JE! MALAIKA WANA JINSIA?

na Tony Alamo

“Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa MUNGU [Malaika wa MUNGU hawakuwahi kuitwa ‘wana wa MUNGU.’ Wana wa MUNGU ni wale waaminio katika NENO la MUNGU (KRISTO). Kirai hiki kimemaanisha wana wa Sethi. Sethi alimwamini MUNGU kama alivyofanya Habili.1] waliwaona hao binti za wanadamu [hao binti walikua wa uzao wa kaini, mwana wa Adamu ambaye hakumcha MUNGU] ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wowote waliowachagua” (Mwanzo 6:1-2). MUNGU amewakataza watoto wa MUNGU kuoa watoto waovu, watoto wa ufisadi.2

Malaika hawana viungo vya uzazi.3 YESU alisema hivyo katika Marko 12:25. Na MUNGU kamwe, hawaiti malaika “wana.”

“Kwa maana [MUNGU] alimwambia malaika yupi WAKATI WOWOTE, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake BABA, Na yeye atakuwa kwangu mwana? Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza [Anasema “wa kwanza” akimaanisha kwa kuasili, watakuwepo wengi wengine – sisi] ulimwenguni, Asema [MUNGU], Na wamsujudu [YESU, MWANAWE wa pekee] malaika wote wa MUNGU. Na kwa habari za malaika ASEMA, Afanyaye malaika ZAKE kuwa pepo, na watumishi WAKE kuwa miali ya moto. Lakini kwa habari za MWANA Asema, Kiti CHAKO cha enzi, ee MUNGU, ni cha milele na milele: Na fimbo ya ufalme WAKO ni fimbo ya adili... Je! Yuko malaika [MUNGU] Aliyemwambia wakati wowote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako? Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu [sisi, kama wana wa kupanga wa MUNGU] wale watakaourithi wokovu?” (Waebrania 1:5-8, 13-14).

Sasa, tukirejea “malaika hawana viungo vya uzazi” – unapaswa kufahamu kwamba tutakapofika Mbinguni, hata sisi hatutakuwa navyo. Sababu ya mimi kufundisha hili ni ili uweze kuwatambua waalimu wa uongo wanaosema kuwa malaika waliingiliana na binti za wanadamu, na kuzalisha majitu. Tena, MUNGU hawaiti malaika “wana.” Haya ni mafundisho ya uongo.

Wakorintho wa pili 6:14-18 inatuambia, “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya KRISTO na Beliari [Belizebabu, ibilisi]? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu [sisi] la MUNGU na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la MUNGU aliye hai; kama MUNGU alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa MUNGU wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa BABA kwenu, nanyi mtakuwa Kwangu wanangu wa kiume na wa kike [siyo malaika], asema BWANA MWENYEZI.”4

“Nao Wanefili (majitu) walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo [baada ya siku hizo, hata leo], wana wa MUNGU [siyo malaika – tena, wana wa Sethi, mbadala wa Habili, Mtu wa Mungu] walipoingia kwa binti za binadamu [waovu], wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari [hodari katika mambo ya kimwili] zamani, watu wenye sifa [kama wapiga miereka, masumbwi, wanyanyua vitu vizito, si Wacha Mungu]. BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu [siyo malaika, au nusu-watu, nusu-malaika] ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote” (Mwanzo 6:4-5)

YESU ameweka wazi kwamba malaika hawaoi malaika (wala hawaoi wanadamu). Kule Mbinguni si sisi wala malaika watakaokuwa na viungo vya uzazi, au tamaa yoyote ya ngono. Uwepo wa ROHO MTAKATIFU una nguvu namna ambayo daima tutakuwa katika hali ya furaha kuu.

Marko 12:18-25 inasema, “Kisha Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiama (ufufuo), wakamwendea [YESU], wakamwuliza na kusema, Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mkewe wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mkewe [hata kama anaye mke mwingine] akampatie ndugu yake mzao.5 Basi kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao. Wa pili naye akamtwaa akafa, wala yeye hakuacha mzao. Na wa tatu kadhalika; hata na wote saba, wasiache mzao. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. Basi, katika kiama (ufufuo) atakuwa mke wa yupi katika hao? Maana wote saba walikuwa naye. YESU akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uwezo wa MUNGU? Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.” Hawatendi vitendo vya ngono, hawawezi.

Hivyo basi, Mbinguni, si sisi wala malaika watakaokuwa na viungo vya uzazi (maungo yasiyovutia). MUNGU alipowaumba malaika, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa na viungo vya uzazi, hivyo hawajawahi kuingiliana na malaika au binti za wanadamu. Mafundisho haya ya uongo ni uovu mkuu. Ni ya kipepo mno!! Biblia inasema Hawa ni mama wa wote wenye mwili na Adam ni baba.6 Kama watu wanaongozwa kuamini mafundisho haya ya uongo, wanaweza kuamini kwamba wanadamu wote hawatoki kwa Adamu na Hawa. Wanaweza kudhani kwamba hawana asili ya dhambi ya Adamu na hawamuhitaji KRISTO.7 Hata hivyo, baadhi ya watu ni wendawazimu na wamepagawa na roho chafu za ngono ambazo huharibu roho za watu hawa. Roho hizi zinaweza kupotosha roho ambazo hazichukui, nguvu na mamlaka ya YESU juu yao.8 Sulemani katika umri wake wa uzee, alisukumwa na wanawake waovu, ambao, bila shaka hawakuwa waumini katika MUNGU.9

Soma Biblia. Soma kwa bidii ili uwe mfanyakazi aliyekubaliwa na MUNGU.10 Hata hivyo, ni sharti umpokee KRISTO kwanza ili ROHO wa KRISTO na BABA YAKE kwa ROHO wawe ndani yako kukupa nguvu ya kushindana na majaribu na kubaki imara katika BWANA mpaka mwisho. Anza sasa kwa kumwomba MUNGU kwa sala hii:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

Hatimiliki, Novemba 2015 Haki zote zimehifadhiwa Mchungaji wa Ulimwengu Tony Alamo Imesajiliwa Novemba 2015
SWAHILI—VOLUME 22400—DO ANGELS HAVE SEX?


footnotes:

1. Mwa. 4:25-26 return

2. Kut. 34:12-16, Law. 20:26, Kumb. 7:1-6, Ezra 9:1-2, 10-15, 10:10-11, Neh. 13:23-27, Mal. 2:11, 1 Kor. 7:39, 2 Kor. 6:14-18, Efe. 5:11 return

3. Mat. 22:29-30, Mk. 12:24-25, Lk. 20:34-36 return

4. Yer. 31:31-34, 1 Kor. 6:19-20, Efe. 2:21-22, Tito 2:11-14, Ebr. 8:8-12 return

5. Mwa. 38:8-11, Kumb. 25:5-6, Rut. 4:5, 10, Mat. 22:24 return

6. Mwa. 3:20, 4:1-2, 25-26, 5:3-4, Kumb. 32:8, Isa. 43:27, Mal. 2:10, Mdo. 17:25-26 return

7. Yoh. 3:16, 36, 10:7-11, 14:6, Rum. 3:23, 5:12-19, 11:32, 1 Kor. 15:21-22, Gal. 3:22, Filp. 2:8-11, Ebr. 2:9 return

8. Lk. 9:1-2, Yoh. 14:12, 16:33, Mdo. 1:8, 1 Thes. 1:5, 2 Tim. 1:9, 1 Yoh. 4:4 return

9. 1 Fal. 11:1-11, Neh. 13:23-27 return

10. Yosh. 1:8, Mat. 4:4, Yoh. 8:31-32, Efe. 6:11-17, Kol. 3:16, 2 Thes. 2:15, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, 1 Pet. 2:2 return


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return