MAJARIBIO MATATU YASIYOFANIKIWA KUMPINDUA MUNGU

na Tony Alamo

Je, haikuudhi kwamba Shetani ameidanganya dunia nzima? Amefanya haya katika matukio matatu ambapo, wazi wazi amejaribu kuchukua nafasi ya MUNGU na Ufalme wa MUNGU. Majaribio yake mawili yameshindwa vibaya, na hili la tatu analofanya sasa hivi litashindwa hivi karibuni.

Jaribio la kwanza la Shetani kumpindua MUNGU lilikuwa katika bustani ya Edeni, wakati Shetani alipomuuliza Hawa, “Hivi ndivyo alivyosema MUNGU?” Mwanzo 3: 1-3 inasema, “Basi nyoka [Shetani] alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA MUNGU. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema MUNGU, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke [badala ya kukemea na kumkataa] akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula.” Lakini MUNGU alisema, kuhusu matunda ya mti wa katikati ya bustani, “Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.” Wakati MUNGU anasema “msije mkafa,” YEYE hasemi kifo ni cha muda mfupi, jambo la dakika. Humaanisha kifo ni mauti ya milele kwa roho ya mwanamme au mwanamke, milele katika moto wa Jehannamu, mauti ya milele. Ukweli wa jambo hili umeelezwa katika Maandiko ya Agano la Kale na Jipya.1

Mwanamke, kama ilivyo kwa wakazi wengi wa dunia, kamwe hawaoti kwamba unapokubali hoja za Shetani, unakubali umilele unaoogofya na kutisha, Jehannamu isiyokuwa na mwisho, ambayo ina athari zaidi zinazochizisha kwa pamoja roho na akili ya muhanga wake. Kuzimu itacheua moshi wa maumivu ya waovu milele (Ufunuo 14:9-11). Wale wanaomwabudu (yaani kumsikiliza) Shetani, serikali yake ya dunia-moja, na kanisa lake la dunia (Katoliki) watakumbwa na mauti hayo hayo.2 Shetani katika umbo la nyoka, hufanya hila, kama alivyomdanganya Hawa, na sasa anadanganya dunia nzima.3

Katika kitabu cha Ufunuo 12:9, Shetani ameelezewa kama joka kubwa. “Yule joka akatupwa, yule mkubwa [kutoka Mbinguni], nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote.” Shetani alijua kwamba kwa kumdanganya Hawa, angeweza kuihukumu dunia nzima.4 Hawa alikuwa mwinjilisti wa kwanza wa Shetani; alikuwa mbuzi wa kwanza. Ili kuwa mbuzi wa Shetani, huwezi kumwamini YESU, au kuwa mmoja wa wanafunzi WAKE. Huwezi kuishi maisha ya KRISTO ya kusulubiwa, bali utalazimika kuwa huru kutenda yanayokupendeza. Huwezi kumshuhudia KRISTO bali kumkana, YEYE AJAYE ulimwenguni kuwaokoa wadhambi.5

Wakati Shetani alipomwambia Hawa kwamba, hakika hamtakufa, mtakuwa kama MUNGU, hivyo basi kula na umpe Mumeo naye ale, Hawa akafanya kama alivyosema (shetani), na akamuhubiria mumewe. Mara wakafumbuliwa macho (Mwanzo 3:7). Walitambua kuwa wamekuwa wadhambi, na kwamba walikuwa wamedanganywa. Utawala wa dunia sasa ni mali ya Shetani badala yao, na hakuna kitu tena ila kuwa na imani katika kifo cha baadaye cha KRISTO na ufufuo vinaweza kuwarejesha kwa MUNGU.

Awali, MUNGU aliwabariki Adamu na Hawa kuliko viumbe wote. Akawapa mamlaka juu ya ulimwengu wote, kila kiumbe hai. Mwanzo 1:28 inatuambia kuwa MUNGU akawaambia, “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha: Na mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” Adam na Hawa walikuwa watawala wa dunia nzima na kila kitu ndani yake. Mara Shetani alipowadanganya, dunia nzima ikaingia dhambini chini ya utawala wa ibilisi, hivyo MUNGU akapanga kuukomboa ulimwengu kwa kushuka duniani kama mwanadamu.6 MUNGU akawa Mwana wa Mtu. Alijikana NAFSI YAKE kwa ajili yetu, hadi mauti ya NAFSI YAKE pale msalabani, ikifuatiwa na ufufuo na kupaa KWAKE kwenda Mbinguni.7

Yohana 3:16 inasema, “Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa MWANAWE wa pekee, ili kila mtu amwaminiye [si Shetani wala mwingine awaye yote] asipotee bali awe na uzima wa milele.” Kuwa na maisha ya uzima wa milele inawezekana tu kama KRISTO, ambaye ni MUNGU, Njia, Kweli, na Uzima, anadumu ndani yako kama maisha yako (Yohana 14:6).8 Huwezi kuwa na uzima wa milele kirahisi kwa kusali sala ya wadhambi. Lazima uwe mwanafunzi pia. BWANA anatuamuru kujitwika msalaba wetu na kumfuata YEYE (Luka 9:23-25).9 Kuwa na uzima wa milele, hatuwezi kamwe kushuka toka msalabani.10 Kwa maneno mengine hatuwezi kutenda dhambi tena.

Shetani ni adui aliyeshindwa.11 Hapo mwanzo, ilionekana kana kwamba shetani alikuwa na mamlaka duniani milele. Lakini leo, kama tukimtii KRISTO na kumkataa Shetani, serikali yake ya dunia-moja, na makanisa yake ya ibada za kishetani yanayoongozwa na shetani, mamlaka itakuwa kwetu katika KRISTO.12

Jaribio la pili la mwanadamu kumpindua MUNGU na utawala WAKE Mbinguni lilikuwa katika Babeli. Halikufanikiwa, bila shaka. Mwanzo 11:1-9 inazaa kumbukumbu kwamba “Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi ya tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko. Wakaambiana, Haya na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.

“BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao [kama Democrats na Republicans (vyama vya siasa vya Marekani) wasivyoelewana leo, kwa hiyo hakuna la maana linalokamilishwa]. Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.”

Jaribio la Shetani la tatu na la mwisho kujaribu kumpindua MUNGU na ufalme WAKE linatokea katika nyakati hizi za sasa. Baadhi ya watu wanasema uongo kwamba UFO wanaowaona wanatoka kwenye sayari nyingine, lakini huu ni uongo. UFO hawatoki sayari nyingine; wanatoka Mbinguni. Sababu natambua hili ni kwa sababu wakati mimi na Susie tulipokuwa tunakwenda Las Vegas kufunga ndoa, tulikuwa kwenye barabara kuu kati ya Los Angeles na Las Vegas usiku sana. Ilikuwa giza wakati Susie, ambaye alikuwa akiendesha gari, alipochukua mkono wangu wa kushoto na akaniambia, “Tony, hebu tumuombe MUNGU na tumuulize ikiwa kuna UFO, tunataka kuwaona.” Ni hakika kwamba viumbe kutoka sayari nyingine wasingeweza kusikia sala zetu kwa MUNGU, wala wasingeweza kujibu sala tulizokuwa tukifanya kwa MUNGU. Ghafla, jeshi la UFO likapaa moja kwa moja kwenye kioo cha mbele cha gari letu. Walisogea karibu mno kiasi ambacho nilidhani watatugonga. MUNGU alijibu sala zetu mara moja. MUNGU alipojibu maombi yetu haraka, imani yangu kwa MUNGU na kujibu KWAKE maombi iliimarika.

Ndege zifananazo na magurudumu zimetajwa mara kadhaa katika Biblia.13 Ni majeshi ya MUNGU ya kifalme ya malaika yakichunguza uovu wa dunia ya leo kabla MUNGU hajakomesha uovu ulio juu ya nchi KRISTO anaporudi. MUNGU huwatuma Malaika katika kipindi hiki cha wakati wa taabu (nasi tuko taabani). Malaika wanatoa taarifa kwa MUNGU, kisha MUNGU huwatuma malaika waharibuo ili kuangamiza maeneo fulani yaliyo maovu katika nchi.14 YEYE huangamiza kwa tauni (ambayo ni magonjwa), njaa, mafuriko, matetemeko ya ardhi, vimbunga, na nyingine nyingi.

Sehemu kubwa ya watu duniani wanaamini kwamba wanadamu watamshinda MUNGU akili. Wamesahau siku za nyuma, ambapo MUNGU alihatarisha majaribio yao. Shetani alimwambia Hawa kwamba hamtakufa, bali “mtakuwa kama miungu.” Lakini alidanganya. Tunatambua hili kwa sababu Hawa na mumewe wote walikufa. Pia, Nimrodi na idadi kubwa ya watu duniani hawakuweza kukamilisha mnara wao, wala hawakujenga Jiji lao Mbinguni. Haikufanikiwa kutokea.

Tena, idadi kubwa ya watu duniani imetumia mabilioni ya dola, na iko tayari kutumia trilioni za dola zaidi, kuhamisha idadi kubwa ya watu kwenda kwenye sayari nyingine, sayari nyingine ambayo wanadhani ina sifa zote za dunia. Lakini hakuna sayari yoyote yenye sifa hizo. Ulimwengu uliodanganyika unasubiri kwa shauku kuu kuona upumbavu huu ukitokea. Wameamini mafundisho ya uongo ya serikali moja ya dunia na kanisa la mapepo, vyote vikiongozwa na Shetani, ambaye Mungu alisema kuwa atadanganya dunia nzima katika siku hizi za mwisho (Ufunuo 12:9).  MUNGU alisema kuwa Kanisa moja la dunia la Shetani, ambalo linaendesha serikali moja-ya-dunia ya shetani, litakuwa katika mji wa vilima saba (bila shaka hii ni Roma, Vatican, Umoja wa Mataifa).15 Kama hutambui kuwa Vatican ni mji, unachohitaji kufanya ni kwenda kwenye shirika la usafiri na kuulizia tiketi kwenda mji wa vilima saba. Watakupa tiketi ya Roma, Italia. Tena, hii ni Roma hasa ambayo kishetani inaendesha Umoja wa Mataifa, ambao ni serikali moja ya dunia. Pia inaitwa “New World Order(Mpango Mpya wa Dunia) na “kiti cha shetani” (Ufunuo 2:13). NENO LA MUNGU, kupitia Malaika mwenye mapigo saba na Malaika wengine, punde watakuja kuiharibu dunia (na waovu wote).16

Ufunuo 17:1-6, 8 inasema, “Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba [Vitasa hivi vimejaa mapigo saba ya mwisho yaliyobebwa na UFO, ambavyo kwa kweli ni IFO, vitu vipaavyo vinavyotambulika. Tunaweza kuvitambua IFO kwa kumjua MUNGU na NENO LAKE. MUNGU ni NENO (Yohana 1:1, Ufunuo 19:13).], akanena nami [Malaika huyu alinena nami, Yohana], akisema, njoo huku; Nitakuonyesha hukumu ya Yule kahaba mkuu [Kanisa Katoliki, Vatican] aketiye juu ya maji mengi [mataifa yote ya dunia]: Ambaye wafalme wa nchi [wakuu wote wa serikali, pamoja na majaji wa Vatican na waendesha mashitaka wa Vatican] wamezini naye [kila dhambi mbaya na mateso na mashitaka ya wasio na hatia (watu wa MUNGU)], nao wakaao katika nchi wamelewa kwa mvinyo wa uasherati wake. [Hii inamaanisha kuwa kile wakiitacho usahihi wa kisiasa (kama ndoa za jinsia-moja, ushoga), wapinga-Uyahudi, wapinga-Ukristo, kiu-ya-damu, mauaji, wizi na kila kitu kiendacho kinyume na MUNGU na NENO LAKE.]

“Akanichukua [Yohana] katika ROHO hata jangwani [Ulimwenguni]: nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana [Mwanamke ni Vatican, dini-moja ya dunia, na mnyama mwekundu ni Umoja wa Mataifa, ambalo ni gari la Vatican. Linalombeba sehemu mbalimbali ili aweze (mwanamke) kuharibu kazi na watu wa MUNGU kwa Sheria zake za Kanoni. Mwenye] kujaa majina ya makufuru [kama mtu mwenye pepo akichomwa na neno la Mungu, Vatican na serikali moja ya dunia inasema ni uhalifu kumtaja MUNGU katika shule za umma, vyumba vya mahakama, viwanja vya siasa, makumbusho, na maeneo mengine ya kimkakati duniani. Na kwa sababu viongozi wengi katika Kanisa Katoliki ni mashoga, wameunda kanuni mpya, kwamba kupinga ushoga ni dhambi ya kikatili (uhalifu wa chuki). Kuwa na msimamo huu, ni lazima uwe umechukua Alama ya Mnyama katika paji la uso wako (Ufunuo 14:9-11). Hili ni jambo baya sana kiroho.], mwenye vichwa saba na pembe kumi [Hii inatuambia kuwa serikali-moja ya dunia imeundwa na serikali nyingi, yaani, serikali nyingi zimeungana kuwa moja. Zote zinafikiri kwa namna moja; katika hali ya upofu zote zinapokea chochote asemacho Shetani (Ufunuo 17:12-15). Ibilisi hulifanya kuwa jambo la kizalendo unapopokea kila kitu asemacho, na si la kizalendo kama hupokei kila kitu anachosema].

“Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu [hizi ni rangi za dini ya kishetani Kanisa Katoliki], amepambwa kwa dhahabu na kito cha thamani, na lulu [Fedha zote zilizokusanywa na Mamlaka ya Ndani ya Mapato kinyume cha sheria ni mali ya Vatican. Kwa uhalisia wana matrilioni ya dola za kupoteza.], naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake: [Vatican, ambayo kwa mara nyingine ni kiti cha Shetani, ni chanzo cha kila dhambi duniani, na kuzimu.] Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, LA SIRI, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI [maneno ‘yameandikwa katika kipaji cha uso wake’ kwa lugha rahisi inamaanisha akili yake imefyonzwa katika maovu yote ya kishetani].

“Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu [Vatican ya Shetani inafahamika vema kwa umwagaji wote damu duniani, ikiwa ni pamoja na utoaji mimba, maangamizi makuu (holocaust), mauaji ya kikatili ya Kihispania (Spanish Inquisition), na kila vita vilivyowahi kutokea], na kwa damu ya mashahidi wa YESU [Malaika wa BWANA alimwambia Yohana haya]: Nami nilipomwona [Vatican],…Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako.” “Mnyama ambaye alikuwako” ilikuwa Rumi kabla ya kuanguka, na leo Shetani ameifufua Rumi kwa roho yake ya kishetani, ambayo imekuwa ikitukuzwa kwa vipindi vya dhiki.

Ninapozungumzia mateso na mashitaka ambayo kanisa langu limepitia kwa kipindi cha miaka hamsini, siyazungumzii ili kulalamika au kutafuta kuonewa huruma, lakini kumwonyesha kila mtu kwa mapana ni jinsi gani ni rahisi kuvumilia maovu yote kutoka Kanisa la kishetani la Katoliki, kwa sababu MUNGU amenipa maono. Bila maono watu huangamia (Mithali 29:18). Tunapaswa kufurahi tunapoteswa kwa ajili ya YESU. Itachukua vitabu tele kukuelezea baadhi ya mateso. MUNGU aliniambia kuwa nahitaji kuwa na nguvu mara milioni 100 za kiroho kuliko mti mkubwa wa mwaloni ulioanguka nje ya kanisa langu yapata dakika 15 baada ya kuuambia mkutano kile BWANA alichoniambia.17

“Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. Furahini siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo” (Luka 6:22-23).

Nawaambieni mbele za MUNGU na wakaazi wote wa dunia kwamba vile watu waviitavyo UFO havitoki kwenye sayari nyingine, lakini ni Malaika wa Mbinguni. Natoa ahadi ya roho yangu katika hili. Wanaokuambia vinginevyo ni wafuasi wa Shetani waliodanganyika, sawa na Hawa, watu wa Babeli, na Umoja wa Mataifa, na watakupeleka Jehannamu pamoja nao. Ubinadamu hauwezi na kamwe hautachukua nafasi ya MUNGU. Ubinadamu umeshindwa tangu zamani, na utashindwa daima.

YESU KRISTO ni NENO la MUNGU. Amini katika NENO la MUNGU (katika YESU KRISTO), nawe utaokoka (Matendo 16:31). Kumkubali KRISTO, NENO LA MUNGU, sali sala hii:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Hatimiliki Agosti 2014, 2015 Haki zote zimehifadhiwa Mchungaji wa Dunia Tony Alamo ® Imesajiliwa Agosti 2014, 2015
SWAHILI—VOLUME 20100—THREE UNSUCCESSFUL ATTEMPTS TO OVERTHROW GOD


footnotes:

1. Zab. 9:17, Isa. 5:11-15, 33:10-14, 66:24, Mat. 3:12, 5:29, 7:13, 8:11-12, 10:28, 13:38-42, 47-50, 18:6-9, 22:8-13, 25:31, 41-46, Mk. 9:42-48, Lk. 3:17, 16:19-26, 2 The. 1:7-9, 2 Pet. 2:1-9, Yud. 5-7, Ufu. 14:9-11, 19:20, 20:15, 21:8, 27 return

2. Ufu. 13:1-8, 14:8-11, 17:1-15, 18:1-8 return

3. Mwa. 3:1-6, Isa. 14:9-17, Mat. 24:11-12, 24, 2 Kor. 4:3-4, 11:13-15, 2 The. 2:3-12, 2 Tim. 3:13, Ufu. 13:1-8, 11-18, 16:13-14, 17:1-2, 8, 18:2-3, 23 17:8, 19:19-21, 20:1-3, 7-10 return

4. Rum. 5:12-21, 1 Kor. 15:20-22 return

5. Mat. 20:28, 26:28, Yn. 1:29, 3:14-17, 6:51, 10:11-18, 11:49-52, Mdo. 5:30-31, 20:28, 26:23, Rum. 5:6-11, 1 Kor. 15:3-4, Gal. 1:3-4, 2:20, 4:4-5, Efe. 5:2, 1 Thes. 1:10, 5:9-10, 1 Tim. 2:5-6, Tit. 2:13-14, Ebr. 2:9-10 return

6. Yn. 1:4-13, 12:46, Rum. 5:6-21, Gal. 4:4-5, Ebr. 2:14-18 return

7. Mat. 16:21, 20:17-19, 26:31-57, 28:1-10, 16-20, Mk. 10:32-34, Lk. 9:23, Yn. 10:7-18, Mdo. 1:1-11, Gal. 2:20, Fil. 2:5-11, Ebr. 12:1-3, 1 Yn. 3:16 return

8. Eze. 36:27, Yn. 14:15-20, 23, 26, 15:3-7, 17:21-23, 26, Rum. 8:10-11, 12:1-2, 1 Kor. 3:9, 16-17, 2 Kor. 6:16-18, Gal. 2:20, Efe. 2:10-22, 3:16-21, Flp. 2:13, Kol. 1:27-29, 2 Tim. 1:14, 1 Yn. 3:24, 4:4, Ufu. 3:19-21 return

9. Mat. 16:24-26, Mk. 10:17-30, Lk. 9:59-62, 14:26-27, 33, Yn. 12:24-26, Rum. 8:1-14, 35-37, 12:1-2, 1 Kor. 9:26-27, 2 Kor. 5:9-21, 6:1-10, Gal. 5:16-17, 24, Flp. 3:7-9, Kol. 3:5-17, 2 Tim. 2:4, Tit. 2:12, Ebr. 11:8-26, 1 Pet. 4:1-2, Ufu. 12:10-11 return

10. Mat. 10:22, 24:13, Mdo. 14:22, Rum. 11:22, Kol. 1:22-23, 1 Tim. 4:16, 2 Tim. 2:1-3, 3:13-17, 4:5, Yak. 2:17-26, 5:10-11, 1 Yn. 2:24-25 return

11. Isa. 14: 9-20, Eze. 28:11-19, Yn. 12:31, 2 The. 2:3-10, Ebr. 2:14, 1 Yn. 2:13-14, 3:8, 4:4, Ufu. 1:18, 12:3-4, 9-12, 20:1-3, 7-10 return

12. 2 Kor. 6:14-18, Ufu. 18:1-5 return

13. Zab. 68:17, Eze. 1:1-24, 3:12-13, kifu. 10, 11:14-25, Dan. 7:7-9 return

14. Mwa. 19:1-25, 2 Sam. 24:1-17, 2 Fal. 19:35, 2 Nya. 32:19-22, Zab. 78:49, Mat. 13:41-42, Mdo. 12:23, 2 The. 1:7-9, Ufu. kifu. 8, 9:1-5, 13-15, 14:8-11, 15-20, 15:1, kifu. 16, 18:1-2, 21, 19:17-21, 20:1-3, 21:9 return

15. Dan. 2:40, 7:19-25, Ufu. 13:1-8, 14:8, kifu. 17, 18 return

16. Ufu. 8:7-12, 9:1-11, 15, 14:14-20, 16:2-4, 8-12, 17-21 return

17. Soma “The Tree,” Toleo. 6500, “The Most Powerful Position in the Whole Universe,” Toleo la. 19700 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return