MALKIA WA MAKAHABA

na Tony Alamo
Rosalind Musselman

Ibada ovu ya Mama Bikira mungu ya Kanisa Katoliki imejengwa juu ya msingi wa mafundisho ya uongo ya ubikira “wa kudumu wa Maria.” Maria, mama wa Yesu, aliinuliwa na mfumo wa kisiasa wa Kikatoliki wa Kirumi kuwa mungu wa kike ambaye ni Bikira Maria asiye wa kweli, lakini Biblia inathibitisha Maria hakuwa bikira wa kudumu wala mungu mwanamke (goddess).

Tukifuatisha kutoka huko nyuma, mwanzo wa mafundisho haya ya uongo, utatambua asili ya kweli ya uovu wa ibada ya Maria na utaelewa uendelezaji wake wa kishetani. Kwa kutazama mbele katika unabii wa Biblia, utaona mafundisho haya ya uongo kuwa ni muhimu sana katika kufunua “Fumbo” la siri la  Babeli lililosemwa katika Ufunuo 17. Msingi wake wa kale ni ibada ya mungu mwanamke ambayo kupitia kwayo upapa unachukua nafasi kubwa.

Jinsi tutakavyoendelea, utaona kwa nini ni muhimu kuwa Rumi inayang’ang’ania makufuru haya, mafundisho ya uongo ili kutoa ilani ya mifumo ya kisiasa ya kidini ya nyakati za mwisho ambayo kupitia kwayo Mpinga Kristo atakuwa na mamlaka juu ya dunia yote kwa muda mfupi.

Ili kufunua fedheha hii, msingi wa uongo, hebu tuangalie ukweli wa Neno lenye uhakika la Mungu. Biblia inasema dhahiri kwamba Maria alikuwa na watoto wengine. Ndugu wanne wa Yesu wanatajwa kwa majina. Yesu pia alikuwa na maumbu/dada wapatao wawili. Majina yao hayakutajwa, lakini katika wingi, “maumbu yake,” imejumuishwa katika maandiko yafuatayo:

“Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo na Yusufu, na Simoni, na Yuda? Na maumbu yake wote hawapo hapa petu?” (Mathayo sura ya 13, mstari wa 55-56)

“Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake” (Marko sura ya 6, mstari wa 3).
Biblia inamuita Yesu “mwana mzaliwa wa kwanza” wa Mariamu. Hakuna mahali popote katika Neno la Mungu ameitwa “mwana wa pekee wa Mariamu.” Kumbuka maandiko yafuatayo:
“Asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU” (Mathayo sura ya 1, mstari wa 25).

“Akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni” (Luka sura ya 2, mstari wa 7).
Ukweli ni kwamba [Maria] alikuwa na watoto wengine kwa sababu ya neno, “mzaliwa wa kwanza” katika Kigiriki (lugha ya awali ambayo Biblia ilikuwa imeandikwa), kama inavyotokea katika maandiko mawili hapo juu, ni prototokos. Kwa tafsiri halisi, prototokos linamaanisha, “Wa kwanza kati ya wengine wengi.”

Kama Yesu angekuwa mwana wa pekee wa Maria, neno sahihi la kigiriki lingekuwa monogenes, lenye maana, “mwana wa pekee,” “binti wa pekee,” au “mtoto wa pekee.” Monogenes linatokea mara kadhaa katika Maandiko ya Agano Jipya, ikiwa ni pamoja na yafuatayo: “Na alipokaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye” (Luka sura ya 7, mstari wa 12).

“Kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga” (Luka sura ya 8, mstari wa 42).
Neno hili, monogenes, limetumika pia kumtaja Bwana Yesu kama “Mwana wa Pekee wa Baba.”

“Naye Neno [Yesu] alifanyika mwili, akakaa kwetu; (nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba;) amejaa neema [nguvu] na kweli” (Yohana sura ya 1, mstari wa 14).

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana sura ya 3, mstari wa 16).

Karne nyingi kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, Mungu alitoa unabii katika Neno lake kwamba Masihi atakuwa na ndugu zake, na mama Yake atakuwa na watoto wengine. Maandiko yafuatayo yanasema hili wazi kabisa:

“Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu” (Zaburi 69, mstari wa 8). Katika Agano Jipya tunasoma “Basi ndugu zake wakamwambia, ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. . .Ukifanya mambo haya, basi ujidhihirishe kwa ulimwengu. Maana hata nduguze hawakumwamini” (Yohana sura ya 7, mstari wa 3-5). “Hata nduguze walipokwisha kukwea kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea” (Yohana sura ya 7, mstari wa 10).

Rumi kwa ushetani inatangaza kwamba nduguze Yesu walikuwa ni binamu zake ambaye mama yao aliitwa Maria na Klopa. Pia kwa dharau wanamwelezea Yusufu kuwa ni mzee sana kuzaa watoto na Maria, lakini alikuwa na watoto kwa ndoa yake ya awali.

Mungu alimwahidi Daudi kwamba ukoo wake utakalia kiti chake cha enzi milele (II Samweli sura ya 7, mstari wa 16). Ukoo wa kifalme ulichukuliwa kutoka kwa baba kwenda kwa mwana, si mama kwenda kwa mwana. Malaika mpashaji habari, Gabriel, alimwambia Maria yafuatayo:

“Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita YESU. Huyo atakuwa mkuu, ataitwa mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake” (Luka sura ya 1, mstari wa 31-32).

Ukweli umethibitishwa katika maneno yafuatayo ya Yesu:

“Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye shina na mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’ara ya asubuhi” (Ufunuo sura ya 22, mstari wa 16).

Akiwa kama mtoto wa kambo wa Yusufu, na mzaliwa wa kwanza katika familia, Yesu akawa mrithi wa kisheria wa kiti cha Daudi kupitia Yusufu.

Mfumo wa Kanisa Katoliki uliojaa uovu umemuinua Mama yake mungu mwanamke Bikira Maria kwenye nafasi ya juu zaidi katika viumbe kama “Mama wa Mungu.” Maria hakuwa mama wa Mungu. Alikuwa Mwebrania wa kawaida mjakazi wa Bwana, akapata upendeleo wa kuchaguliwa Naye [Bwana] kama bikira atakayebeba mimba ya Yesu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Katika kutimiza unabii, ilimpasa Kristo kuja duniani kama mwanadamu.

Yesu alikuwa pamoja na Baba kabla ya ulimwengu kuumbwa. Aliacha enzi mbinguni, akaja chini duniani, na kufa msalabani. Kama Mwana-Kondoo wa sadaka wa Mungu, alimwaga damu yake ili kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu zote. Hivyo basi, Maria hakuwa zaidi ya kitamizi, mjakazi wa kawaida wa Bwana. Hakuwa na uwezo wa kipekee, na wala hana uwezo wa kipekee hata sasa!

Katika kutunza ule ukweli wa, “uongo,” wa kisiri, ofisi ya Mama mungu mke bandia ambayo asili yake ni Babeli, Ukatoliki wa Kirumi ya kipepo umempa Maria nguvu muhimu za kiungu. Njia mbaya ilikuwa imeandaliwa. Kilichobaki kilikuwa ni kumpa [Maria] jina la Mama mungu mwanamke wa kipagani wa Babeli ya kale. Kwa mujibu wa hadithi za kale, Mama mungu mwanamke alizaa mwana wa miungu, na bado ana ubikira wa kudumu. Maria wa Kirumi ni wa ukoo wa moja kwa moja na Ishtar, yaani mungu mwanamke wa uongo wa Babeli ya kale.

Fikiria na upokee yafuatayo kutoka katika Neno la Mungu la milele:

“Nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi. Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu” (Ufunuo sura ya 17, mstari wa 3-6).

Mungu anamaanisha “mwanamke,” kwa kutumia neno la umoja, “yake [a kike].” Neno la Mungu daima linamwelezea mwanamke kiistiari likionyesha taswira ya mfumo wa kidini. Hapa tuna fununu ya utambulisho huu wa kishetani “Siri, Babeli Mkuu, Mama wa Makahaba,” ambayo si mwanamke halisi, bali mfumo wa kisiasa, na wa kidini ya uongo. 

Mfumo huu mbaya wa kisiasa wa Rumi ya Kikatoliki una msingi wake wa kidini wa ibada ya kishetani ya kumwabudu Maria (Ibada ya sanamu ya kumwabudu Bikira Maria, kumwabudu mama kuliko Mwana) imedhihirishwa wazi kama kahaba wa kale ikiwa imehusishwa na kanuni ya kisiasa ya kidini na mafumbo ya siri za Babeli. Binti zake wa kikahaba ni madhehebu yote ya kishetani ya aina zote zinazoweza kufikiriwa. Kichini-chini mengi yamepandishwa hadi kwenye ofisi za serikali, kuunda Mpango Mpya wa Dunia (New World Order) na mafumbo ya “alama elfu za nuru” (giza). Wote ambao wamepokea mafundisho yake ya kishenzi kwa muda mchache wanazawadiwa na Shetani kwa ofisi za nyadhifa kubwa na kusifiwa kwa maneno ya uongo ya kupokea “alama za nuru” kwa ajili ya kufanya matakwa yake. Viongozi hawa wa kishetani wa kitaifa na kimataifa (mabinti wa kikahaba) wanaunda serikali moja ya kanisa ya dunia, Siri ya Babeli Mkuu, wakipewa mamlaka na joka (Shetani) (Ufunuo sura ya 13, mstari wa 4).

Fumbo hili la Babeli linayadanganya madhehebu. Mungu alisema kutakuwa na anguko/ukengeufu mkuu wa makanisa katika siku za mwisho: “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji [mwisho wa dunia], usipokuja kwanza ule ukengeufu [wa makanisa/madhehebu ya kidini]; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu [kiongozi wa serikali moja ya dunia na kanisa, Mpinga Kristo]”(II Wathesalonike sura ya 2, mstari wa 3). Makanisa na serikali leo hii vimekubali machukizo, desturi za makufuru, ibada na mafundisho ya mfumo huu wa Babeli ya siri ya kale uitwao Ukatoliki. Wanapambana na wakristo wa kweli, kama mimi binafsi, kwa sababu tunaihubiri kweli. Mfumo huu wa kisiasa ambao una ujasiri wa kudanganya kuhusu Mungu Baba, Mungu Mwana, Yesu, Roho Mtakatifu, na mjakazi mdogo wa Mungu, Maria, hautaona ugumu kudanganya kuhusu hali ya dunia, mimi au Mkristo mwingine yeyote.

Dini ya kishetani ya kisiri ya Babeli ya kisiasa ya kale, iliyoanzishwa na Nimrodi na malkia wake, Semiramisi, imesambaa miongoni mwa mataifa yote. (Alikuwa Ishtar, hata hivyo, ambaye alikuwa “njozi ya uongo” Mwenye mamlaka Mama mungu mwanamke wa Babeli). Malengo ya ibada yalikuwa Baba mkuu wa Bandia, Mwanamke mwenye mwili wa kibinadamu au Malkia wa Mbinguni, na mwanawe asiye wa kiungu mwovu. Dini hii iliota ndoto kuwa ina hekima ya hali ya juu na siri nyingi za Mungu. Kulikuwa na vioja vingi, ibada za ajabu na kuungama mbele ya makasisi.  

Akiwa kama mungu (akiabudiwa au kuheshimiwa kama mungu), Nimrodi alikuja kufahamika kama Baali. Jina la mwenzake wa kike likawa Baalti. Katika lugha ya Kiswahili, linatafsirika “Mama Yangu”; kwa Kilatini, “Mea Domina”; na kwa Kiitaliano, limetafsiriwa na kufahamika kama “Madonna!”

Miongoni mwa Wafoeniki, mama mungu mke alikuwa akijulikana kama “Mama wa Bahari.” Hata jina hili kiujanja hutumika kwa Maria, ingawa hakuna uhusiano baina ya Maria halisi wa Biblia na bahari.
Kwa uongo, Maria pia huitwa “Malkia wa Mbinguni.” Cheo hiki si cha mama wa Yesu. “Malkia wa Mbinguni” kilikuwa ni cheo cha uongo cha Mama mungu mwanamke aliyekuwa akiabudiwa karne nyingi kabla Maria hajazaliwa. Tukirejea nyuma siku za Yeremia, watu walikuwa wakimwabudu bure “Malkia wa Mbinguni” wa bandia na kufanya ibada za kiovu kwa heshima yake. Tazama unabii ufuatao wa jambo hili kutoka kwenye Biblia:

“Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni...” (Yeremia sura ya 7, mstari wa 18).

Lakini Mungu anasema nini? Mungu asema “Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu” (Isaya sura ya 45, mstari wa 5).

Kuabudu na kutukuza sanamu, watakatifu na masalio, maungamo ya kibinafsi, ishara ya msalaba, Krismasi, Siku ya Mwanamke, Kwaresima, pamoja na ibada nyingine za kipagani na sherehe kwa utaratibu zilichukuliwa/kukubaliwa na dini ya siri ya kishetani ya Babeli ya kisiasa ya Kikatoliki (sasa ni mkuu wa serikali moja ya dunia na kanisa). Mafundisho hayo, kwa mujibu wa Neno la Mungu, ni wendawazimu. Kama unashangaa ni kwa nini “mfumo” katika dunia hii unayoishi ni “shaghalabaghala” ni kwa sababu mfumo huu wa wendawazimu kwa kasi unachukua nafasi ya ule ulio mkamilifu, maelekezo yenye maana ya Mwenyezi, Mtakatifu, wa Milele, Mungu aliye hai. Mfumo huu wa Babeli ya kisiri wa serikali moja ya dunia unatiwa nguvu kukuambatanisha, kukukatisha tamaa na kukudanganya na kanuni na taratibu zao za dini ya kishetani. Lakini kweli ya Yesu itakuweka huru. Kuna wimbo usemao, “Shetani alikuwa amenifunga, lakini Yesu akaniweka huru, Utukufu Haleluya, Yesu ameniweka huru,” “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana sura ya 8, mstari wa 32). “Sheria ya BWANA ni kamilifu, huiburudisha nafsi” (Zaburi 19, mstari wa 7).

Wakati wa karne ya kwanza ya mfumo wa kisiasa wa Kanoni ya Kirumi, hapakuwa na msisitizo uliowekwa juu ya Maria. Haukuwepo hadi wakati wa Constantine – mapema Karne ya Nne – ambapo serikali ya kishenzi ya Kirumi ilianza kumtazama Maria kama Mama yake (Rumi), mungu mwanamke. Wanawake wa Rumi, Thrace, Uarabuni, na mahali pengine, walianza kumwabudu Maria wa Kanisa Katoliki kama mungu mwanamke halisi na kutoa sadaka za keki madhabahuni mwake. Katika muda wa miaka michache, “Ibada ya Maria” haikuwa tu imekubalika na mfumo wa kisiasa wa Katoliki, bali pia ilikuwa moja ya makufuru yake makuu. Kazi ya shetani ni kukuhadaa kwa kufanya macho yako yasimtazame Yesu na kuyaelekeza kwenye jambo lingine ambalo si mwokozi wako mmoja na wa pekee, na kufanya iwe vigumu kwako kwenda mbinguni na kuokoka kutokana na mateso ya Jehannamu ya milele. Yohana, kwa Roho Mtakatifu, alitabiri ushetani huu, mwanamke kahaba (kanisa) anayeendesha serikali zote za dunia, na wakitii kila iliyo amri yake.

Shetani alihitaji kanisa na serikali ili alazimishe kuabudiwa, kanisa lake la kishetani na serikali, na mafundisho yake mengi ya uongo. Shetani hajali ni nani au nini unaabudu, ilimradi si YESU MWOKOZI WA KWELI. Ataonyeshwa utii (kulingana na maandiko matakatifu) kwake na mafundisho yake mengi ya uongo yatakayomfanya kila mmoja kupokea alama katika mkono wake wa kuume au paji la uso (chip ya kompyuta). “Nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru” (Ufunuo sura ya 17, mstari wa 3). Na mwanamke huyu (kanisa la Shetani) atakuwa “amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu” (Ufunuo sura ya 17, mstari wa 4).

Mnamo 431 B.K., katika Baraza la Efeso (Mji wa Mama mungu mwanamke wa uongo wa kipagani Diana), mafundisho ya kishetani ya “ibada ya Maria” yalifanywa mafundisho rasmi ya uongo ya mfumo wa kisiasa wa Katoliki. Makufuru haya ya kishetani yamekua kwa haraka sana kwa nguvu hivi kwamba Maria sasa anajulikana katika mfumo wa kisiasa ya Rumi ya Kikatoliki, ambayo inaongoza serikali moja ya dunia na kanisa, kama mungu mke. Kwa makufuru anaabudiwa kuliko hata Yesu Kristo Mwenyewe! Uzoefu huu dhahiri ni mwendelezo kutoka Babeli ya kale, asili halisi ya Ukatoliki, ambapo Mama mungu mke aliabudiwa kuliko Mwana, au Baba Mkuu.

Baadhi ya mafundisho ya kutisha ya kishetani kuhusu mungu mwanamke wa uongo, Maria yalikuwa yamekumbatiwa na mfumo wa kisiasa wa Rumi ya Kikatoliki ambao kwa sasa wanauita Mpango Mpya wa Dunia (New World Order), alama elfu za nuru (giza), lakini ukweli ni kwamba hamna chochote kipya au nuru. Yesu alisema kwamba mfumo huu ulikuwa unatoka kwa “yule nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote” (Ufunuo sura ya 12, mstari wa 9).

Desemba 8, 1854, Papa Pius IX kwa aibu alitunga yafuatayo: “Mwana wa milele wa Mungu, alipotaka kuchukua mwili wa asili ya mwanadamu kwa ajili ya wokovu na utukufu wa binadamu, na akataka kwa aina fulani kujiingiza kwenye ndoa ya siri na jamii yote ya wanadamu, hakufanya hivyo kwanza bila ya kuwa na idhini ya uhuru kamili toka kwa mama Yake mteule ambaye aliwakilisha wanadamu wote.”

Thomas Aquinas alikwenda mbali zaidi na uasi huu wa kudhihaki na kupotosha: “Katika habari ya malaika Gabrieli kwa Bikira Maria atamzaa Yesu, idhini ya Bikira ilikuwa ikisubiriwa katika nafasi ya jamii yote ya wanadamu. Hakuna litakalotujia isipokuwa kwa mapenzi ya Mungu kupitia Maria. Ni kwa sababu hii kwamba hakuna awezaye kumfikia Mwana bila kupitia kwa mama: Tunaamini katika haki ya Mungu isiyo na mipaka, na tunapata hofu na kutetemeka mbele yake. Kama uelewevu wa matendo yetu unatufanya tutetemeke, tunahitaji wakili na mlinzi, ambaye ana nguvu mbele za Mungu. Ndiye Maria, anayestahili sifa zetu zote; hututazama kutoka juu katika wema kamili na kuzingatia. Kristo kwa uhuru alipenda kuwa chini yake na kumtii, hivyo sisi nasi tunapaswa kujiweka chini ya ulinzi wake na uaminifu, kwa pamoja na mipango yetu na matendo, usafi wetu na maungamo yetu, huzuni yetu na furaha, na maombi na matakwa. Yote yaliyo yetu ni lazima tuyakabidhi kwake [Maria].”

Lakini Biblia inasema tumwamini Bwana kwa moyo, roho, akili na nguvu zetu zote na “Enyi watu, mtumainini siku zote, Ifunueni mioyo yenu mbele ZAKE: Mungu ndiye kimbilio letu” (Zaburi 62, mstari wa 8). “Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake, wala hakuwaelekea wenye kiburi, wala hao wanaogeukia uongo” (Zaburi 40, mstari wa 4). Biblia pia inawaambia Wakristo kwamba kila kitu kinatoka kwa Mungu kwa JINA LA YESU, “Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA ATUKUZWE NDANI YA MWANA” (Yohana sura ya 14, mstari wa 13). Maandiko yenye uhakika pia yanatuambia “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu “(I Timotheo sura ya 2, mstari wa 5).

Viongozi wote wa dini za shetani hawauelekezi ulimwengu kwa Yesu kama Biblia takatifu inavyosema, lakini kwa wengine (miungu wa uwongo), kama vile kiongozi wa dini ya kishetani Yohane Paulo II ambaye anaiweka dunia wakfu kwa Maria, na mara zote anaonekana akipiga magoti, akiomba kwa Maria katika mguu wa sanamu yake iliyotengenezwa kwa plasta na plastiki.

Itakuwa vigumu kwangu kuthibitisha imani ya uongo ya dini hii ya kishetani ya Kirumi na mpango wake mpya wa dunia, alama elfu za nuru ya serikali, bila Neno la Mungu lisilokosea, Biblia takatifu KJV. Yeyote asomaye Biblia kamwe hawezi kuwaabudu watakatifu, Maria, papa au yeyote zaidi ya Yesu, Baba Yake, na Roho Mtakatifu.

Mashirika ya serikali (FCC, mifumo ya mahakama na shule nk.) yakiongozwa na dini ya kishetani ya Kirumi na kiongozi wake Papa yanafanya kila kitu katika uwezo wao kufutilia mbali na kuiharibu Biblia Takatifu, kwa sababu ibilisi anayeyamiliki anajua kwamba uwezekano wa kuharibu roho yako ya milele ni mzuri kama wakiweza kumng’oa Mungu, Mwanawe Kristo Yesu na Maandiko Matakatifu kutoka kwenye upeo wako. Imani zote zisizo za kweli zimethibitishwa kuwa uongo na Biblia KJV pekee.

Yesu anasema, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mathayo sura ya 11, mstari wa 28). Biblia inasema ni Yesu pekee hakuwa na dhambi, aliye safi, na hivyo anao uwezo wa kusamehe dhambi kupitia damu Yake.

Yesu pekee ndiye mwenye nguvu ya kuokoa na kuponya. Maombi yanaweza kujibiwa pale tu yanapoombwa kwa Baba katika Jina la Yesu. Yesu alisema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani” (Mathayo sura ya 28, mstari wa 18). Yesu alisema, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi” (Yohana sura ya 14, mstari wa 6). Yesu alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima, Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi” (Yohana sura ya 11, mstari wa 25).

Maria alikuwa mwenye dhambi. Alikuwa mwenye dhambi. Na baada ya Yesu kuzaliwa [Maria] alikuwa na makosa tele. Mungu anawaamuru wazazi kuwaangalia kwa makini watoto wao. Maria, akijua kwamba Yesu alikuwa Masihi, alimwacha Yesu bila ya kumwangalia kwa siku tatu. Arusini kule Kana ya Galilaya kwa ujinga aliingilia kazi ya Mwokozi na alikemewa kwa ajili ya hilo. Maria alikuwa mbali na ukamilifu na usafi. Ilimpasa Maria kuokolewa kwa neema iokoayo (nguvu) na damu ya Yesu.

Ikiwa imepotoka na kujaa makufuru dini hii ya kishetani ya “ibada ya Maria” katika dirisha maarufu kwenye makanisa makubwa ya kidayosisi ya Chartres (Chartres - Jiji lililopo Kaskazini mwa Ufaransa), yanayojulikana kama “Notre Dame de la belle verriere” (Mama yetu wa dirisha zuri la kioo lililotiwa rangi za kuona), kwa mzaha anawakilishwa na Utatu tumboni mwake kwa madhumuni ya kufanya udanganyifu wa kipepo zaidi. Katika madirisha mengine ya kioo yaliyotiwa rangi, kwa ufidhuli amekuwa akiketi pembeni mwa Mungu Baba na Mungu Mwana, hivyo kuunda Uungu wa Utatu pamoja nao wa Baba, Mwana, na “Mama Bikira,” kwa kufuru ya kumweka Maria mbele ya Roho Mtakatifu. Kuna dhambi moja isiyosamehewa, dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ambayo kwayo hakuna msamaha. “Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao” (Mathayo sura ya 12, mstari wa 32).

Ni lazima tubatizwe kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” (Mathayo sura ya 28, mstari wa 19). Maandiko yanasema wazi wazi, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, [si Maria] nawe utaokoka pamoja na nyumba yako” (Matendo sura ya 16, aya ya 31).

Maria halisi – Maria wa Biblia – alikuwa kweli amebarikiwa na Mungu, kwani alikuwa amechaguliwa na Mungu kama chombo (kitamizi) kumleta Yesu duniani kwa kuzaliwa na bikira. Hata hivyo, hajawahi kuwa, wala hana, wito mwingine wowote au nguvu za kipekee. Chukizo gani hili kwa Mtakatifu, Bwana Mwenye Enzi kuu, ambaye wazi wazi anatuonya katika Neno Lake:
“Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote: [Inamaanisha HAPANA wokovu kwa yeyote ila kwa Yesu. Hii inamjumuisha Maria.] kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” (lakini Yesu) si mwingine ikiwa ni pamoja na Maria (Matendo sura ya 4, aya ya 12).

Neno Takatifu la Mungu, mamlaka yetu ya mwisho, limeweka wazi sana kwamba Maria hana nafasi juu ya Mkristo mwingine yeyote. Maria hakutundikwa msalabani na kumwaga damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu. Ni Yesu peke yake, na katika jina lake pekee ndipo penye wokovu.

Ingawa ibada ya Bikira Maria imekuwa kwa kasi, ikimuinua juu ya viumbe wote hata juu kuliko Yesu Kristo, kumbukumbu ya awali sana, kama ya Nyaraka za Paulo, hakuna mahali zimemtaja Maria!
Ni muhimu kusisitiza upya kwamba Maria halisi wa Biblia hakuwa ​​chombo ambacho kingejitukuza nafsi yake. Badala yake, alichaguliwa kwa wema wake wa unyenyekevu na utii kwa Mungu na kumkubali Mwokozi wa kweli na mpatanishi kwa Mungu, na jina lake ni Yesu. Alikuwa “mtumishi wa kike wa Mungu” wa kawaida wa Bwana, kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe, na ilimpasa kumkubali Bwana Yesu Kristo kama Mwokozi wa nafsi yake ili aokolewe kama mtu mwingine yeyote yule. 

“Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema” (Luka sura ya 1, mstari wa 38).

Neno “mjakazi” linamaanisha “mtumwa wa kike.” Halimaanishi “malkia.” Kamwe, katika Neno la Mungu, Yesu “hakumvisha taji” Maria au kumuinua  kwenye nafasi yoyote juu ya “mjakazi wa Bwana.” Ulikuwa mfumo wa kisiasa wa Rumi ya Kikatoliki uliomvisha taji “mungu wao mwanamke Bikira Maria” kama “Malkia.” Kwa ujumla jambo hili linamhusisha na vinasaba vya Ishtar wa Babeli ya kale, ambapo  “mungu mke Mama” ni “Malkia” daima na akiwa na mamlaka kuu juu ya “Mwanawe” na wafuasi wake wote waaminifu.

Injili ya Marko inamnukuu Yesu akikataa vikali pendekezo kwamba mama Yake alikuwa na hadhi yoyote maalumu. Tazama kifungu kifuatacho:
“Na makutano walikuwa wameketi, wakimzunguka, wakamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta. Akawajibu, akasema, Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani? Akawatazama wale walioketi wakimzunguka pande zote, akasema, Tazama, mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana mtu yeyote atakayeyafanya mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu” (Marko sura ya 3, mstari wa 32-35).

Injili ya Luka inaandika kwa usahihi zaidi kukataliwa huku, katazo dhahiri la mwelekeo wowote wa kumpa heshima maalumu Maria:
“Ikawa alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya. Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika” (Luka sura ya 11, mstari wa 27-28).

Neno la Mungu kwa ufasaha linashuhudia uungu wa Yesu na kwa hakika halijawahi kuipandisha hadhi ya mama Yake. Maria hakuwahi kuitukuza hadhi yake kamwe, lakini badala yake alisema, “Moyo wangu wamtukuza Bwana” (Luka sura ya 1, aya ya 46). Maria analenga katika mwelekeo sahihi. Maandiko yote yanaelekeza kwa Yesu, na si kwa mwingine awaye yeyote. Yesu ni Mwokozi, Bwana na Mwalimu, na Mungu!! Yesu ni Alfa, Omega, mwanzo na mwisho, ufufuo, njia, na kweli, uzima. Yesu ni Neno la Mungu lililofanywa kuwa mwili. “Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, (nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee wa Baba;) amejaa neema [nguvu] na kweli” (Yohana sura ya 1, mstari wa 14). Yesu alisema, “Mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya Mimi” (Yohana sura ya 14, mstari wa 6). Kulingana na Agano Jipya, mamlaka ya mwisho, Maria hakuwa na nafasi maalum katika jamii ya awali ya Kikristo huko Yerusalemu. Matendo ya Mitume inataja tu kwa ufupi kwamba alikuwa mshiriki wa jumuiya hii (Matendo sura ya 1, mstari wa 14).

Katika Injili ya Yohana, neno kwa neno, Yesu “alimtoa mama Yake” kwa mwanafunzi wake kipenzi. Kama alivyofanya, hamuiti tena “mama,” lakini alimtaja akimaanisha “Mwanamke.” Huu haukuwa ukatili au dharau kwa upande wa Yesu, ulikuwa ni ukweli tu. Miguuni mwa msalaba, nafasi yake kama “Mama” wa Yesu ilifikia tamati:
“Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mwanamke, tazama, mwanao! Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake” (Yohana sura ya 19, mstari wa 26-27).

Kwa muhtasari, Neno Takatifu la Mungu, mamlaka ya mwisho, linathibitisha utambulisho kamili wa Maria kimaandiko na jukumu lake kama “mjakazi wa Bwana.”

1) Alikuwa bikira hadi Yesu alipozaliwa: Luka sura ya 1, mstari wa 27.
2) Baada ya kuzaliwa kwa Yesu hakuwa bikira tena bali alimzalia Yusufu watoto wengine wengi: Mathayo sura ya 13, mstari wa 55-56.
3) Alikuwa amebarikiwa kuliko wanawake wote kwa sababu tu Mungu alimtumia kama chombo ambacho kupitia hicho Yesu angekuja duniani: Luka sura ya 1, mstari wa 28.
4) Maria alimtukuza Bwana, na si nafsi yake mwenyewe: Luka sura ya 1, mstari wa 46. Wokovu ni wa Bwana: Matendo sura ya 4, mstari wa 12.
5) Maria hakuwa bikira wa kudumu. Alikuwa na wana wengine wenye majina, Yakobo, Yose, Simoni, na Yuda na mabinti kadhaa: Mathayo sura ya 13, mstari wa 55-56.
6) Uhusiano kama mama wa Yesu ulikoma pale msalabani, ambapo hamwiti tena “mama” bali “Mwanamke”: Yohana sura ya 19, mstari wa 26-27.
7) Yesu alisema anamkirimu heshima nyingi Mkristo yeyote aliyezaliwa mara ya pili, tunapolitii Neno Lake, kama alivyofanya kwa Maria. Yesu aliona mapema dini inayomwabudu Maria ya kikahaba ya mfumo wa kisiasa wa Kikatoliki, na wakati wa huduma yake hapa duniani, aliwakemea wanaosikiliza hisia zao ambao walijaribu kupanda mbegu ya ibada ya Maria: Luka sura ya 11, mstari wa 27-28, Mathayo sura ya 12, mstari wa 48-50.

Bwana wetu anatuambia kwamba kama Wakristo waliozaliwa mara ya pili tukifanya mapenzi ya Baba yetu, aliye mbinguni, tunayo ahadi kubwa kama ile ya Maria! Tunapo mkubali Bwana Yesu Kristo kama Mwokozi wetu binafsi, anaingia mioyoni mwetu kupitia Roho Mtakatifu, kama Yesu alivyofanya kwa Maria. Hili halitakufanya kuwa malkia wa mbinguni wa wanawake au ninyi wanaume kuwa mfalme wa pili wa mbinguni. Linatufanya kuwa watumishi wa Mungu waliokombolewa. Watumishi wa Mungu aliye Juu mno wanafanya kama bwana wao anavyoamuru.
Yesu alisema, “Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo” (Yohana sura ya 15, mstari wa 14).

Kama unataka kuzaliwa mara ya pili, kuwa mtumishi wa Mungu, basi ni lazima ukubali wokovu kwa vigezo vya Mungu, si vile vya uongo vya mfumo wa kisiasa, ili uweze kuingia katika ufalme wa mbinguni na si jehannamu. Vigezo vya Mungu vimeainishwa wazi katika Biblia Takatifu, na ni lazima uwe makini kuchunguza vigezo vya Mungu tu na ujiweke mbali kabisa na mafundisho yote ya uongo. Inamaanisha kukataa chochote kile. Wanaomwabudu Maria wanapaswa kuitwa wafuasi-wa-Maria na si Wakristo, Wakristo wanamwabudu Kristo siyo Maria au yeyote yule.

Neno kwa neno, Agano Jipya limeandikwa katika damu ya Yesu, si damu ya Maria au ya mtu yeyote yule. Njoo kwa Mwokozi wa kweli pekee wa roho yako sasa kwa kusali sala hii kwa muumbaji wako, Mungu aliye hai, na unapofanya hivyo, Yesu ataingia ndani ya mwili wako na kutakasa dhambi nafsini mwako kwa damu Yake. Sali sala hii:

OMBI

BWANA wangu na MUNGU wangu, ihurumie roho yangu, mimi mwenye dhambi.1 Ninaamini kwamba YESU KRISTO ni mwana wa MUNGU aliye hai. 2 Ninaamini kwamba alikufa msalabani na kumwaga damu yake ya thamani ili nisamehewe dhambi zangu zote nilizozifanya hapo awali.3 Ninaamini kwamba Mungu alimfufua YESU kutoka kwa wafu kupitia nguvu za ROHO MTAKATIFU4 na ya kuwa ameketi upande wa kuume wa MUNGU kwa wakati huu akisikiliza maungamo ya dhambi zangu na haya maombi yangu.5 Ninafungua mlango wa moyo wangu na kukukaribisha moyoni mwangu, BWANA YESU. 6 Nioshe dhambi zangu kwa damu uliyoimwaga kwa ajili ya nafsi yangu pale msalabani Kalivari,7 hutanikataa, BWANA YESU, utanisamehe dhambi zangu na kuiokoa roho yangu. Ninalijua hili kwa sababu NENO LAKO, yaani Biblia linasema hivyo.8 NENO LAKO linasema hutamkataa yeyote na mimi nikiwemo.9 Hivyo ninajua umenisikia na umenijibu; na ninafahamu kwamba nimeokoka.10 Ninakushukuru BWANA YESU kwa kuokoa roho yangu na nitaonesha shukrani zangu kwa kufanya yale unayoniamuru na kwa kutotenda dhambi tena.11

Baada ya kuokoka, YESU alisema kuwa ni lazima kubatizwa kwa kuzamishwa kabisa kwenye maji mengi kwa jina la BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU.12 Kwa makini, soma Biblia ya KJV, tafsiri ya Kiswahili ya The Bible League, Waenezaji wa Neno la Mungu tangu 1938 na ufanye inavyosema.13

BWANA anakutaka uwaambie wengine kuhusu wokovu wako. Unaweza kusambaza makala ya Injili ya mchungaji Tony Alamo. Tutakutumia makala hizi bila malipo. Tupigie simu ama ututumie barua pepe kwa habari zaidi. Mshirikishe mtu mwingine na ujumbe huu.

Iwapo unataka dunia yote, iokolewe kama YESU anavyoamuru, basi usimwibie MUNGU zaka na sadaka zake. MUNGU alisema, “Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote [na dunia hii yote]. Leteni zaka [zaka ni asilimia 10 ya mapato yako yote] kamili ghalani, ili kiwemo chakula [chakula cha kiroho] katika nyumba yangu [roho zilizookolewa], mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:8-12).


Swahili Alamo Literature

Tafadhali wasiliana nasi kwa habari zaidi au kwa vitabu vyetu vyenye mada nyingine ambazo unaweza kuvutiwa nazo:

Tony Alamo, World Pastor, Tony Alamo Christian Ministries Worldwide 

P.O. Box 2948, Hollywood, CA 90078

Namba yetu ya simu kwa ajili ya maombi na habari iliyo wazi kwa saa ishirini na nne ni: (661) 252-5686  •  Faksi: (661) 252-4362

Huduma ya Tony Alamo Christian Ministries Worldwide hutoa mahali pa kuishi pamoja na vitu vyote muhimu kwa maisha kwa wale walio Marekani ambao wanataka kumtumikia BWANA kwa mioyo yao yote, roho zao zote na nguvu zao zote.

Huduma yetu hufanyika jijini New York kila Jumanne, saa mbili usiku na mahali pengine kila usiku.

Tafadhali wasiliana nasi kupitia simu namba (908) 937-5723 kwa habari zaidi. CHAKULA HUTOLEWA BAADA YA KILA IBADA.

Tuma maombi ujipatie kitabu cha Mchungaji Alamo kiitwacho, The Messiah, kinachomwonesha KRISTO alivyo katika Agano la Kale kwa jumbe za unabii zipatazo 333.

Kuwa mmoja wa watumishi katika kuvuna roho za watu kwa kuwa msambazaji wa makala na vitabu vya Mchungaji Alamo

Machapisho yetu na jumbe kwenye tepu za sauti hayalipishwi kitu ikiwemo gharama ya kusafirisha kupitia meli.

Iwapo kuna mtu atajaribu kukulipisha, tafadhali tupigie simu kwa namba: (661) 252-5686.

MAKALA HIZI ZIMEBEBA MPANGO WA KWELI WA UKOMBOZI (Matendo ya Mitume 4:12)

USIZITUPE: ZIFIKISHE KWA MTU MWINGINE.

Kwa wale ambao mko kwenye nchi nyingine, tunawashauri kutafsiri makala hizi kwa lugha zenu. Iwapo mtachapisha tena, tafadhali jumuisha haki hii na usajili:

© Hatimiliki Novemba 1995, Machi 2012, 2015 Haki zote zimehifadhiwa Mchungaji wa Ulimwengu Tony Alamo ® Imesajiliwa Novemba 1995, Machi 2012, 2015
SWAHILI—THE QUEEN OF WHORES


Prayer footnotes:

1. Psa. 51:5, Rom. 3:10-12, 23 return

2. Matt. 26:63-64, 27:54, Luke 1:30-33, John 9:35-37, Rom. 1:3-4 return

3. Acts 4:12, 20:28, Rom. 3:25, I John 1:7, Rev. 5:9 return

4. Psa. 16:9-10, Matt. 28:5-7, Mark 16:9, 12, 14, John 2:19, 21, 10:17-18, 11:25, Acts 2:24, 3:15, Rom. 8:11, I Cor. 15:3-7 return

5. Luke 22:69, Acts 2:25-36, Heb. 10:12-13 return

6. I Cor. 3:16, Rev. 3:20 return

7. Eph. 2:13-22, Heb. 9:22, 13:12, 20-21, I John 1:7, Rev. 1:5, 7:14 return

8. Matt. 26:28, Acts 2:21, 4:12, Eph. 1:7, Col. 1:14 return

9. Matt. 21:22, John 6:35, 37-40, Rom. 10:13 return

10. Heb. 11:6 return

11. John 5:14, 8:11, Rom. 6:4, I Cor. 15:10, Rev. 7:14, 22:14 return

12. Matt. 28:18-20, John 3:5, Acts 2:38, 19:3-5 return

13. Deut. 4:29, 13:4, 26:16, Josh. 1:8, 22:5, 2 Tim. 2:15, 3:14-17, James 1:22-25, Rev. 3:18 return