Ushuhuda wa Uponyaji

na Tony Alamo

Oktoba 27, 2014
Jina langu ni Mchungaji Isaque Roberto. Natoka Londrina katika Jimbo la Paraná, Brazil, na Ningependa kuwashirikisha jambo kupitia barua pepe hii. Nimekuwa mchungaji Londrina kwa miaka 15. Miaka mitatu iliyopita familia yangu ilihuzunishwa na maafa ambayo yalibadilika kuwa tukio kubwa.

Tarehe 24 Julai, 2011, binti yetu Beatriz Gabriela (akiwa na umri wa miaka saba), alipata ajali mbaya barabarani alipogongwa na dereva wa teksi alipokuwa akitembea kwenye kivukio cha wapita njia. Athari ya ajali ilikuwa kubwa kiasi ambacho, kwa mujibu wa wakaguzi, alitupwa mbali takribani futi 21. Nilikwenda mbio upande alipokuwa, alikua hana pumzi, na nakumbuka nikipiga mayowe, “Mtu yeyote aniitie msaada!” Nilipomtazama tena, niliona gurudumu la pikipiki na sauti iliyosema, “Nitasaidia. Mimi ni mzima moto.” Kwa wakati ule, Mungu alitoa jibu la kwanza pale. Alimlaza Beatriz kifudifudi na kujaribu kumrudishia fahamu, akakohoa damu. Msaada uliwasili, na walipokuwa wakimshughulikia ndani ya gari la wagonjwa, nikaanza kuomba. Ibilisi naye alikuwa akikabiliana nami huku akinionyesha akilini taswira ya mvulana niliyemfahamu ambaye aligongwa na gari akapoteza uwezo wa kuongea na uratibu wake. Kwa sasa familia yake wanambeba kwenye kiti cha magurudumu. Kwa wakati ule, ibilisi alikuwa akiniletea taswira yake akisema, “Hivyo ndivyo binti yako atakavyokuwa.” 

Beatriz alipelekwa hospitali na kulazwa akiwa na vipimo vifuatavyo: amevunjika mguu wa kushoto, amevunjika mkono wa kushoto,  amevunjika mtulinga wa kulia na kushoto, bandama imekatwa sana, mapafu yameharibika na jeraha la kichwa la ngazi ya 3 (ngazi ya 4 ni kifo).

Tulipofika kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi, tulimwona binti wetu akiwa ameunganishwa na vifaa kadhaa, akipumulia mashine, na akiwa amezimia. Siku tatu baada ya ajali, Julai 27, daktari wa upasuaji wa akili aliyekuwa akimhudumia alituita na kusema, “Sina habari njema. Hali yake imezidi kuwa mbaya zaidi. Beatriz hasaidiki na dawa alizopatiwa, na amepata uvimbe kwenye ubongo. Kutokana na hali hiyo, damu haizunguki kupita kwenye ubongo, na ndani ya saa chache zijazo ubongo wa Beatriz utakuwa umekufa.” Daktari alisema, “Nina mbadala, ambao ni kufanya upasuaji kuondoa kipande cha fuvu kila upande ili kupunguza shinikizo kwenye ubongo wa Beatriz, hivyo utakuwa na nafasi ya kutanuka. Hata hivyo, hakuna uhakika kwamba hali yake itabadilika au anaweza kuhimili upasuaji.”

Tuliidhinisha upasuaji, kwa sababu tulijua kwamba neno la mwisho lilikuwa ni la Mungu. Walipokuwa wameandaa kila kitu tayari, walituambia tukae na Beatriz ili tuweze kumuaga. Mke wangu alianza kuomba nilipokuwa nikiwaita waombaji wengine na kuwaelezea hali halisi. Mke wangu alipokuwa mbele ya Beatriz akiomba, mtu mmoja alimjia na kusema, “Mama, nakushauri umwombee Mungu amchukue, kwa sababu kama akifanikiwa kuishi, atakuwa tu mtu wa kulala kitandani.” Saa chache baadaye, bila kujua kilichotokea, nilipokea ujumbe kwenye simu yangu kutoka kwa shemeji yangu (wa-kike) ambaye alisema alikuwa akiomba wakati wa mchana na alipata maono. Aliona pepo wabaya wakimjia mke wangu na kusema maneno yale yale.

Upasuaji ulidumu kwa takribani saa tano. Walipomleta Beatriz kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, kichwa chake chote kilikuwa kimefungwa bendeji na uso wake ulikuwa umeharibika. Sasa ikawa ni kusubiri tu. Tulimwomba Mungu amponye, lakini habari mbaya ziliendelea kuja – nimonia,  maambukizi ya hospitali.

Siku moja kabla ya siku ya kuzaliwa ya Beatriz (Agosti 8), daktari alisema angemtoa kwenye kitulizo kuona kama angeweza kuzinduka kutoka kwenye hali ya kuzimia. Niliuliza, “Unadhani itamchukua muda gani kuamka?”

“Hakuna namna naweza kujua kwa hakika,” alisema. “Anaweza kuamka leo, kesho, wiki ijayo, mwezi ujao, mwakani, lakini pia anaweza asiamke tena,” alihitimisha.

Siku chache baadaye, vifaa vya msaada wa kupumua viliondolewa.  Tulianza kushereheka kwa sababu alianza kuamka. Hata hivyo, wakati wa usiku Beatriz alikua amemeza mate yake wakati akipumua. Tulipofika hospitali, tulimwona akiwa anapumua kwa shida sana. Timu ya matibabu walikuwa wakifanya yote waliyoweza kumrejesha katika hali nzuri zaidi. Tulitoka kwenda kupata chakula cha mchana, na tuliporudi na kuomba kuingia ndani, tulizuiliwa. Nilichungulia kupitia kwenye mlango na nikaona karibia timu nzima ilikuwa imezunguka kitanda chake ikiwa inalia. Ilitubidi tusubiri dakika kadhaa, na tuliporuhusiwa kuingia ndani, tuliona kwa mara nyingine Beatriz amewekewa bomba la kupumulia. Mmoja wa madaktari alisema, “Imetubidi kumwekea bomba la pumzi, na Beatriz atatakiwa kuvuta oksijeni yake kwa kutumia bomba. Hakuwa na uwezo wa kuvuta pumzi yake mwenyewe.” Habari mbaya zaidi – sababu nyingine ya kuomba. Siku kadhaa baadaye, Beatriz alizinduka kutoka kwenye hali yake ya kuzimia na akapelekwa sehemu ya wagonjwa.

Tuliendelea kumlilia Mungu na kufunga muda wote. Wakati Beatriz alipokuwa sehemu ya wagonjwa, tulibadili chumba kile kuwa kituo cha maombi, saa 24 kwa siku. Tulikuwa na nyimbo za kuabudu zikicheza. Tuliomba kila saa. Watu waliingia ndani na kumwona Beatriz akiwa amelala kitandani miguu yake ikiwa imefungwa bendeji, amefungwa mashine za kupumulia na za kulishia na wakasema, “Pawezaje kuwa na imani kiasi hiki  mahali hapa?” Kwa pamoja kulikuwa na siku 53 za kulazwa hospitali.

Wakati Beatriz aliporuhusiwa, alifika nyumbani bila kuonyesha dalili yoyote ya  kupata nguvu tena. Tulikuwa na kitanda cha hospitali, kiti cha kuogea, na kiti cha gurudumu nyumbani. Mke wangu alikuwa akizungumza na mtaalamu wa mazoezi ya viungo na kumuuliza, “Daktari, unadhani itachukua muda gani Beatriz kuweza kutembea?” Daktari akajibu, “Kwa miaka ambayo nimehudumu katika udaktari, sijawahi kuona katika maandishi yoyote ya kitabibu au kusikia habari yoyote ya mtu yeyote aliyewahi kupona kwenye ajali kama aliyopata Beatriz. Labda siku moja anaweza kutembea kwa kutumia magongo au mtu wa kumshika akitembea, lakini kuweza kutembea tena kawaida – kwa maoni yangu – kamwe haiwezekani tena.” Hata hivyo, tulidhamiria katika roho zetu kwamba asiishie katika hali hiyo. Imara tuliendelea kumtafuta Bwana, wakati mwingine katika imani, wakati mwingine tukilia, lakini mara zote tuliamini. Siku moja tulimchukua kwenye kliniki ya jamii kwa sababu tulihitaji rufaa, na nilimwambia daktari kwamba ilikuwa ni jambo la haraka. Daktari aliomba kumwona Beatriz, na nilipotembea kuingia ofisini nikiwa nimembeba mikononi mwangu, daktari aliuliza, “Bw., kwa nini una haraka kiasi hicho? Nini kinaweza kubadilika katika hali ya mtoto huyu?”

Beatriz alilazimika kufanyiwa upasuaji kuwekewa chombo bandia mahali mfupa wa fuvu uliondolewa. Tulipata makisio ya (Real za Kibrazili) $147,500.00 (karibia $60,000.00 Dola za marekani). Hatukuwa na pesa, hivyo tulikuwa na sababu nyingine ya kuomba. Tukiwa tumepokea maelekezo kutoka kwa Mungu kupitia rafiki, tulianza kampeni ya kupata pesa. Siku ya Alhamisi, nilipokea simu. Alikuwa ni mwanamke aliyeanza kuuliza maswali kuhusu Beatriz. Aliuliza ni kiasi gani tulichohitaji bado, nami nikasema (BRL) $57,000.00 (23,000.00 Dola za marekani). Alisema kwamba ataangalia kama anaweza  kutusaidia. Jumatatu iliyofuata, nilipokwenda benki kuangalia salio, niligundua kwamba mtu yule alikuwa ameweka kiasi cha fedha tulichokuwa tunahitaji. Ndani ya siku 40 tuliweza kupata kila sarafu tuliyokuwa tunahitaji. Bwana Asifiwe!

Upasuaji ulifanyika tarehe 23 Desemba, 2011. Kwa wakati huo, Beatriz tayari alikuwa anaweza kukaa kwa msaada wa mito na aliweza kukaa kwenye kiti cha magurudumu. Tarehe 27, Desemba nilikwenda kusema kwaheri kwa Beatriz kabla ya kuondoka kwenda kanisani. Nilishika mikono yake na kumwambia kwamba nilikuwa nakwenda kanisani. Mara nikamsikia akivuta mikono yangu. Nilimshika kwa nguvu na mara ya kwanza akasimama. Niliogopa na nikarudi hatua nyuma, na kwa wakati huo huo, alipiga hatua moja mbele na akaendelea kutembea. Mungu ni mwaminifu!
Siku zilivyosonga mbele, Beatriz aliendelea kurejeza uwezo wake. Alianza kuongea na kuandika. Katika mwezi Mei 2012, alirudi shuleni.

Leo, miaka mitatu baadaye, yeye ni ushuhuda hai wa muujiza, usioweza kueleweka, uthibitisho kwamba Mungu ni mwaminifu kwa Neno Lake na anawajibu vyema wale wote wanaoamini. Neno ambalo ninalo kwa ajili ya maisha yako wakati wote ni, “KILA JAMBO LINAWEZEKANA KWAKE AAMINIYE” (Marko 9:23).

Siku chache zilizopita, mke wangu alikuwa na mtaalamu wa mazoezi ya viungo, na daktari alikuwa akimwonyesha Beatriz kwa mmoja wa wanafunzi wake na akasema, “Huu ni muujiza, kwa sababu kama isingalikuwa Mungu, asingekuwa (Beatriz) hapa. Hapakuwa na dawa ya kuweza kumponya.”

Dawa haikuweza kufanya chochote, lakini MUNGU ANAWEZA! ANAWEZA KUFANYA KAZI MAISHANI MWAKO PIA!
Mchungaji Isaque Roberto

Ushuhuda huu umeshirikishwa na kanisa zima katika Londrina na umekuwa mfano wa nguvu ya Mungu kutupa changamoto, katika imani yetu. Tazama ushuhuda ambao tumerekodi kanisani kwenye You Tube: http://www.youtube.com/watch?v=YHqbBk0A4nA.


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.