JE! MUNGU ANAMPA MWANAMKE HAKI YA KUTOA MIMBA IWAPO NI MHANGA WA UBAKAJI?

na Tony Alamo

MUNGU anasema, “Tazama, roho zote ni mali YANGU; kama vile roho ya baba ni mali YANGU, ndivyo ilivyo roho ya mwana. Mali YANGU; roho itendayo dhambi, itakufa. Bali kama mtu ni mwenye haki, na kuyatenda yaliyo halali na haki; hakula juu ya milima [kuabudu sanamu], wala hakuviinulia macho vinyago vya nyumba ya Israeli, wala hakumtia unajisi mke wa jirani yake [kuzini naye], wala hakumkaribia mwanamke wakati wa kutengwa kwake; wala hakumdhulumu mtu, bali amemrudishia mdeni wake rehani yake, wala hakumnyang’anya mtu mali yake kwa nguvu, naye amewapa wenye njaa chakula chake, na kuwavika nguo walio uchi; ambaye hakumkopesha mtu ili apate faida, wala hakupokea ziada ya namna yoyote; naye ameuepusha mkono wake na uovu, na kufanya hukumu ya haki kati ya mtu na mwenzake; tena ikiwa amezifuata sheria ZANGU, na kuzishika hukumu ZANGU; mtu huyu ni mwenye haki; hakika ataishi, asema BWANA MUNGU.

“Walakini akizaa mwana aliye mnyang’anyi, mmwaga damu, atendaye mambo hayo mojawapo; wala hakutenda mojawapo la mambo hayo yampasayo, bali amekula juu ya milima [kuabudu sanamu], na kumtia unajisi mke wa jirani yake [kuzini naye], na kuwadhulumu maskini na wahitaji, na kuwanyang’anya watu mali yao kwa nguvu, wala hakurudisha rehani [hajalipa zaka zao], naye ameviinulia macho vinyago, na kufanya machukizo, naye amekopesha watu ili apate faida na kupokea ziada; Je! Ataishi [milele] baada ya hayo? La, hataishi [milele]; amefanya machukizo hayo yote; hakika atakufa; damu yake itakuwa juu yake.

“Na kama yeye huyo akizaa mwana, naye ameona dhambi zote za baba yake alizozitenda, akaogopa, asifanye neno lolote kama hayo; hakula juu ya milima [kuabudu sanamu], wala hakuviinulia macho vinyago vya nyumba ya Israeli, wala hakumtia unajisi mke wa jirani yake [kuzini naye], wala hakumdhulumu mtu, wala hakutwaa kitu kiwekwe rehani [hakuzuia zaka na sadaka zake], wala hakumnyang’anya mtu mali yake kwa nguvu, bali amewapa wenye njaa chakula chake, na kuwafunika nguo walio uchi; tena ikiwa ameuzuia mkono wake asimwonee maskini, wala hakupokea faida na ziada, naye amezifanya hukumu ZANGU, na kuzifuata sheria ZANGU; hatakufa  huyu kwa sababu ya uovu wa baba yake, hakika ataishi [milele]. Kwa habari za yule baba yake, kwa sababu aliwaonea watu kwa ukali mwingi, na kumnyang’anya ndugu yake mali yake kwa nguvu; na kuyatenda yasiyo mema kati ya watu wake, tazama, atakufa [milele] katika uovu wake.

“Lakini ninyi mwasema, kwani yule mwana asiuchukue uovu wa baba yake? Yule mwana atakapofanya yaliyo halali na haki, na kuzishika mari ZANGU na kuzitenda, hakika ataishi [milele]. Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa [milele]; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki ya mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.

“Lakini mtu mbaya akighairi; na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri ZANGU zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi [milele], hatakufa [milele]. Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi. Je! Mimi ninafurahia kufa [milele] kwake mtu mwovu? Asema BWANA MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi [milele]?” (Ezekieli 18:4-23).

MUNGU hasemi tu kuwa roho zote ni ZAKE, lakini katika Hesabu 16:22, Musa na Haruni walisema YEYE ni “MUNGU wa roho za wenye mwili WOTE.” Katika Yeremia 32:27 MUNGU anasema, “Mimi ni BWANA, MUNGU wa WOTE wenye mwili.” MUNGU, katika Yeremia 1:5, alimwambia, “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua.”

Jinsi gani mtu yeyote aweza kuwa na ujasiri wa kuiharibu nafsi, roho na mwili wa mtoto yeyote mchanga wa mwanadamu ambaye MUNGU alimjua kabla kuumbwa katika tumbo, waache kabla ya kutoka tumboni, hata katika tukio la kubakwa?

Sheria halisi ni sheria ya MUNGU.1 Hebu tuone sheria ya MUNGU inavyosema: “Akifumaniwa mtu mume amelala na mwanamke aliyeolewa na mume, na wafe [kimwili na kiroho] wote wawili, mtu mume aliyelala na mwanamke, na yule mwanamke naye; ndivyo utakavyoondoa uovu katika Israeli. Pakiwa na kijana aliye mwanamwali ameposwa na mume [amechumbiwa], na mwanamume akimkuta mjini, akalala naye; watoeni nje katika lango la mji ule, mkawapige kwa mawe hata wafe; yule kijana, kwa kuwa hakupiga kelele, naye yu ndani ya mji; na yule mume, kwa kuwa amemtweza mke wa mwenzake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako. Lakini yule mtu mume kama akimkuta kondeni kijana aliyeposwa, naye mume akamtenza nguvu [akambaka], akalala naye; yule mtu mume aliyelala naye na afe pekee; lakini yule kijana usimfanye neno; hana dhambi yule kijana ipasayo kuuawa: kwa kuwa ni mfano wa mtu kumwondokea mwenzake akamwua, ni vivyo lilivyo jambo hili: kwani alimkuta kondeni, yule kijana aliyeposwa akalia [akalia kuomba msaada kwa sababu hakutaka kubakwa], pasiwe na mtu wa kumwokoa [ili asibakwe]. Mtu mume akimwona kijana aliye mwanamwali ambaye hajaposwa, akamshika na kulala naye [akambaka], wakaonekana; yule mtu mume aliyelala naye na ampe baba yake yule kijana shekeli hamsini za fedha, kisha na awe mkewe, kwa kuwa amemtweza; hana ruhusa ya kumwacha [kumpa talaka] siku zake zote” (Kumbumkumbu la Torati 22:22-29).

Kwa mara ya kwanza nilipoiona sheria hii nilifikiria, “Mwanamke awezaje kutaka kuolewa na mwanaume yeyote ambaye alimbaka?” Kisha kwa haraka, akili yangu ilirudi nyuma hadi miaka arobaini na nane iliyopita katika ofisi ya mwanasheria katika Beverly Hills ambapo kwa mara ya kwanza nilifahamiana na MUNGU. ALINIAMURU kuwaambia watu katika ofisi ile kwamba YESU KRISTO ALIKUWA ANAKUJA duniani tena. ROHO WA MUNGU alikuwa juu yangu kwa nguvu ya namna hiyo, nami nilianza kuhojiana NAYE, nikisema, “BWANA, nitawaambia kesho. Nitawapigia simu. Nitawatumia nyaya, telegramu, lakini usinifanye niwaambie sasa.” Ofisi ilikuwa imejazwa na wasaidizi wa watu wangu na watu wengine kutoka tasnia ya filamu. Nilidhani wangenikamata na kunipeleka kwenye hifadhi ya wendawazimu kama ningefanya kile ALICHOKUWA AKINIAMBIA kusema na kufanya. Hivyo MUNGU ALIANZA kuivuta roho yangu, nafsi yangu, ndani na nje ya mwili wangu, na kunifahamisha kuwa kama nisingesema kile ALICHONIAMBIA kusema, ningekufa saa ile papo hapo. Hapakuwa na chochote ambacho ningeweza kufanya KUMZUIA kuniua. Wakati huo huo, nilikuwa nikihisi jinsi ALIVYOKUWA na nguvu na akili nyingi, na nilifahamu kuwa hakuna yeyote aliyeweza KUMZUIA kufanya lolote ALILOTAKA kulifanya. Kabla ya jambo hili kunitokea, sikuwahi kumwamini MUNGU au YESU. Nilifahamika kama wakala bora wa matangazo katika aina yoyote ya biashara ikiwa ni pamoja na biashara za maonyesho. Tokea siku ile na kuendelea, niliacha kuwa wakala wa matangazo na nikaanza kumtafuta BWANA. Sina tatizo kuamini chochote alichosema MUNGU au asemacho. Kama MUNGU anamwambia mwanamume ni lazima amuoe mwanamke aliyembaka ambaye hajaolewa na kuishi naye maisha yake yote, na kisha anamwambia mwanamke kuwa lazima aolewe na mwanamume huyo na awe tayari kuishi naye hadi atakapokufa, ningependekeza kuwa wafanye hasa kile MUNGU anachowaamuru kufanya.

Tena, mara ya kwanza nilipoiona sheria hii, ilionekana kuwa kali kwangu. Sasa kwa kuwa namjua MUNGU na nguvu zake YAKE, najua pia kwamba YEYE ni BOSI. Unajua, wanawake wa leo wanabaka kirahisi. Wanaweza kuonekana kama malaika, lakini sivyo walivyo. Nimekutana na wengi wao ambao wanaonekana kama malaika lakini nimegundua ni waongo na ibilisi.

Mwanamke akiwa na mimba kwa sababu alibakwa, asiitoe. Akiitoa, huo utakuwa uuaji nambari moja, na atakwenda Jehannamu kwa sababu hiyo. Kutoka 20:13, Kiebrania cha awali, kinasema, “Usiue,” na yeyote atakayeua ni lazima auawe. “Uuaji” ni pamoja na wa watoto wachanga wasiozaliwa. “Mtu awaye yote ampigaye mtu, hata akafa, hana budi atauawa huyo” (Kutoka 21:12). Nini kitatokea kwa wauaji wote? “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na WAUAJI, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili” (Ufunuo 21:8). Na watu ni waongo kwa kusema kuwa watoto ambao hawajazaliwa si watu na si hai. Kama watoto hawa wachanga si hai, basi wanawezaje kuwaua? Na kwa nini wawaue kama si hai?

Wale wanaotoa mimba na wale wanaofanya kazi ya kutoa mimba, na wale walipua mabomu ya kujiua wote ni WAUAJI. Unapaswa kutubu sasa kwa sababu hukumu inakuja upesi kuliko unavyofikiri.
Katika Kutoka 21:22-25, tunaona adhabu ya kutoa mimba kwa bahati mbaya. “Watu waume wakiteta pamoja, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mume wa huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema. Lakini kwamba pana madhara zaidi, ndipo utatoza UHAI KWA UHAI, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, kuteketeza kwa kuteketeza, jeraha kwa jeraha, chubuko kwa ajili ya chubuko.” Mtoto anayekua tumboni mwa mama ni hai.

Katika Mathayo 22:31b-32, YESU alisema, “Hamjalisoma neno lililonenwa na MUNGU, akisema, Mimi ni MUNGU wa Ibrahimu, na MUNGU wa Isaka, na MUNGU wa Yakobo? MUNGU si MUNGU wa wafu bali wa walio HAI.” Tena, mtoto anayekua tumboni mwa mama yu HAI na anakua, na MUNGU ni baba wa mtoto wa mwanadamu.2

Waabudu sanamu wanajulikana vyema kwa uuaji wa watoto wao wenyewe, hadi siku hii ya leo. Yeremia 32:35 inasema, “Tena walijenga mahali palipoinuka kwa Baali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwapitisha wana wao na binti zao katika moto [mauaji/kuavya mimba] kwa ajili ya Moleki, jambo nisilowaagiza; wala HALIKUNIINGIA moyoni MWANGU kwamba walitende chukizo hilo; wapate kumkosesha Yuda.”

Makahaba wawili walimjia mfalme Sulemani, mtu mwenye hekima kuliko wote duniani,3 wakiwa na mgogoro: “Ndipo wanawake wawili, makahaba, walimwendea mfalme, wakasimama mbele yake. Na mwanamke mmoja akasema, Ee bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja; nami nalizaa nilipokuwa pamoja naye nyumbani. Kisha, siku ya tatu baada ya kuzaa kwangu, ikawa mwanamke huyu naye akazaa; na sisi tulikuwa pamoja; hapakuwa na mtu mwingine pamoja nasi nyumbani, isipokuwa sisi wawili tu.

“Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia. Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu, nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipotazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa. Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme. Ndipo mfalme akasema, Huyu anasema, Mtoto wangu yu hai, na mtoto wako amekufa. Na huyu anasema Sivyo hivyo; bali mtoto aliyekufa ni wako, na mtoto aliye hai ni wangu. Mfalme akasema, nileteeni upanga. Wakaleta upanga mbele ya mfalme. Mfalme akasema, mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu na huyu nusu.

“Ndipo mwanamke yule, ambaye mtoto aliye hai ni wake, akamwambia mfalme kwa maana moyoni mwake alimwonea mtoto wake huruma, akasema, Ee bwana wangu, mpe huyu mtoto aliye hai, wala usimwue kamwe. Lakini yule mwingine akasema, Asiwe wangu wala wako; na akatwe. Ndipo mfalme akajibu, akasema, Mpe wa kwanza mtoto aliye hai, maana yeye ndiye mama yake. Na Israeli wote wakapata habari ya hukumu ile aliyoihukumu mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya MUNGU ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu” (1 Wafalme 3:16-28).

Ingekuwa jambo jema kwa wanawake wa leo wanaopenda kuua vitoto vichanga kuanza kuwa na moyo huo huo kama kahaba mwenye huruma aliyeelezwa hapo juu, ambaye alisema mwache mtoto! Alikuwa ni mama!

Mwigizaji Tony Curtis aliulizwa alikuwa ameonaje kumbusu Marilyn Monroe. Mrembo kama wanaume wengi walivyofikiri kuwa alikuwa, Tony Curtis alisema, “Ilikuwa kama kumbusu Hitler!” Nimesikia kwamba Marilyn Monroe ametoa mimba kadhaa, kwamba ameua vichanga kadhaa. Pengine hii ndiyo sababu Curtis, Myahudi, anazikumbuka kambi za kifo za Vita ya Pili ya Dunia, ambapo Wayahudi milioni sita wasio na hatia waliuawa na Hitler.Alidhani ilikuwa kama kumbusu Hitler alipoulizwa wakati alipombusu Marilyn Monroe katika filamu. Hivi ndivyo ninavyojisikia kuhusu wanawake wa leo wanaoamini katika utoaji wa mimba, uuaji! Mwanaume yeyote awezaje kutaka kubusu mmoja wao?

Zaburi 82:3-4 inasema, “Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara [“fukara” wakiwa ni wanadamu ambao hawajazaliwa ambao wanachukuliwa kama sio mwanadamu]. Mwokoeni maskini na mhitaji; Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.” Fanya hivi uishi (milele). Tubu dhambi zako zote. Sali sala hii:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Hatimiliki Desemba 2013, 2015 Haki zote zimehifadhiwa Mchungaji wa Ulimwengu Tony Alamo ® Imesajiliwa Desemba 2013, 2015
SWAHILI—VOLUME 18700—DOES GOD PERMIT A WOMAN THE RIGHT TO HAVE AN ABORTION IF SHE IS A VICTIM OF RAPE?


footnotes:

1. Kut. 20:3-17, Zab. 111:7-8, 119:89, 152, 160, Mit. 3:1-2, Isa. 40:8, Yer. 23:29, Dan. 7:9-10, Mal. 4:4, Mat. 5:17-19, Mk. 13:31, Rum. 3:31, Yak. 2:8-13, 1 Pet. 1:23-25, Ufu. 20:12-13 return

2. Amu. 13:5, Ayu. 31:15, Isa. 49:5, Yer. 1:5, Lk. 1:15, 39-41 return

3. 1 Fal. 4:29-34, 2 Nya. 1:7-12 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return