paulo kukutana na BWANA kwenye barabara ya kwenda Dameski, maneno ya kwanza aliyoyazungumza yalikuwa, “U nani WEWE, BWANA?” (Paulo alifahamu kuwa alikuwa ni BWANA, kama sivyo asingeuliza, “U nani WEWE, BWANA?”) Kisha BWANA akamwambia, “MIMI ndimi YESU unayeniudhi wewe  [Pindi mtu yeyote amtesapo mshiriki wa kanisa  la KRISTO, anamtesa KRISTO. Hii ni kwa sababu sisi ni mwili WAKE, hekalu LAKE, yaani Mwili wa KRISTO].” 1 Wakorintho 3:16-17 hutuambia  hivi, “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la MUNGU, na ya kuwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la MUNGU [Mwili wa BWANA, ambao ndio sisi], MUNGU atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la MUNGU ni Takatifu, ambalo ndilo ninyi.” Ni Takatifu kwa sababu hamfuati dini mfu, ambayo kwayo KRISTO na BABA, kwa njia ya ROHO haishi ndani yake, lakini wewe ni Mkristo uliyezaliwa mara ya pili. KRISTO kwa njia ya BABA na kwa njia ya ROHO, huishi ndani yako, kama umeokolewa, u hekalu la MUNGU. Hii ndio sababu MWILI ambao MUNGU anaishi ndani yake ni Mtakatifu, na mwili ambao MUNGU haishi ndani yake sio Mtakatifu ila ni najisi. Kwa hakika utataka kuwa Mtakatifu zaidi kila kitu wakati utakaposimama kwenye Kiti cha Hukumu cha MUNGU.

Dunia imejaa vikwazo na vizuizi. Hivi ni vikwazo vya Shetani vinavyofanya akili yako kukosa mwelekeo kwenye jambo lililo muhimu kabisa katika ulimwengu huu, ambalo ni kuidumisha roho yako katika kumtumikia MUNGU na kumdumisha KRISTO na BABA YAKE kuishi ndani yako. “Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake; kwa maana hudhaniwaje kuwa ni kitu?” (Isaya 2:22).

Chagua jambo moja: je, unataka kuwa MWILI Mtakatifu wa MUNGU, au unataka kuwa mwili mwingine tu wowote ulio najisi ambao ndani yake Shetani hukaa? Ikiwa chaguo lako ni kuwa MWILI wa KRISTO, omba sala hii:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Hatimiliki Aprili 2013, 2015 Haki zote zimehifadhiwa Mchungaji wa Ulimwengu Tony Alamo   ® Imesajiliwa Aprili 2013, 2015
SWAHILI—VOLUME 17800—THE DIFFERENCE  BETWEEN SALVATION AND RELIGION


footnotes:

1. Isa. 1:11-16, 29:13-14, Yer. 7:8-11, 23:33-40, Eze. 13:1-23, Mik. 3:11, Mat. 6:5, 7-8, 7:21-23, 15:7-9, 21:28-32, 23:1-37, Lk. 6:46, 18:10-14, Yoh. 5:40, 6:35-58, 10:1-15, 14:6, 15:2, 2 Tim. 3:1-7, Tit. 1:16, Yak. 2:19 return

2. Dan. 12:3, Mat. 10:7-8, 28:19-20, Lk. 24:46-48, Mdo. 1:8, 2:38-41, 10:39-43, Rum. 7:4, 10:13-15, 1 Kor. 1:17-18, 21, 9:16-17, Efe. 3:2-10, Kol. 1:25-29, 2 Tim. 4:2, 5 return

3. Mat. 28:19, Rum. 6:3-5, Kol. 2:10-12 return

4. Kumb. 18:13, 1 Fal. 8:61, Zab. 119:1-3, Mat. 5:48, 2 Kor. 13:11, Efe. 4:11-13, 5:25-27, Flp. 3:12-15, Kol. 1:21-22, 1 Tim. 6:14, 2 Tim. 3:16-17, Yak. 1:4, 1 Yoh. 3:6-10, Ufu. 21:7, 27 return

5. Mwa. 17:1, Law. 11:44-45, 19:2, 20:26, Kumb. 18:13, 1 Fal. 8:61, Zab. 15:1-5, 24:3-5, 119:1-3, Yoh. 17:17-23, Rum. 6:4-14, 8:1-14, 37, 2 Kor. 6:14-17, 13:11, Gal. 5:16, Efe. 4:11-13, 5:25-27, 6:10-18, Flp. 1:9-11, 2:12-15, 3:12-14, 4:13, Kol. 1:10-11, 21-22, 1 Thes. 4:6-7, 1 Tim. 6:11-14, 2 Tim. 3:16-17, Ebr. 2:18, 12:14, 13:20-21, Yak. 1:4, 27, 1 Pet. 1:15-16, 5:8-10, 1 Yoh. 2:14, 3:5-10, 4:4, Ufu. 3:1-5, 7:13-15 return

6. Ayu. 28:28, Zab. 111:10, Mith. 1:7, 9:10, 15:33 return

7. Dan. 7:7, 19-27, Ufu. 13:1-7, 17:1-18 return

8. Yer. 4:16, Danieli sura ya 4, Mat. 13:24-30, 36-43, 47-50, 24:29-31, Lk. 15:4-10, 1 Kor. 11:10, 1 Tim. 5:21, Ufu. 14:13-20 return

9. Kumb. 31:21, 2 Fal. 19:27, 1 Nya. 28:9, Ayu. 31:4, 34:21-22, 25, Zab. 44:21, 139:1-6, 12-16, Mith. 15:3, 11, Isa. 29:15-16, Lk. 16:15, Ebr. 4:13, 1 Yoh. 3:20 return

10. Mhu. 12:13-14, Dan. 7:9-10, Mat. 3:12, 24:3-15, 29-44, Mk. 4:22, Rum. 2:5-13, 16, 14:10-12, 2 Kor. 5:10-11, 2 Thes. 1:7-10, 2 Tim. 4:1, 8, Ebr. 10:30-31, Yud. 14-15, Ufu.1:7, 11:18, 20:11-15 return

11. Mwa. 2:16-17, 3:1-6 return

12. Mwa. 5:22-24, Ebr. 11:5 return

13. Mwa. 6:11-18, 22, Ebr. 11:7 return

14. Mwa. 12:1-8, 17:1-9, Mdo. 7:2-3, Ebr. 11:8 return

15. Kut. sura ya 3, Mdo. 7:29-34 return

16. Mdo. 9:1-22, Gal. 1:13-19 return

17. Dan. sura ya 3 return

18. Eze. 36:27, Yoh. 14:15-20, 23, 26, 15:1-11, 26, 16:7-14, Rum. 8:1, 10-11, 26-28, 1 Kor. 3:9, 16-17, 6:19-20, 2 Kor. 6:16-18, Efe. 2:18-22, Flp. 2:12-13, Kol. 1:27-29, 2 Tim. 1:14, 1 Yoh. 4:4, 5:12 return

19. Isa. 30:21, Yoh. 15:1-5, 17:21-23, 26, 1 Kor. 15:10, 2 Kor. 5:17-21, Gal. 2:20, Efe. 3:16-21, 1 Yoh. 2:20, 27 return

20. Yoh. 8:42-43, 10:27 return

21. return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return