KUVAMA KATIKA HUDUMA.

Nina desturi ya kulizoea na kulipenda Kanisa la Alamo. Ninajihisi kuwa sehemu ya Huduma za Mchungaji Tony Alamo. Hili ndilo kanisa pekee nililoona kuwa linahubiri Neno la kweli la Mungu. Nimekuwa katika makanisa mengi lakini sikuweza kupata ukweli halisi lakini wakati nilipoanza kusoma fasihi za Injili za Mchungaji Alamo, Mungu Wangu! Maisha yangu yalibadilika kwa kiasi kikubwa.

Nilianza maisha mapya hivi karibuni baada ya kusoma jarida moja tu; ilinitosha kubadilika. Ninawaonea huruma wale walioamua kupuuza ukweli kwa kulipinga kanisa hili. Jinsi wanavyozidi kulipinga, ndivyo wanavyozidi kuwa mbali na ni dhahiri kuwa punde watatumbukia shimoni. Nasikitika kusema kwamba huo ndio ukweli. Hebu jiulize mwenyewe kama wewe ni mmoja wao. Mungu akitwaa pumzi yake ya bure, je utakuwa pamoja Naye au utakuwa ukipiga mayowe kwa uchungu katika ziwa liwakalo moto maisha yako yote!!??

Chakula cha akili:)

Nuwaha Oscar
Mbarara, Uganda

 

tonyalamochristianministries.com